Kinachoendelea kati ya Russia na Ukraine ndo kitazaa World War III (WW3)

Kinachoendelea kati ya Russia na Ukraine ndo kitazaa World War III (WW3)

Uko low sana kwenye huu mzozo,kwa taarifa yako Russia anapigana na ulaya nzima+Amerika ni zaidi ya nchi 40,

Ukraine ni uwanja wa mapambano tu, nothing else
Vip Russia. Iran Syria North Korea au hujui nae kuna nchi nyingi tu nyuma yake
 
Nyuma ya Ukraine kuna mataifa 30 dhidi ya Mrussia wakiongozwa na Marekani. Na kila baada ya muda tunaona wakitoa vifurushi vya misaada ya kijeshi kwa Ukraine
Wiki ilopita urusi walipiga underground tunnel moja kulikuwa na top officials wa NATO huko chini wote waligeuzwa ndafu, sasa jiulize walienda kufanya nini ukraine
 
1. Mbona Putin kila mara anaitangazia Dunia kuwa anapigana na West (USA) na siyo Ukraine. Kauli hiyo karudia tena 9/5/2023. Nani tumwamini kati ya wewe na putin?

2. Ni nchi gani yenye mchango mkubwa kwa NATO?

3. Technology inayotumiwa kutengeneza military equipment za NATO ni ya nchi zipi?
Tunazunghmzia DIRECT yaani itokee Marekani kaingia na jeshi lake ardhi ya Urusi au China
 
Kama ni vita vingepiganwa miaka ya Cold War lakini haikutokea kilichoiangusha Soviet Union ni kuporomoka kwa uchumi na mbinu za kijasusi za NATO.

Marekani na Urusi haitatokea zikapigana direct hata siku moja hizo ni story tu za vijiweni
Hazitapigana sababu Russia hawezi vamia Marekani ila Marekani ana uwezo huo
 
..makombora yanayorushwa na Russia yatakayosababisha ajali ktk mitambo ya umeme wa nyuklia iliyoko Ukraine.

..kwa hali inavyoendelea nadhani ni suala la muda tu kutakuwa na ajali mbaya ya kihistoria Ukraine na ajali hiyo itapelekea vita kusimama / kusitishwa / kuisha.
Unafuatilia mambo mkuu? Yaani Urusi apige makombora kwenye mitambo anayoishikilia na kuisimamia mwenyewe?!

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Analysts wa masuala ya kivita, wanasema uwezo wa kivita wa Urusi ulikuwa exagerated.

Russia alipoivamia Ukraine, hakuma nchi iliyojitokeza kuisaidia Ukraine aina yoyote ya silaha kutokana na hofu ya mataifa mbalimbali juu ya uwezo mkubwa wa kivita wa Russia. Na hakuma nchi hata moja iliyoamininkuwa Ukraine ingetoa upinzani wa kivita kwa Russia.

Ni mpaka pale Ukraine ilipoweza kuizuia Russia kufanikisha mipango yake na kusababisha vifo vingi vya askari wa Urusi, ndipo mataifa mengine wakaona, kumbe inawezekana Ukraine kutoa upinzani kwa Russia. Mataifa mengi yakaanza kutoa misaada mbalimbali ya silaha za kivita kuisaidia Ukraine.

Ukweli vita hii imeianika wazi sana Urusi, na kuonekana kuwa kumbe nguvu ilizokuwa inafikiriwa Urusi inazo, haina kwa kiwango hicho.

Mataifa ya Magharibi yanazidi kuipa silaha Ukraine ili kuilazimisha Urusi kumaliza stock yake ya silaha. Sasa Urusi imelazimika kutumia mpaka silaha zilizotumika wakati wa vita ya pili ya Dunia.

Kwa upande mwingine, uchumi wa Urusi ambao ulikuwa tayari unalegalega, ambao ulifikia hatua mpaka kusaidiwa na mataifa ya Magharibi, sasa lazima utatikisika sana. Mataifa ya Ulaya yanatoa ziada kuisaidia Ukraine, Russia analazimika kutumia kile anachokihitaji sana kwa maendeleo ya wananchi wake. Vijana wasomi na wataalam wa Urusi wanakimbilia nchi za Magharibi kuogopa athari za kiuchumi na kulazimishwa kwenda mstari wa mbele kupigana vita. Haya yote, baada ya muda yatauumiza sana uchumi wa Russia.

Russia kwa sasa nguvu pekee iliyobakia nayo ni makombora ya nuklia, lakini kwa silaha nyingine na uwezo wa kupigana, haina tofauti na mataifa mengi ya Ulaya. Siyo tishio tena kwa nchi yoyote kwenye masuala ya uwezo wa kivita.
Umevuta majani gani? We mtu anazidi kuongeza maeneo anayomiliki kwenye nchi yako halafu unamuona how come tuu?!

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Urusi inakwenda kushindwa vita, urais wa Putin unategemea matokeo ya vita hiyo. Very likely atapinduliwa / kuuawa.

Hilo ni miongoni mwa mambo yanayowaumiza vichwa mataifa ya magharibi, Putin wanamjua vizuri, akiondokewa ghafla anaweza kuibuka kiongozi mwingine ambaye ni kichaa zaidi akaikuza vita mpaka kwenye matumizi ya silaha za nyuklia.

Ndio maana hawaipi Ukraine kila kitu, hawataki ishinde kwa kishindo na ghafla kiasi cha kuupasua uongozi wa Putin, wanataka idhoofishe Urusi mpaka ikubali majadiliano ya amani.
Nyie mnafuatilia habari wapi? Haujasikia hata jana katibu wa baraza la usalama la Ukraine Oleksiy Danilov analalamika wanapata presha kubwa sana kutoka viongozi mbalimbali wa Ulaya na dunia ya kuanzisha mazungumzo ya amani na Urusi tena "on Russian terms"?!

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Hapa tunachoweza kuangalia ni indicators! Kwasasa mataifa ya ulaya yanasukumwa mno na Marekani katika kufanya maamuzi kuliko kutumia uhuru wa kuchagua eidha wafanye au wasifanye! Hiki kitu kinawakera sio kama stor tu! Unahis kauli ya macron kuwa Ulaya sio kibaraka wa Marekan ni mshirika hivo Marekan wasiwapeleke peleke tu inatokana na nn? Angela Merkel pamoja na Macron miaka ya 2018 waliwah kutoa wazo kuwa Ulaya iwe na jeshi lake la muungano lisilo na Marekani wakimaanisha nn? Walienda mbali zaid na kusema jeshi litakalo weza kuikabili Urusi na marekan wakileta uchokozi! Ni indicators tu brother zinaonyesha ulaya kuchoshwa na na mshirika wao Marekani
Hata hivi karibuni raisi wa Ufaransa Macron alizungumzia jambo hilohilo
 
Hamna kitu. Nato uwezo wao wa kisilaha hauwezi kumfikia mrussia. Tatizo marekani ana brag sana kuhusu military equipment zake ila Urusi huwezi kuta anaongea au kuonyesha kwa mbwe mbwe utashangaa tu mzigo huo apo uwanjani.

Nadhani ni swala la muda mtaelewa. Sijui huwa mnatazama vyombo gani vya habari.
It's has been more than a year! Hamna kitu pale, wamefikia mahali wananunua silaha toka Iran na South Africa.
 
Mwanaume yuko Kaskazini anapambana na Mataifa 30 tena yenye nguvu na vikwazo juu. Mpeni respect Russia asee.

Hivi US angevaa uhusika wa Russia angetoboa hata mwezi tu??
 
Tangu Putin atangaze Special Military operational yake Feb 2022 dhidi ya Ukraine, wengi waliamini kuwa huo ndo ulikuwa mwanzo wa vita kuu ya tatu (World War III) hasa Marekani na NATO walipoweka wazi kuwa wataisaidia silaha Ukraine ili iweze kujilinda dhidi ya mvamizi (Russia).

Marekani alipozishawishi nchi za EU kuisaidia Ukraine, fikra za WW3 ndo zilikolea kwa watu wengi (Pro-Russia na Pro-Ukraine).

Kinachoendelea sote tunaofuatilia vita hiyo tumekiona na tunajua, sina sababu ya kueleza.

Waliokuwa wakiamini kuwa hiyo vita ni mwanzo wa WW3 walikuwa na sababu muhimu zifuatazo;

1. Waliamini kuwa Russia ni super power na kwamba ina uwezo wa kupiga nchi zote ikiwemo marekani.

2. Waliamini vita ya Russia na Marekani itakuwa vita ngumu sana na wengine wakaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa Marekani akiingilia ugomvi wa Russia na Ukraine ndo utakuwa mwanzo wa Marekani kupigwa na kusambaratishwa na super power aitwaye Russia.

3. Pro Russia na hata viongozi wa Russia waliamini kuwa Russia ina uwezo wa kumpiga Marekani kwa makombora yake anayoyaitwa Intercontinental Ballistic missiles, Hypersonic missiles na Nuclear missiles. Eti Kwamba Russia makombora yake ni hatari sana na ya technology ya hali ya juu sana.

4. Sababu nyingine ni kwamba waliamini kuwa Russia ana air defense systems hatari sana wakiwa wanarejea S-300 na S-400 series. Kwamba anga la Urusi linalindwa sana huwezi kupenya na kwamba marekani hana air defense systems kama za Russia.

Katika kutafakari na kufanya assessment kuhusu hali halisi ya kinachoendela katika vita ya Ukraine na Russia. Tunahitaji kujua kama kweli watu walichokuwa wanafikilia kimekuwa kweli au kimeenda kinyume chake kwa kujiuliza maswali yafuatayo.

1. Je, bado tunaamini kuwa vita ya Ukraine na Russia itazaa vita kuu ya tatu ya Dunia (World War III) ?

2. Ni kweli Russia ni supper power kama watu walivyoamini kabla ya vita kuanza ?

3. Ni kweli Russia ana uwezo wa Kuipiga Marekani na nchi zingine Duniani na pengine kuitawala Dunia.

4. Ni kweli Russia and air defense systems za hatari kuliko marekani na nchi yoyote duniani na kwamba anga lake liko salama hakuna kitu cha kupenya kwenye anga lake?

5. Ni kweli Russia ana silaha nzito za kutisha na zenye kutumia technology kubwa kuliko marekani na nchi zingine?

6. Ni kweli jeshi la Russia liko imara sana kama ambavyo tuliamini mwanzo na kwamba wana mafunzo imara ya kutumia silaha za kivita?

Tupate maoni na tafakari yenu bila matusi na ushabiki usio na hoja yenye mantiki. Tusitawaliwe na u pro-Russia au Ukraine tukajikuta tumetoka kwenye hoja.
Hii vita itamalizwa kwa Russia kufanya mashambulizi makali na ambayo hayajawahi kutokea.

Mashambulizi hayo ya Russia yatasababisha vifo vya askari wengi wa pande zote lakini ni Ukraine ndo wataopotea zaidi.

Vita hii yaonekana itakuwa imeisha mwanzoni mwa Julai au mwanzoni mwa mwezi August 2023.

Itabidi itumike "Wild Card" kwa Poland ambayo itategemea watachukulia vipi ushindi wa Russia, hivyo Poland itaamua kuitangaza Ukraine (Upande wa Magharibi ikiwemo Kyiv) kuwa sehemu yake.

Mimi kwa mawazo yangu ni kwamba kama Ukraine ingekuwa ni nchi kamili bila kutokea USSR na haina support yoyote ya NATO na hila za US ningekuwa niko pamoja nae.

Lakini kwa kuwa ameamua kutumika kwa ajili ya kuidhoofisha Russia na kutishia usalama wa Russia, hapo siiungi mkono Ukraine.

Uharibifu, vifo vya vijana wengi, wake kwa waume na watoto vyote vimebaki akutofaidisha upande wowote.

Hivyo suala ni Russia na Ukraine kuketi na kuchora ramani mpya na kila nchi ikae na ilivyo sasa.

Russia haiwezi kuiachia Crimea ambayo ni US ndo wanoitaka ili wajenge kituo cha kijeshi hapo kwenye Bahari Nyeusi, na Russia haiko tayari kuona hiyo ikitokea.

Pia Russia haiwezi kuachia kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia ambacho kama Ukraine yabaki nacho itakuwa ni tishio kwa usalama wa Russia.
 
Mkuu kwa jinsi wamagharibi walivo na .n..y..e..g.. mshindo, kama mrusi ni dhaifu basi kwa sasa mda mrefu wangeshakiwasha na kuondoka,ila mzee hii ngoma nzito mana juzi wenyewe wamekili kuzidi kuitenga urusi ni kujiumiza wenyewe,
Ukweli ndio huo

Dhaifu wote walivamiwa wakapigwa.

Kwanini dhaifu huyu anaogopwa kuvamiwa.

Mimi natamani sana hii vita iishe iwe kupigwa Russia au kupigwa Ukraine

Au kupatanishwa muhimu tu nataka iishe.
 
Uzi umejaa hisia tu.mleta Uzi una mapenzi ya upande wa west ila umejificha kichaka Cha karanga....
 
Analysts wa masuala ya kivita, wanasema uwezo wa kivita wa Urusi ulikuwa exagerated.

Russia alipoivamia Ukraine, hakuma nchi iliyojitokeza kuisaidia Ukraine aina yoyote ya silaha kutokana na hofu ya mataifa mbalimbali juu ya uwezo mkubwa wa kivita wa Russia. Na hakuma nchi hata moja iliyoamininkuwa Ukraine ingetoa upinzani wa kivita kwa Russia.

Ni mpaka pale Ukraine ilipoweza kuizuia Russia kufanikisha mipango yake na kusababisha vifo vingi vya askari wa Urusi, ndipo mataifa mengine wakaona, kumbe inawezekana Ukraine kutoa upinzani kwa Russia. Mataifa mengi yakaanza kutoa misaada mbalimbali ya silaha za kivita kuisaidia Ukraine.

Ukweli vita hii imeianika wazi sana Urusi, na kuonekana kuwa kumbe nguvu ilizokuwa inafikiriwa Urusi inazo, haina kwa kiwango hicho.

Mataifa ya Magharibi yanazidi kuipa silaha Ukraine ili kuilazimisha Urusi kumaliza stock yake ya silaha. Sasa Urusi imelazimika kutumia mpaka silaha zilizotumika wakati wa vita ya pili ya Dunia.

Kwa upande mwingine, uchumi wa Urusi ambao ulikuwa tayari unalegalega, ambao ulifikia hatua mpaka kusaidiwa na mataifa ya Magharibi, sasa lazima utatikisika sana. Mataifa ya Ulaya yanatoa ziada kuisaidia Ukraine, Russia analazimika kutumia kile anachokihitaji sana kwa maendeleo ya wananchi wake. Vijana wasomi na wataalam wa Urusi wanakimbilia nchi za Magharibi kuogopa athari za kiuchumi na kulazimishwa kwenda mstari wa mbele kupigana vita. Haya yote, baada ya muda yatauumiza sana uchumi wa Russia.

Russia kwa sasa nguvu pekee iliyobakia nayo ni makombora ya nuklia, lakini kwa silaha nyingine na uwezo wa kupigana, haina tofauti na mataifa mengi ya Ulaya. Siyo tishio tena kwa nchi yoyote kwenye masuala ya uwezo wa kivita.
Kumbuka hiyo ni SMO na sio war!Putin anasema hajaanza anything serious hapo Ukraine!
Hizo nyingine ulizoleta hapa ni ngonjera tu!
Hao hao analyst wa west walituzuga kuwa Urusi hana uwezo wa kuendesha SMO miezi 3,hao hao walisema Russia kaishiwa silaha miezi ya mwanzo ya SMO!Imekuja kubainika ni tofauti,so hizo porojo ni propaganda tu kuidiscourage Russia!
 
Nope, Urusi angekuwa kwenye vita na NATO hata wiki asingemaliza. Anga lote lingefungwa.

Kwa kifupi NATO wameona udhaifu wa Urusi wemeamua kuimaliza indirectly. Wangeamua kuwapa kila kitu Ukraine basi vita ingeshaisha asubuhi na mapema.

Wanaozijia vizuri silaha za NATO wanatambua kuwa Ukraine kapewa basic necessities tu, kikubwa sana anachopewa na intelligence.
Wanaimalizaje indirectly wakati uchumi wao ndio uko hoi bin taaban?Libya alikuwa member wa NATO?Mbona waliingia mazima?
Yaani west wako tayari kuona maelfu ya watu wa Ukraine wakifa kila siku Ili kummaliza Russia indirectly?Kwanini wasiimalize vita mapema kunusuru vifo vingi vinavyotokea kila siku?
Russia sio Zimbabwe,US na NATO wanalijua Hilo ila wewe pro NATO wa Tandahimba unajua tofauti!
 
Hoja yako nimeielewa na una hoja.
1. Kwamba NATO na USA hawataki kumaliza vita hii mapema ili wamdhoofishe kwanza Russia kiuchumi na military power taratibu.

2. Kwamba, USA na NATO hawataki kumpa Ukraine silaha nzito. Ukiwa unamaanisha kuwa USA na NATO wana silaha nzito kuliko Russia.

3. Hili la Putin kupinduliwa huenda ndo maana 9/5/2023 iliitangazia dunia kuwa anataka kupinduliwa na west akiwa na maana ya USA.
Hahahaaaaaa,Nyie jamaa mnajikuna na kucheka wenyewe!
 
Kitendo Cha kushindwa kuipiga Ukraine ndani ya masaa24 walioahidi wenyewe wenye akili tushajua nguvu Yao ipoje
Walikuahidi wapi?Unaweza kuweka source ya habari Yako?Wenzako tumeshawaomba Toka mwaka Jana watupe source lakini wameshindwa na imebaki ni porojo tu za hapa na pale!Hizi propaganda mfu hazibadili chochote uwanja wa mapambano!
 
Nope, Urusi angekuwa kwenye vita na NATO hata wiki asingemaliza. Anga lote lingefungwa.

Kwa kifupi NATO wameona udhaifu wa Urusi wemeamua kuimaliza indirectly. Wangeamua kuwapa kila kitu Ukraine basi vita ingeshaisha asubuhi na mapema.

Wanaozijia vizuri silaha za NATO wanatambua kuwa Ukraine kapewa basic necessities tu, kikubwa sana anachopewa na intelligence.
Ni mpuuzi pekee atafikiri wababe hawa wakae sehemu moja kisha utoke salama. US, UK, German, France, Italy. Hasa hasa US na UK. Huko kuna watu bright kweli kweli hasa ktk Inteligence. Hapo weka mbali washirika wao wa mbali kama Israel, Japan n.k hizo Race za Asia nazo ni vichwa kweli kweli.

Tukumbuke pia US mpaka Warusi wapo, Wachina n.k. Watu wanachukulia simple uwezo wa US ktk nyanja nzima ya Tec na Vita.
 
Back
Top Bottom