Analysts wa masuala ya kivita, wanasema uwezo wa kivita wa Urusi ulikuwa exagerated.
Russia alipoivamia Ukraine, hakuma nchi iliyojitokeza kuisaidia Ukraine aina yoyote ya silaha kutokana na hofu ya mataifa mbalimbali juu ya uwezo mkubwa wa kivita wa Russia. Na hakuma nchi hata moja iliyoamininkuwa Ukraine ingetoa upinzani wa kivita kwa Russia.
Ni mpaka pale Ukraine ilipoweza kuizuia Russia kufanikisha mipango yake na kusababisha vifo vingi vya askari wa Urusi, ndipo mataifa mengine wakaona, kumbe inawezekana Ukraine kutoa upinzani kwa Russia. Mataifa mengi yakaanza kutoa misaada mbalimbali ya silaha za kivita kuisaidia Ukraine.
Ukweli vita hii imeianika wazi sana Urusi, na kuonekana kuwa kumbe nguvu ilizokuwa inafikiriwa Urusi inazo, haina kwa kiwango hicho.
Mataifa ya Magharibi yanazidi kuipa silaha Ukraine ili kuilazimisha Urusi kumaliza stock yake ya silaha. Sasa Urusi imelazimika kutumia mpaka silaha zilizotumika wakati wa vita ya pili ya Dunia.
Kwa upande mwingine, uchumi wa Urusi ambao ulikuwa tayari unalegalega, ambao ulifikia hatua mpaka kusaidiwa na mataifa ya Magharibi, sasa lazima utatikisika sana. Mataifa ya Ulaya yanatoa ziada kuisaidia Ukraine, Russia analazimika kutumia kile anachokihitaji sana kwa maendeleo ya wananchi wake. Vijana wasomi na wataalam wa Urusi wanakimbilia nchi za Magharibi kuogopa athari za kiuchumi na kulazimishwa kwenda mstari wa mbele kupigana vita. Haya yote, baada ya muda yatauumiza sana uchumi wa Russia.
Russia kwa sasa nguvu pekee iliyobakia nayo ni makombora ya nuklia, lakini kwa silaha nyingine na uwezo wa kupigana, haina tofauti na mataifa mengi ya Ulaya. Siyo tishio tena kwa nchi yoyote kwenye masuala ya uwezo wa kivita.
Nina wasi wasi na vyanzo vyako vya taarifa hizi unazosema hapa.
Hizi ni taarifa ambazo utazikuta CNN, BBC news, Sky News, DW, na channel zinginezo za mataifa ya magharibi ambazo hushirikiana kupotosha juu ya mambo yanayoendelea huko Ukraine.
Ukitaka kubalance facts tazama RT, tazama CGTN na zingine ni za uarabuni ngumu kuzipata kwenye ving'amuzi vyetu hivi local.
Kimsingi mataifa ya magharibi tokea mwanzo wa hii vita walishaanza kuipa silaha Ukraine na hii ilionekana kwa ushahidi wa silaha nyingi used ambazo zilitoka marekani ambazo zilitoka kwenye maghara yake ya silaha zilizokamwatwa na polisi kwenye matukio mbali mbali.
Hii ilijulikana baada ya Urusi kuzikamata eneo la vita na kutrace history ya license na kukuta nyingi zilishamilikiwa US.
Jambo lingine ufahamu ni kuwa Urusi uchumi wake ni wa kijamaa. Mataifa ya kijamaa huwa hayaathiriwi na maswala ya kibiashara sababu serikali ndio inasimamia uchumi kwa asilimia kubwa na kucontrol mahitaji.
Uchumi wa Urusi ni ngumu sana kupitia mushkeri sababu hata pesa yake haipo sana kwenye soko la Dunia na yeye ana fanya biashara na baadhi ya mataifa ya magharibi sio yote na hata sasa baada ya kuzinguliwa amehamisha ushirika wake wa kibiashara anashirikiana na mataifa ya BRICS na pia mataifa washirika kama ya kiarabu, uturuki etc hivyo hakuna cha kumteteresha.
Marekani ni taifa ambalo nguvu yake anategemea kudhoofu wengine ndipo yeye awe imara. Yaani mfano wake ni kama hapa Tanzania, CCM wanadhoofisha elimu ili raia wawe wajinga wasiweze kuelimika na kuongeza ufahamu, hawapendi raia kukuza mitaji na ndio maana TRA na mamlaka zingine za serikali zipo macho zana kudidimiza ukuaji wa makampuni ya ndani huku ya nje yakija yanafanya kila yanachojisikia kwa uhuru, hawapendi raia waendeleze miundo mbinu ili kila mwaka wa uchaguzi waje na sound zile zile za "tutajenga barabara".
Marekani safari hii amekalia kuti kavu maana ingawa anapigana hii Proxy War na Russia ila anajua kuwa hali yake ni mbaya anahangaika sana na mataifa wameshitukia. Dollar inapungua kwenye uchumi wa Dunia kidogo kidogo sababu inaleta shida sana kwenye chumi za mataifa yanayotaka kukua kiuchumi kama china sababu ya vikwazo vya kipumbavu.
Washirika wa marekani yaani UK, France, Canada, na wengineo hali zao si nzuri kama miaka yote na hii vita inazidi kuwafilisi kiuchumi.
Tazama maandamano ya ufaransa unaona hata hivi vyombo vya magharibi wanaonyesha?
Tafuta watu wanaoishi mataifa ya ulaya na Marekani waulize hali ipoje huko utasikia watakwambia namna hali ni mbaya na wanavyoishi kwa bajeti ya siku hadi siku.