- Thread starter
- #61
Hoja zako zimeeleweka murua hujatoka nje ya hoja.1. Kuhesabu idadi ya nchi Russia anazopigana nazo haileti maana sana(It doesn't hold water) kwani kinachoangaliwa hapo ni Objective achievement i.e. umeshinda au umeshindwa vita?
2. Ni kweli Ukraine ni uwanja wa mapambano na uwanja huo aliyeuandaa ni Russia mwenyewe. Kama wajanja waliitumia Ukraine kama chambo, basi Mrusi alimeza chambo. Mrusi kwa bahati mbaya sana hakuzisoma alama za nyakati. Yan Mrusi hawezi kujitoa ufahamu na kudai kwamba hakujua kitakachotokea endapo atatekeleza kile alichokiita ni SMO. Otherwise tukubaliane kwamba Inteligensia yake ni very inferior and rudimentary.
3. Hakuna tena kitisho cha uwezekano wa kuwapo kwa WW111 kwa sababu vita (mapambano) inaelekea ukingoni kwani wapiganaji Warusi wengi hawana usongo/hamu tena na vita hiyo isiyo na malengo. Lakini zaidi wapiganaji wabobezi( Long experienced) fighters walishauawa. Waliopo ni hawa wenye elimu lakini hawana uzoefu kazini. e.g. Hata wababe (Wagners) nao hilo wameliona.
4. Maadui wa Mrusi inaonekana wameongezeka na wamesambaa wapo nje na ndani ya Urusi kwenyewe kitu ambacho kinamchanganya akili na wakati huo huo washirika wake wanasua-sua kutoa misaada e.g. Putin mwenyewe analalamika (hotuba ya tar.09/05/2023) eti watu wake wanataka kumpindua.
1. Hakuna uwezekano wa WW3 kwa sababu vita iko ukingoni kuisha. Kwamba aliyeanzisha vita (Russia) hana mzuka (motivation) tena. Kwa nyongeza ya hoja yako, pia tulimsikia aliyeanzisha vita (Russia) anaomba mazungumzo ya kumaliza vita. Hivyo uwezekano wa WW3 haupo kwa mantiki hiyo.
2. Kwamba aliyeanzisha vita (Russia) hakujua nguvu ya kijeshi atakayokutana nayo kutoka kwa adui (Ukraine). Kwamba hoja ya u super power imefifishwa na nguvu ya kijeshi aliyokutana nayo sababu ali undermine.
3. Kumpindua supper power si jambo jepesi. Lakini 9/5/2023 Dunia ilitangaziwa na super power (Putin) kuwa anataka kupinduliwa na West na akaongeza kwamba maadui wako ndani ya nchi yake. Hili nalo ninafifisha hoja ya supper power kuitawala Dunia kama tulivyoaminishwa huko nyuma. Kama ni super power hofu hiyo inatoka wapi?