Analysts wa masuala ya kivita, wanasema uwezo wa kivita wa Urusi ulikuwa exagerated.
Russia alipoivamia Ukraine, hakuma nchi iliyojitokeza kuisaidia Ukraine aina yoyote ya silaha kutokana na hofu ya mataifa mbalimbali juu ya uwezo mkubwa wa kivita wa Russia. Na hakuma nchi hata moja iliyoamininkuwa Ukraine ingetoa upinzani wa kivita kwa Russia.
Ni mpaka pale Ukraine ilipoweza kuizuia Russia kufanikisha mipango yake na kusababisha vifo vingi vya askari wa Urusi, ndipo mataifa mengine wakaona, kumbe inawezekana Ukraine kutoa upinzani kwa Russia. Mataifa mengi yakaanza kutoa misaada mbalimbali ya silaha za kivita kuisaidia Ukraine.
Ukweli vita hii imeianika wazi sana Urusi, na kuonekana kuwa kumbe nguvu ilizokuwa inafikiriwa Urusi inazo, haina kwa kiwango hicho.
Mataifa ya Magharibi yanazidi kuipa silaha Ukraine ili kuilazimisha Urusi kumaliza stock yake ya silaha. Sasa Urusi imelazimika kutumia mpaka silaha zilizotumika wakati wa vita ya pili ya Dunia.
Kwa upande mwingine, uchumi wa Urusi ambao ulikuwa tayari unalegalega, ambao ulifikia hatua mpaka kusaidiwa na mataifa ya Magharibi, sasa lazima utatikisika sana. Mataifa ya Ulaya yanatoa ziada kuisaidia Ukraine, Russia analazimika kutumia kile anachokihitaji sana kwa maendeleo ya wananchi wake. Vijana wasomi na wataalam wa Urusi wanakimbilia nchi za Magharibi kuogopa athari za kiuchumi na kulazimishwa kwenda mstari wa mbele kupigana vita. Haya yote, baada ya muda yatauumiza sana uchumi wa Russia.
Russia kwa sasa nguvu pekee iliyobakia nayo ni makombora ya nuklia, lakini kwa silaha nyingine na uwezo wa kupigana, haina tofauti na mataifa mengi ya Ulaya. Siyo tishio tena kwa nchi yoyote kwenye masuala ya uwezo wa kivita.