Utakuwa mjinga hasa kama huwezi kuongelea haki na uhuru wa watu. Hakuna kinachozidi hayo.
Unajenga barabara, hospitali, madaraja, reli n.k. kwaajili ya nani? Ni kwaajili ya watu. Kama unawaonea watu, unawateka, unawatesa, unawabambikia kesi, unawabagua, unawapendelea baadhi, unawaua au kuwapoteza, au wengine kuwashambulia kwa risasi, hivyo vitu unavyotengeneza vitakuwa na msaada gani kwao?
Kwa mfano leo hii ukaenda kwenye familia ya watu wenye akili timamu, ukawauliza, mnataka nini - niwaletee maji mpaka hapa nyumbani halafu mmoha kati yenu apotee au niwaache muendelee kutemvea kilometa moha kufuata maji lakini ninyi nyote muendelee kuishi kwa uhuru wenu, unatarajia kupata jibu gani?
Wapinzani wapo sahihi sana. Wanaongelea zaidi juu ya uhuru na haki za watu. Sasa huwezi kuongelea kurejesha haki na uhuru wa watu bila ya kumtaja aliyewapokonya. Na kwa udhahiri kabisa, serikali ya awamu hii ndiyo iliyopokonya haki na uhuru wa watu. Ndiyo iliyotunga sheria gandamizi. Ndiyo iliyowafanya viongozi kuwa na kiburi cha ajabu cha madaraka ambacho hakijawahi kushuhudiwa.