Uchaguzi 2020 Kinachoendelea kwenye kampeni za CHADEMA ni kueneza chuki dhidi ya Magufuli na sio kunadi Sera na Ilani ya chama chao

Uchaguzi 2020 Kinachoendelea kwenye kampeni za CHADEMA ni kueneza chuki dhidi ya Magufuli na sio kunadi Sera na Ilani ya chama chao

Kwani inakuaje Tundu asijue taratibu za kisheria?

Wakati serikali ilipokua inashughulikia swala lake la kupigwa risasi akiwa kwenye matibabu nyie hamkumbuki alifanya nini? Alitafutwa dereva kusaidia upelelezi hakupatikana na badala yake Tundu mwenyewe akaanza kupita BBC, al jeezera, Dutchweller na kwingine kuwaambia amepigwa risasi na Magufuli na kwamba Tanzania sio sehemu salama huku akijua kabisa utaratibu wa shauri likiwa kwenye upelelezi.

Najiuliza kama anamjua aliyempiga risasi kwanini hadi sasa hajamfungulia kesi?
Na kilichomshawishi kurudi sehemu ambayo sio salama ni nini?

Kupigwa risasi Tundu iliniumiza kama ilivyowaumiza wananchi wengi lakini kusema kwamba rais Magufuli alihusika ni mawazo hafifu sana sababu kwa mamlaka aliyo nayo rais kama mtu ametenda makosa ziko njia njia nyingi za kudeal nae sio risasi

Bado naamini vyombo vya usalama vitalifanyia kazi kwa taratibu za nchi na weledi, kwa hiyo afate taratibu ili apate kitu sahihi cha kuongea. Rais hawezi kujibu jambo lililo kwenye vyombo vya sheria
 
Tatizo lenu mmeshazoea kusikia maneno matamu ya kuwapendeza. Mtu akiongea kwa kuwakosoa au kuonesha madhaifu ya magu mnasema kajawa na chuki.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Kwani inakuaje Tundu asijue taratibu za kisheria?

Wakati serikali ilipokua inashughulikia swala lake la kupigwa risasi akiwa kwenye matibabu nyie hamkumbuki alifanya nini? Alitafutwa dereva kusaidia upelelezi hakupatikana na badala yake Tundu mwenyewe akaanza kupita BBC, al jeezera, Dutchweller na kwingine kuwaambia amepigwa risasi na Magufuli na kwamba Tanzania sio sehemu salama huku akijua kabisa utaratibu wa shauri likiwa kwenye upelelezi.

Najiuliza kama anamjua aliyempiga risasi kwanini hadi sasa hajamfungulia kesi?
Na kilichomshawishi kurudi sehemu ambayo sio salama ni nini?

Kupigwa risasi Tundu iliniumiza kama ilivyowaumiza wananchi wengi lakini kusema kwamba rais Magufuli alihusika ni mawazo hafifu sana sababu kwa mamlaka aliyo nayo rais kama mtu ametenda makosa ziko njia njia nyingi za kudeal nae sio risasi
Kuhusus suala la dereva dpp wa tanzania alitakiwa kumuandikia dpp wa ubelgiji akimuomba kumuhoji dereva atoe taarifa na hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya proceeds of crime act
Nani afunguliwe kesi?
 
Chagu, furaha ya mtu hainunuliwi wala kulazimishwa. Mwanzoni wafuasi wa Ccm mlidai kuwa Cdm imekufa. Hii ni baada ya kuwafika bei baadhi yao na wengine mamluki mliowatuma humo. Lakini wananchi wamewaprove wrong . Kuwa Cdm ipo na ipo mioyoni mwao.

Hiki ni kipindi cha campaign, mwacheni kila mgombea ajinadi kwa njia anayoiona ni sahihi kwake. Lissu jana amezungumza almost 40 minutes na alizungumzia matatizo ya watu wa kanda ya ziwa eg. Kilimo cha pamba, matatizo ya wavuvi kufirisiwa na kuchomewa mali zao, ajira kwa vijana nk. Na alitumia kama dk 3 kuzungumzia mambo ya kupigwa kwake risasi. So acha watu waombwe kura.

Ungelaumu vyombo vya matangazo ningekuelewa
Jaduong hivi kampeni za Cdm ya Dk Slaa 2010 unaweza kulinganisha na hizi za leo? Ok anatetea wavuvi kuwa wanaonewa ina maana anataka uvuvi haramu uruhusiwe? Anataka sheria ya uvuvi isifuatwe?
Suala la ajira ni suala gumu. Anadhani serikali inaweza kuajiri wananchi wake wote? Hata Ccm wanatambua hilo ndio maana wanasisitiza watu kujiajiri. Nenda Nigeria mtu ana Phd lakini mama ntilie. Na hao ni wengi tu.
 
Kuhusus suala la dereva dpp wa tanzania alitakiwa kumuandikia dpp wa ubelgiji akimuomba kumuhoji dereva atoe taarifa na hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya proceeds of crime act
Nani afunguliwe kesi?
DPP anajua zaidi yetu
Ndio maana nikasema tuwaachie vyombo vya usalama wao watalifanyia kazi kwa taratibu za nchi na weledi
 
Uzi wowote ukimgusa Lissu unapanda fasta, ukitaka udode ongelea wengine
 
Anapoteza muda. Watanzania wengi hatujui maumivu ya risasi. Anajua yeye na ujinga wake. Na uchaguzi huu anasindikiza tu.
Kha Lihakanga hili ni jibu la watani😁😁😁😁
Maana watani hamchaguagi tukio wala sehemu ya kufanyia utani
 
Mmefanya siasa miaka mitano bila bugudha.... tulieni, ni siku 62 tu
 
Siasa ni game of advantages. Kumbuka Polepole aliwaita wapinzani ni kama virusi vya Korona. Raisi JPM alilokuwa Kilwa, Kilosa alivyoongea kuhusu Wapinzani n.k

Tatizo ni kwamba CCM mlimaliza maneno yote kwenye Miaka mitano.

Hawa mliwazuia sasa maneno yao wanayo kwa kuwa hawakuwa na pa kuyasemea.

Sasa mmewaruhusu na wao ndio wanayatoa.
 
Me nafikiri washauri wake hawako vizuri au hautaki urais?? Kapewa hiyo nafasi ili amrushie maneno mwenzie???

Kwa stail hii no kazi sana nafikiri Chadema ijikite zaidi kwenye kueneza Sera na sio kushambulia na mikoa hii ndo muhimu sanaaaa jamaa likienda huko linamwaga sumu wanasahau yote ya nyuma
Mgombea kumwambia mgombea mwingine ajitoe kwa ahadi ya kupewa ajira ndogondogo ni kipengele namba ngapi kwenye Sera za CCM?
 
Wazee wa kakazi kadogo.... Msimu huu mmepatikana[emoji23]
 
Siasa ni game of advantages. Kumbuka Polepole aliwaita wapinzani ni kama virusi vya Korona. Raisi JPM alilokuwa Kilwa, Kilosa alivyoongea kuhusu Wapinzani n.k

Tatizo ni kwamba CCM mlimaliza maneno yote kwenye Miaka mitano.

Hawa mliwazuia sasa maneno yao wanayo kwa kuwa hawakuwa na pa kuyasemea.

Sasa mmewaruhusu na wao ndio wanayatoa.
Maneno yote yameisha? Huyo Lissu mwenyewe ametoka Belgium kafika Singida anashangaa mataa ya barabarani na traffick lights anadhani yupo bado Belgium.
 
Ajibu maswali hatutaki blabla hiyo airport ya msituni inamsaidiaje mlalahoi wa geita au kuanikia unga na mazao?
 
Back
Top Bottom