Uchaguzi 2020 Kinachoendelea kwenye kampeni za CHADEMA ni kueneza chuki dhidi ya Magufuli na sio kunadi Sera na Ilani ya chama chao

Uchaguzi 2020 Kinachoendelea kwenye kampeni za CHADEMA ni kueneza chuki dhidi ya Magufuli na sio kunadi Sera na Ilani ya chama chao

Me nafikiri washauri wake hawako vizuri au hautaki urais?? Kapewa hiyo nafasi ili amrushie maneno mwenzie???

Kwa stail hii no kazi sana nafikiri Chadema ijikite zaidi kwenye kueneza Sera na sio kushambulia na mikoa hii ndo muhimu sanaaaa jamaa likienda huko linamwaga sumu wanasahau yote ya nyuma
Jiwe akiwasema wapinzani sio kesi
Wapinzan wakimsema Magufuli kesi
 
Kama aliyempiga risasi angekuwa amekamatwa na sheria kufuata mkondo wake Lissu si angekosa la kusema? Sasa ulitaka aongelee wapi wakati mikutano iluzuiwa for 5 years?? Kunywa maji ya limau roho itatulia jombaaa
 
Kama hakuna uchaguzi wa haki sasa mgombea wa Chadema anashiriki kutafuta nini? Kudhurula mikoani kuonyesha jazba na chuki zake huku akiomba michango ya wananchi ambao anadai hawana kitu mifukoni? Acha kuleta hoja za kitoto.
Ubaya gani unaousemea kuzua uongo na kuongea kwa jazba. Kuna kipindi alidai kuna watu wametumwa wamuue kwa sumu.Hujui hizi ni tuhuma nzito,ambazo hazina ukweli.

Narudia tena, hiyo October hakuna uchaguzi bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Hizo tuhuma za Lisu kuhusu jiwe, hata uandike kitabu cha page 500 bado ukweli ndio huo huo anaousema Lisu fullstop.
 
Jaduong hivi kampeni za Cdm ya Dk Slaa 2010 unaweza kulinganisha na hizi za leo? Ok anatetea wavuvi kuwa wanaonewa ina maana anataka uvuvi haramu uruhusiwe? Anataka sheria ya uvuvi isifuatwe?
Suala la ajira ni suala gumu. Anadhani serikali inaweza kuajiri wananchi wake wote? Hata Ccm wanatambua hilo ndio maana wanasisitiza watu kujiajiri. Nenda Nigeria mtu ana Phd lakini mama ntilie. Na hao ni wengi tu.
Nadhani unavyoona hayo ndio yana msingi, basi enenda ukamshauri mgombea wako. Tumechoka na vihoja vya washauri wachawi
 
Si amejenga fly over, ameleta ajira million 6, ameboresha maslahi ya watumishi, ameleta umeme kila kona, amejenga hospital za kutosha sasa ni Mtanzania gani ataweza kueneza chuki dhidi ya mtu huyu ambaye watumishi wa umma, wakulima na wafanyabiashara wanampenda sana?
Nashangaa na mie hapo sasa, huyu kada mtiifu wa mataga ana haha vibaya, kuogopa kukosa buku 7 lol.
 
Yetu macho, kama shambulio la watu wabaya litambeba Lissu huku akieneza chuki.

Hamtaki kuambiwa ukweli, mkiambiwa mapungufu ya Utawala wenu mnasema watu wanaeneza chuki!!!
Je sio kweli kuwa JIWE alisem aliwavunjia nyumba watu wa Kimara bila fidia kwasababu hawakumpigia kura ; lakini akatoa amri wasukuma wale wa Mwanza wasivunjiwe kwasababu walimpigia kura.? Je Jiwe hakuwatukana watu wa Bukoba baada ya tetemeko na kutopeleka michango iliyotolewa kuwasaidia?
 
Tena commander in Chief mwenye askari wasiojua kulenga shabaha, yaani kumuua mtu mmoja wanapoteza risasi 30 na bado wanakosa[emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka km mazuri vileeh, daaah GOD only
 
Alafu hili la kusema eti Ccm inafanya maendeleo ya vitu na sio watu ni aibu kubwa sana. Kwani Hospital ya mkoa ya Musoma ambayo ilikwama kwa miaka 30 ni kwa ajili ya mbuzi? Mimi nipo Segese Tambalale watu wanamshangaa sana huyu mtu wenu. Anasifia wakoloni kuwa walijenga barabara! Hajui kuwa walikuwa wanatunyonya?
Acha kulialia unapoambiwa ukweli. Kwani una ahadi ya kujengewa daraja la baharini huko?
 
Wananchi wengi walitegemea kuwa kampeni zikianza tushudie na kusikia kuwa watatutalia vipi kero zetu.

Mfano tulitarajia kusikia kuwa pamoja na haya mambo makubwa yanayotekelezwa na Ccm na serikali yake wao wangeweza kufanya mazuri zaidi ya hiki kinachofanywa.Mfano tulitegea tusikie kuwa sekta ya afya, elimu na miundo mbinu imeimarishwa na Ccm. Je wao wapinzani watafanya nini zaidi kuperfom zaidi ya kinachofanywa na Ccm sasa hivi?

Hii inadhihirisha wazi kuwa hawa wapinzani hawapo tayari kuchukua dola kama watawala na hawana uwezo wa kutawala bali wamezunguka kueneza chuki na vinyongo walivyonavyo mioyoni mwao. Na hili linatupa mashaka huenda wakiwa na nafasi ya kutawala hawatatekeleza kama Ccm inavyofanya na hata kama wakipata nafasi watatuibia mali zetu za umma na kunedeleza ufisadi.

Nimemsikiliza mgombea wa Chadema akiwa Mwanza anaongea kwa jazba na chuki akiwaaminisha wananchi kuwa rais Magufuli ndio alitoa amri ya yeye kupigwa risasi. Na hii ni kwa sababu alikuwa akipinga jitahada za JPM kulinda rasilimali za watanzania. Na ameyasema haya baad ya kumsikia rais na ambaye ni mkuu wa nchi kuwa anampenda na asipoteze muda kufanya kampeni,bali atulie na atapewa kikazi kidogo cha kufanya. Mimi binafsi najua JPM ni mtu wa utani na huenda alikuwa anamtania tu huyu mgombea wa Chadema.

Lakini mgombea wa Chadema wa urais ameongea maneno makali sana akionyesha dhahiri kuwa ana chuki na JPM na amethibitisha kwa wananchi kuwa JPM alitoa amri ya yeye kupigwa risasi. Hii sio picha nzuri na wala sio sula linalofaa. Mgombea wa Chadema kama anauhakika kuwa JPM alitoa amri ili ashambuliwe anatakiwa afuate taratibu za kisheria na kwa sababu yeye ni mwanasheria anafahamu fika Mahakama kuu inayo mamlaka ya kulazimisha vyombo husika vikalishughulikia suala lake.Lakini pale wananchi wanapojazana ili wasikie utawasaidia vipi kutatua kero zao alafu unabaki kueneza chuki hii haisadii chama chake wala yeye mwenyewe.

Badala yake watu watachoka hizi hadithi zake za kupigwa risasi na October ikifika wataambulia mbunge mmoja tu.
 
Ndio nini sasa? Mtu anamtuhumu mkuu wa nchi kwa kumshambulia kwa risasi anataka nini huyu?
Maswali kaulizwa mwingine, unahangaika wee, kwan vipi unateseka?
Halafu cha ajabu hutoi hayo majibu kumsaidia huyo unae msujudia unabaki kubweka tu hapa poleeee.
 
Sikiliza Cangu wa Malunde, pale Mwanza Tundu Lissu alikuwa anajibu mapigo baada ya mgombea wa CCM kumkejeli kwamba aache kugombea na atampa kazi ndogo ndogo kwa kuwa anampenda Lissu. Eti hana tatizo naye. Kutokana na yaliyompata Lissu miaka 3 iliyopita, alijibu kama alivyojibu. Fikiria ungekuwa wewe. Wakati mwingine tuvae ngozi ya binadamu na si ya fisi!
 
Back
Top Bottom