Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Huu waraka naona umewashika pabaya mno na ni wazi hawana pa kutokea! Si waraka mbaya umesheheni ushauri na tadhahari kwa maslahi ya Watanganyika wote bila kujali imani, itikadi wala asili zao.
Ni waraka usio na chembe ya udini wala itikadi za kisiasa.. Umetembea kwenye mstari wa katiba na sheria za nchi. Ni mkataba uliozingatia kwa asilimia 100 uzalendo, ustawi, utu na urithi wa taifa hili na tunu zake kwa vizazi vya sasa na vijavyo.. Lakini nyuma yake kuna mamlaka inajaribu kuukwamisha kwa kutengeneza watu wasiojitambua kuuhuisha na dini na maisha binafsi ya watu.
Wametengezwa watu wanaohojiwa na kutoa maoni yao. Yaani ni vituko na upuuzi mtupu.. Mpaka unaona kabisa hata huyo aliyewatengeneza akili zake hazina akili kama wao.
Inawezekana kabisa kuna kitu kikubwa zaidi kibaya zaidi cha kuogofya zaidi kuhusiana DPW na Bandari zetu za Tanganyika. Maana baada ya waraka kutoka JK kaibukia huko kwa Wasabato na kutoa nasaha zake zilizoacha maswali mengi kuliko majibu
Mama naye ni mwalikwa huko KKKT sijui atasema nini. Lakini unaweza kutabiri. Chama cha mitume na manabii eti nao wametoa waraka wao unaoupinga wa TEC.
Hizo mbinu zote ni namna ya kutaka kuwatenganisha watanganyika na waraka wa TEC na kutaka kuonesha waraka huo ni wa kikundi cha watu wachache wenye malengo yao mabaya.
TEC hawajakurupuka na hawatajibu mapigo kwakuwa wanajua kwa hakika wanachokifanya na waraka husika utaendelea kusomwa kwa wiki sita mfululizo bila kukoma mpaka hata asiye na masikio ya kusikia kama kenge asikie.
Hii panic ya kijinga ya kutafuta watu mitaani waupinge waraka haitafika popote. Wasabato, KKKT, Pentecost BAKWATA na wengine wote unganeni na TEC kwenye hili mwisho hauko mbali
Umoja wetu ndio mtaji wetu
Mungu ibariki Tanganyika
Mungu wabariki Watanganyika