Kinachoendelea Twitter (X) kuhusu maoni ya watu juu ya Waraka wa TEC ni upuuzi mtupu

Tarehe 25 December 2017, Askofu Zakaria Kakobe akiwa kanisani kwenye ibada ya Christmas, katika kanisa la FGBF Mwenge jijini Dar es Salaam, alinukuliwa akituma salamu kwa Rais wa JMT, Dkt. John P. Magufuli.

"Rais John Pombe Magufuli, nawe unatakiwa kutubu leo. Unaposherekea sikukuu ya Christmas, ili uridhiwe na Mungu unatakiwa nawe utubu".

"Leo ni siku ya watawala wa Tanzania kutubu. Leo tumeanza kuona misingi ya amani ya nchi yetu ikitikiswa. Amani iliyojengwa kwa gharama kubwa na waasisi wetu. Tumeanza kuona nchi hii ni ya chama kimoja na huu ni uovu. Mungu mwenyewe anaheshimu sheria basi kama na sisi tumeweka sheria tunapaswa kuheshimu sheria tulizojiwekea wenyewe. Hii si nchi ya chama kimoja. Kama mnataka kubadilisha si mbadilishe tu mara moja kupitia wabunge wenu wa CCM, si mko wengi?".

"Sheria ni lazima zizingatiwe! Na kwa hili nitapiga kelele mpaka Mlima Kilimanjaro. Huwezi kusema wewe huwezi kusemwa, wewe ni nani? Mungu anasemwa vibaya sembuse wewe?".

"Mungu mwenye nguvu kuliko Magufuli, ana nguvu kuliko majeshi yote ya nchi, lakini anatukanwa na bado hatumii majeshi yake. Hata wewe unaweza ukawa mvumilivu"

Baada ya kauli hii, Askofu Kakobe alipokonywa passport yake, alihojiwa uraia wake na aliandamwa na TRA kwa madai ya kodi.

Huyu alikuwa ni kiongozi wa dini ya Kikistro na alimkosoa Mkristo Magufuri

Huu ulikuwa udini? Wa dini gani?

Askofu wa Catholic Jimbo la Rulenge (Severine Niwemugizi) alimkosoa mkatoliki mwenzake Magufuri juu ya haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano.

Aliishia kupokonywa passport na kuhojiwa uraia wake.

Alikuwa mdini? Akishabikia dini gani?

Nachukizwa sana na yeyote ambaye atataka kutugawa kwa misingi ya kidini.

Kukosoa haiwezi hata mara moja kuwa udini.

Kuwa kiongozi wa dini hakumnyimi haki kiongozi huyo kupata haki zake za kikatiba kutoa maoni juu ya mambo ya nchi yake kama anavyoweza kufanya Mwalimu, daktari, mkulima au mfugaji.

Tukemee wale wote wanaotaka kujificha kwenye udini pale tu wanapokosolewa kwa makosa waliyoyafanya wenyewe.

Mungu Ibariki Tanzania na watu wote.

Uhuru, Umoja na Amani

From your commander of the hand to mouth battalion

A dull, Colorless and Clueless old man now chewing Mugombero the turbo charger

Credit: Fortunatus Buyobe View attachment 2723492
Dah! Mkuu una Library ya vioja vya nchi hii wewe!

Umenikumbusha ishu ya Kakobe, nilikuwa stressed hadi nimejikuta nacheka sana.

Halafu Kakobe alivyo mjanja, alikuja kumsifia Magufuli kiaina, basi hapo hapo yakaisha!

Enhe na la kupimana mikojo unalikumbuka?
 
Huu waraka naona umewashika pabaya mno na ni wazi hawana pa kutokea! Si waraka mbaya umesheheni ushauri na tadhahari kwa maslahi ya Watanganyika wote bila kujali imani, itikadi wala asili zao.

Ni waraka usio na chembe ya udini wala itikadi za kisiasa.. Umetembea kwenye mstari wa katiba na sheria za nchi. Ni mkataba uliozingatia kwa asilimia 100 uzalendo, ustawi, utu na urithi wa taifa hili na tunu zake kwa vizazi vya sasa na vijavyo.. Lakini nyuma yake kuna mamlaka inajaribu kuukwamisha kwa kutengeneza watu wasiojitambua kuuhuisha na dini na maisha binafsi ya watu.

Wametengezwa watu wanaohojiwa na kutoa maoni yao. Yaani ni vituko na upuuzi mtupu.. Mpaka unaona kabisa hata huyo aliyewatengeneza akili zake hazina akili kama wao.

Inawezekana kabisa kuna kitu kikubwa zaidi kibaya zaidi cha kuogofya zaidi kuhusiana DPW na Bandari zetu za Tanganyika. Maana baada ya waraka kutoka JK kaibukia huko kwa Wasabato na kutoa nasaha zake zilizoacha maswali mengi kuliko majibu

Mama naye ni mwalikwa huko KKKT sijui atasema nini. Lakini unaweza kutabiri. Chama cha mitume na manabii eti nao wametoa waraka wao unaoupinga wa TEC.

Hizo mbinu zote ni namna ya kutaka kuwatenganisha watanganyika na waraka wa TEC na kutaka kuonesha waraka huo ni wa kikundi cha watu wachache wenye malengo yao mabaya.

TEC hawajakurupuka na hawatajibu mapigo kwakuwa wanajua kwa hakika wanachokifanya na waraka husika utaendelea kusomwa kwa wiki sita mfululizo bila kukoma mpaka hata asiye na masikio ya kusikia kama kenge asikie.

Hii panic ya kijinga ya kutafuta watu mitaani waupinge waraka haitafika popote. Wasabato, KKKT, Pentecost BAKWATA na wengine wote unganeni na TEC kwenye hili mwisho hauko mbali

Umoja wetu ndio mtaji wetu
Mungu ibariki Tanganyika
Mungu wabariki Watanganyika

View attachment 2723488
Screenshot_20230820-181354_X.jpg

nape kapaniki huko
 
Kataa utapeli ,kataa udini ,kataa waabudu binadamu wenzao.

Kataa wakwepa kodi pale bandari kwa mlengo wa dini.

Kataa wanaume wasiotaka kuoa hao waumini mngewapataje ,kama sio kukosa akili?

Kataa wapitisha Silaha kwa kivuli cha dini?

Kataa utapeli kabisa serikali haina dini.!!
20230821_100418.jpg
20230821_100106.jpg
 
Dah! Mkuu una Library ya vioja vya nchi hii wewe!

Umenikumbusha ishu ya Kakobe, nilikuwa stressed hadi nimejikuta nacheka sana.

Halafu Kakobe alivyo mjanja, alikuja kumsifia Magufuli kiaina, basi hapo hapo yakaisha!

Enhe na la kupimana mikojo unalikumbuka?

[emoji23][emoji23][emoji1787]
 
Huu waraka naona umewashika pabaya mno na ni wazi hawana pa kutokea! Si waraka mbaya umesheheni ushauri na tadhahari kwa maslahi ya Watanganyika wote bila kujali imani, itikadi wala asili zao.

Ni waraka usio na chembe ya udini wala itikadi za kisiasa.. Umetembea kwenye mstari wa katiba na sheria za nchi. Ni mkataba uliozingatia kwa asilimia 100 uzalendo, ustawi, utu na urithi wa taifa hili na tunu zake kwa vizazi vya sasa na vijavyo.. Lakini nyuma yake kuna mamlaka inajaribu kuukwamisha kwa kutengeneza watu wasiojitambua kuuhuisha na dini na maisha binafsi ya watu.

Wametengezwa watu wanaohojiwa na kutoa maoni yao. Yaani ni vituko na upuuzi mtupu.. Mpaka unaona kabisa hata huyo aliyewatengeneza akili zake hazina akili kama wao.

Inawezekana kabisa kuna kitu kikubwa zaidi kibaya zaidi cha kuogofya zaidi kuhusiana DPW na Bandari zetu za Tanganyika. Maana baada ya waraka kutoka JK kaibukia huko kwa Wasabato na kutoa nasaha zake zilizoacha maswali mengi kuliko majibu

Mama naye ni mwalikwa huko KKKT sijui atasema nini. Lakini unaweza kutabiri. Chama cha mitume na manabii eti nao wametoa waraka wao unaoupinga wa TEC.

Hizo mbinu zote ni namna ya kutaka kuwatenganisha watanganyika na waraka wa TEC na kutaka kuonesha waraka huo ni wa kikundi cha watu wachache wenye malengo yao mabaya.

TEC hawajakurupuka na hawatajibu mapigo kwakuwa wanajua kwa hakika wanachokifanya na waraka husika utaendelea kusomwa kwa wiki sita mfululizo bila kukoma mpaka hata asiye na masikio ya kusikia kama kenge asikie.

Hii panic ya kijinga ya kutafuta watu mitaani waupinge waraka haitafika popote. Wasabato, KKKT, Pentecost BAKWATA na wengine wote unganeni na TEC kwenye hili mwisho hauko mbali

Umoja wetu ndio mtaji wetu
Mungu ibariki Tanganyika
Mungu wabariki Watanganyika

View attachment 2723488
Kitu kikubwa cha kuogofya ni UNAFIKI NA UZANDIKI wa BARAZA kutoa waraka wenye nia ya kugonganisha na kuchonganisha.

LENGO LA WARQKA WA TEC sio maoni bali ni kuzua taharuki miongoni mwa Jamii.

TEC ni chombo cha kanisa hivyo tukiruhusu kanisa au msikiti kutoa matamko kwenye masuala ya kisiasa ni hatari kwa ustawi wa nchi yetu.

Leo waraka umetolewa na TEC, kesho watatoa BAKWATA kutetea kitakacho fuata ni malumbano ya KIDINI.

MIMI NI RC lakini sikubaliani na njia waliyo itumia TEC.

Vikiibuka vita vya kidini hakuna atakaye pona, tusifike huko lakini TEC wanataka kutufikisha huko....hii ni hatari tusiichekelea kwani hakuna atakaye pona
 
Kwa Rais Mstaafu @jmkikwete na mnaosema Baraza La Maaskofu wana chuki za kidini. Naombeni mnieleweshe:

- Baraza hili la maakofu (TEC) mwaka 2018 lilipotoa waraka wa Pasaka wa kupinga mauaji na utekaji wa watu uliofanywa na Serikali ya Jiwe walikua na vhuki ya Kidini na 'Mkatoliki' Mwenzao Magufuli?

- Mmesahau Askofu Severine Niwemuguzi alinyang’anywa Passport na kuambiwa sio raia kwa sababu ya kupinga uonevu wa
Jiwe, alikua na chuki na Mkatoliki mwenzake?

- Wakati wa COVID Baraza La Maaskofu lilipotoa waraka wa kumpinga Magufuli kuwa COVID haipo na kutaka serikali iruhusu watu wapewe chanjo, walikua na chuki za kidini na Magufuli Mkristo mwenzao?

- Walivyo kemea madudu ya uchaguzi wa 2020 walikuwa na chuki za kidini na Magufuli Mkristo mwenzao?

- Kama kila wakati kukiwa na mjadala wa kitaifa wanatoa Waraka, na hamkuwai kuona shida, kwanini mnataka sasa wasitoe?

- Kwahiyo wakitoa kwa Mkristo mwenzao sio chuki? Wakitoa sasa kwa Muislam ndio wana chuki?
Nacho kupendea mkuu unatembea na maktaba, una kumbu kumbu zote yaani!
Wajitokeze wajibu hoja hii sasa!

Halafu anayewatuma nadhani anashinda mitandaoni kufuatilia kazi aliyozituma misukule zake zimfanyie!

Maana mimi sioni mantiki ya msingi inayoleta chanzo cha mgogoro wa kidini, isipokuwa watu wanarukia matawi bila kuanzia kwenye shina.

Watueleze ni nani huyo anayepinga uislam?

Yaani watetezi wa maslahi ya nchi, leo wanageuzwa kuwa ni wapinga uislam!

Tuna safari ndefu sana waTz hasa genge la mibaka uchumi kutumia upumbafu wa wajinga kama mtaji.
 
Huu waraka naona umewashika pabaya mno na ni wazi hawana pa kutokea! Si waraka mbaya umesheheni ushauri na tadhahari kwa maslahi ya Watanganyika wote bila kujali imani, itikadi wala asili zao.

Ni waraka usio na chembe ya udini wala itikadi za kisiasa.. Umetembea kwenye mstari wa katiba na sheria za nchi. Ni mkataba uliozingatia kwa asilimia 100 uzalendo, ustawi, utu na urithi wa taifa hili na tunu zake kwa vizazi vya sasa na vijavyo.. Lakini nyuma yake kuna mamlaka inajaribu kuukwamisha kwa kutengeneza watu wasiojitambua kuuhuisha na dini na maisha binafsi ya watu.

Wametengezwa watu wanaohojiwa na kutoa maoni yao. Yaani ni vituko na upuuzi mtupu.. Mpaka unaona kabisa hata huyo aliyewatengeneza akili zake hazina akili kama wao.

Inawezekana kabisa kuna kitu kikubwa zaidi kibaya zaidi cha kuogofya zaidi kuhusiana DPW na Bandari zetu za Tanganyika. Maana baada ya waraka kutoka JK kaibukia huko kwa Wasabato na kutoa nasaha zake zilizoacha maswali mengi kuliko majibu

Mama naye ni mwalikwa huko KKKT sijui atasema nini. Lakini unaweza kutabiri. Chama cha mitume na manabii eti nao wametoa waraka wao unaoupinga wa TEC.

Hizo mbinu zote ni namna ya kutaka kuwatenganisha watanganyika na waraka wa TEC na kutaka kuonesha waraka huo ni wa kikundi cha watu wachache wenye malengo yao mabaya.

TEC hawajakurupuka na hawatajibu mapigo kwakuwa wanajua kwa hakika wanachokifanya na waraka husika utaendelea kusomwa kwa wiki sita mfululizo bila kukoma mpaka hata asiye na masikio ya kusikia kama kenge asikie.

Hii panic ya kijinga ya kutafuta watu mitaani waupinge waraka haitafika popote. Wasabato, KKKT, Pentecost BAKWATA na wengine wote unganeni na TEC kwenye hili mwisho hauko mbali

Umoja wetu ndio mtaji wetu
Mungu ibariki Tanganyika
Mungu wabariki Watanganyika

View attachment 2723488
Chawa yupo kazini😂😂😂
 
Kitu kikubwa cha kuogofya ni UNAFIKI NA UZANDIKI wa BARAZA kutoa waraka wenye nia ya kugonganisha na kuchonganisha.

LENGO LA WARQKA WA TEC sio maoni bali ni kuzua taharuki miongoni mwa Jamii.

TEC ni chombo cha kanisa hivyo tukiruhusu kanisa au msikiti kutoa matamko kwenye masuala ya kisiasa ni hatari kwa ustawi wa nchi yetu.

Leo waraka umetolewa na TEC, kesho watatoa BAKWATA kutetea kitakacho fuata ni malumbano ya KIDINI.

MIMI NI RC lakini sikubaliani na njia waliyo itumia TEC.

Vikiibuka vita vya kidini hakuna atakaye pona, tusifike huko lakini TEC wanataka kutufikisha huko....hii ni hatari tusiichekelea kwani hakuna atakaye pona
ee1d182305a30d7b43bd2911de0a77fc.jpg
 
Nacho kupendea mkuu unatembea na maktaba, una kumbu kumbu zote yaani!
Wajitokeze wajibu hoja hii sasa!

Halafu anayewatuma nadhani anashinda mitandaoni kufuatilia kazi aliyozituma misukule zake zimfanyie!

Maana mimi sioni mantiki ya msingi inayoleta chanzo cha mgogoro wa kidini, isipokuwa watu wanarukia matawi bila kuanzia kwenye shina.

Watueleze ni nani huyo anayepinga uislam?

Yaani watetezi wa maslahi ya nchi, leo wanageuzwa kuwa ni wapinga uislam!

Tuna safari ndefu sana waTz hasa genge la mibaka uchumi kutumia upumbafu wa wajinga kama mtaji.
Tuna safari ndefu sana waTz hasa genge la mibaka uchumi kutumia upumbafu wa wajinga kama mtaji[emoji419][emoji375]
 
Huu waraka naona umewashika pabaya mno na ni wazi hawana pa kutokea! Si waraka mbaya umesheheni ushauri na tadhahari kwa maslahi ya Watanganyika wote bila kujali imani, itikadi wala asili zao.

Ni waraka usio na chembe ya udini wala itikadi za kisiasa.. Umetembea kwenye mstari wa katiba na sheria za nchi. Ni mkataba uliozingatia kwa asilimia 100 uzalendo, ustawi, utu na urithi wa taifa hili na tunu zake kwa vizazi vya sasa na vijavyo.. Lakini nyuma yake kuna mamlaka inajaribu kuukwamisha kwa kutengeneza watu wasiojitambua kuuhuisha na dini na maisha binafsi ya watu.

Wametengezwa watu wanaohojiwa na kutoa maoni yao. Yaani ni vituko na upuuzi mtupu.. Mpaka unaona kabisa hata huyo aliyewatengeneza akili zake hazina akili kama wao.

Inawezekana kabisa kuna kitu kikubwa zaidi kibaya zaidi cha kuogofya zaidi kuhusiana DPW na Bandari zetu za Tanganyika. Maana baada ya waraka kutoka JK kaibukia huko kwa Wasabato na kutoa nasaha zake zilizoacha maswali mengi kuliko majibu

Mama naye ni mwalikwa huko KKKT sijui atasema nini. Lakini unaweza kutabiri. Chama cha mitume na manabii eti nao wametoa waraka wao unaoupinga wa TEC.

Hizo mbinu zote ni namna ya kutaka kuwatenganisha watanganyika na waraka wa TEC na kutaka kuonesha waraka huo ni wa kikundi cha watu wachache wenye malengo yao mabaya.

TEC hawajakurupuka na hawatajibu mapigo kwakuwa wanajua kwa hakika wanachokifanya na waraka husika utaendelea kusomwa kwa wiki sita mfululizo bila kukoma mpaka hata asiye na masikio ya kusikia kama kenge asikie.

Hii panic ya kijinga ya kutafuta watu mitaani waupinge waraka haitafika popote. Wasabato, KKKT, Pentecost BAKWATA na wengine wote unganeni na TEC kwenye hili mwisho hauko mbali

Umoja wetu ndio mtaji wetu
Mungu ibariki Tanganyika
Mungu wabariki Watanganyika

View attachment 2723488
Dawa imepulizwa nchi nzima juzi sasa hiv mende wanatoka kila tundu.
 
Tatizo Taifa letu lina watu wa hovyo sana, wana reasoning capacity ndogo na wengine wapo kwenye utawala. Kuna watu ukiwasikiliza mpaka unajiuliza huyu ana akili kweli na alifikaje hapo alipo au anafanya makusudi.

Wengine ni wanafiki, wabinafsi na wenye kuendekeza masirahi binafsi. Hotuba za Mwalim zilikuwa zipo sahihi sana na aliyaona haya yanayotokea leo. Kuna watu wapo tayari kufanya chochote ilimradi tu umemlipa bila kuangalia athali zitakazotokea siku zijazo, RUSHWA RUSHWA RUSHWA ni adui wa haki siku zote.

Tatizo la low reasoning capacity ni la muda mrefu sana na serikal imekuwa iki ignore hili tatizo kiasi kwamba limekuwa normalized.

Hii migogoro ya nchi ndio ime shed light how deeply hili tatizo limeenda
 
Dawa imepulizwa nchi nzima juzi sasa hiv mende wanatoka kila tundu.
Msome huyu anavyotumia nguvu nyingi kupotosha

Sheikh Mussa Juma amesema Wapinzani na Maaskofu wanaomsaka Rais Samia Suluhu Hassan hawana shukrani wanaendekeza Udini na maslahi yao binafsi nakusahau hisani waliyowafanyia kipindi walipokuwa hawana kitu.

Akizungumza huko visiwani Zanzibar katika mawaidha Sheikh Mussa Juma amesema Rais Samia ni kiongozi wenye huruma na uadilifu ndani yake hivyo wanaomsakama wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi.

"Hapa kwetu ndio kabisa madudu haya ya kisiasa sijui wakina Mbowe kina Lissu waliyoyaficha ndani ya mioyo yao yalikuwa ni makubwa zaidi kuliko wanayoyadhihirisha, angalia sasa hivi wanavyotapika maneno yale angalia ni udini tu ule, kama huyo Dkt. Slaa yeye ndio kamaliza mchezo mmemsikia mwenyewe Udini tu ule hakuna kitu kingine Udini tu..sasa yale ndio yaliyokuwa yamejificha hawana shukrani hata kidogo" alisema

Sheikh Mussa Juma amesema Rais Samia ni mtu mwenye imani wanaomuanda wanapaswa kumshukuru na kumheshimu kutokana nakuwafanyia hisani kwa kuwarejeshea vitu vyao walivyopoteza kipindi cha awamu ya Tano.

"Alikuwepo Magufuli kawanyongesha watu, kawaadhibu watu, kawatesa watu hawana hatia wamenyamaza kimya, Mwenyezi Mungu kafanya Rehema zake katuletea mtu ana imani watu wanaishi kwa raha , watu wanapendana, wanasaidiana, mnyonge anasaidiwa leo hawa wakina Mbowe, Lissu hawana Shukrani mtu kama huyo alowafanyia hisani kama huyu Lissu alipofanyiwa mambo mazito mtu wa kwanza kwenda kumtizama ni Rais Samia wale waliobakia wote maaskofu ambao sasa hivi ndio wanamtukana Samia kwa sababu ya uislamu hakuna kingine na maslahi yao waliyokuwa wanaipata kwenye ile bandari wanamsaka hawana shukrani wote hao maaskofu walikuwa wameufyata wanamuogopa Magufuli , lakini tazama alichomfanya Rais Samia kamlipa kila kitu chake kamrejeshea ambavyo alikuwa kanyang'anywa na huyo Mbowe hivyo hivyo kila kitu chake karejeshewa kalipwa pesa chungu mzima ambazo zingewasaidia wananchi , Rais Samia anaonyesha huruma kwa rai wake alafu hawa wanakuja juu wanamtukana na kumkashifu kwa maslahi yetu wenyewe sisi wananchi lakini kwa sababu wao kuna maslahi yao ya dini pale wanahisi atakuja kuondoka , pamoja na maslahi yao walikuwa wanapitisha vitu pale...." alisema Sheikh huyo

Pamoja na yote Sheikh Mussa dunia ilipofikia sasa mambo mema yanaonekana mabaya huku mabaya yakionekana mema hata hivyo amemuomba Rais Samia aendelee kuishi maisha marefu kutokana na uadilifu na huruma alionao katika uongozi wake.

"Mbona mambo sasa hivi yanaanza kuchimbuka yaliyokuwa yamejificha na sisi ndio tunayasubiri kwa hamu kwa sababu tulipokuwa tunasema nyinyi mlituona sisi wabaya lakini sasa hivi Mwenyezi Mungu anayachimbua, mmemsikia Slaa alivyosema nyie waislamu mmekaa tu mmemsikia na uislamu wenu mnasikia wanavyomfanyia muislamu mwenzenu wanavyomwandama, wanaranda kwenye mikoa kwa kutumia pesa hizi hizi wanazopewa zetu wenyewe kama rai wanamsakama Mhe. Rais Samia lakini Mwenyezi Mungu atamuhifadhi, atamlinda na shari zao ataendeleza uadilifu, ni Rais pekee aliyekuwa hana mfano na waliyokuwa wamepita mwenye huruma mpaka na vilema tunamuombea dua na tutazidi kumuombea sasa kama wewe unanuna nuna"_ Sheikh Mussa Juma akizungumza msikitini Zanzibar
20230821_110454.jpg
 
Msome huyu anavyotumia nguvu nyingi kupotosha

Sheikh Mussa Juma amesema Wapinzani na Maaskofu wanaomsaka Rais Samia Suluhu Hassan hawana shukrani wanaendekeza Udini na maslahi yao binafsi nakusahau hisani waliyowafanyia kipindi walipokuwa hawana kitu.

Akizungumza huko visiwani Zanzibar katika mawaidha Sheikh Mussa Juma amesema Rais Samia ni kiongozi wenye huruma na uadilifu ndani yake hivyo wanaomsakama wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi.

"Hapa kwetu ndio kabisa madudu haya ya kisiasa sijui wakina Mbowe kina Lissu waliyoyaficha ndani ya mioyo yao yalikuwa ni makubwa zaidi kuliko wanayoyadhihirisha, angalia sasa hivi wanavyotapika maneno yale angalia ni udini tu ule, kama huyo Dkt. Slaa yeye ndio kamaliza mchezo mmemsikia mwenyewe Udini tu ule hakuna kitu kingine Udini tu..sasa yale ndio yaliyokuwa yamejificha hawana shukrani hata kidogo" alisema

Sheikh Mussa Juma amesema Rais Samia ni mtu mwenye imani wanaomuanda wanapaswa kumshukuru na kumheshimu kutokana nakuwafanyia hisani kwa kuwarejeshea vitu vyao walivyopoteza kipindi cha awamu ya Tano.

"Alikuwepo Magufuli kawanyongesha watu, kawaadhibu watu, kawatesa watu hawana hatia wamenyamaza kimya, Mwenyezi Mungu kafanya Rehema zake katuletea mtu ana imani watu wanaishi kwa raha , watu wanapendana, wanasaidiana, mnyonge anasaidiwa leo hawa wakina Mbowe, Lissu hawana Shukrani mtu kama huyo alowafanyia hisani kama huyu Lissu alipofanyiwa mambo mazito mtu wa kwanza kwenda kumtizama ni Rais Samia wale waliobakia wote maaskofu ambao sasa hivi ndio wanamtukana Samia kwa sababu ya uislamu hakuna kingine na maslahi yao waliyokuwa wanaipata kwenye ile bandari wanamsaka hawana shukrani wote hao maaskofu walikuwa wameufyata wanamuogopa Magufuli , lakini tazama alichomfanya Rais Samia kamlipa kila kitu chake kamrejeshea ambavyo alikuwa kanyang'anywa na huyo Mbowe hivyo hivyo kila kitu chake karejeshewa kalipwa pesa chungu mzima ambazo zingewasaidia wananchi , Rais Samia anaonyesha huruma kwa rai wake alafu hawa wanakuja juu wanamtukana na kumkashifu kwa maslahi yetu wenyewe sisi wananchi lakini kwa sababu wao kuna maslahi yao ya dini pale wanahisi atakuja kuondoka , pamoja na maslahi yao walikuwa wanapitisha vitu pale...." alisema Sheikh huyo

Pamoja na yote Sheikh Mussa dunia ilipofikia sasa mambo mema yanaonekana mabaya huku mabaya yakionekana mema hata hivyo amemuomba Rais Samia aendelee kuishi maisha marefu kutokana na uadilifu na huruma alionao katika uongozi wake.

"Mbona mambo sasa hivi yanaanza kuchimbuka yaliyokuwa yamejificha na sisi ndio tunayasubiri kwa hamu kwa sababu tulipokuwa tunasema nyinyi mlituona sisi wabaya lakini sasa hivi Mwenyezi Mungu anayachimbua, mmemsikia Slaa alivyosema nyie waislamu mmekaa tu mmemsikia na uislamu wenu mnasikia wanavyomfanyia muislamu mwenzenu wanavyomwandama, wanaranda kwenye mikoa kwa kutumia pesa hizi hizi wanazopewa zetu wenyewe kama rai wanamsakama Mhe. Rais Samia lakini Mwenyezi Mungu atamuhifadhi, atamlinda na shari zao ataendeleza uadilifu, ni Rais pekee aliyekuwa hana mfano na waliyokuwa wamepita mwenye huruma mpaka na vilema tunamuombea dua na tutazidi kumuombea sasa kama wewe unanuna nuna"_ Sheikh Mussa Juma akizungumza msikitini ZanzibarView attachment 2723697
Mi hata cnaga muda wa kuwasoma hawa jamaa ni zero brain. Waje wapinge kwa vifungu basi wao shida yao ni maaskofu kuandika
 
Huu waraka naona umewashika pabaya mno na ni wazi hawana pa kutokea! Si waraka mbaya umesheheni ushauri na tadhahari kwa maslahi ya Watanganyika wote bila kujali imani, itikadi wala asili zao.

Ni waraka usio na chembe ya udini wala itikadi za kisiasa.. Umetembea kwenye mstari wa katiba na sheria za nchi. Ni mkataba uliozingatia kwa asilimia 100 uzalendo, ustawi, utu na urithi wa taifa hili na tunu zake kwa vizazi vya sasa na vijavyo.. Lakini nyuma yake kuna mamlaka inajaribu kuukwamisha kwa kutengeneza watu wasiojitambua kuuhuisha na dini na maisha binafsi ya watu.

Wametengezwa watu wanaohojiwa na kutoa maoni yao. Yaani ni vituko na upuuzi mtupu.. Mpaka unaona kabisa hata huyo aliyewatengeneza akili zake hazina akili kama wao.

Inawezekana kabisa kuna kitu kikubwa zaidi kibaya zaidi cha kuogofya zaidi kuhusiana DPW na Bandari zetu za Tanganyika. Maana baada ya waraka kutoka JK kaibukia huko kwa Wasabato na kutoa nasaha zake zilizoacha maswali mengi kuliko majibu

Mama naye ni mwalikwa huko KKKT sijui atasema nini. Lakini unaweza kutabiri. Chama cha mitume na manabii eti nao wametoa waraka wao unaoupinga wa TEC.

Hizo mbinu zote ni namna ya kutaka kuwatenganisha watanganyika na waraka wa TEC na kutaka kuonesha waraka huo ni wa kikundi cha watu wachache wenye malengo yao mabaya.

TEC hawajakurupuka na hawatajibu mapigo kwakuwa wanajua kwa hakika wanachokifanya na waraka husika utaendelea kusomwa kwa wiki sita mfululizo bila kukoma mpaka hata asiye na masikio ya kusikia kama kenge asikie.

Hii panic ya kijinga ya kutafuta watu mitaani waupinge waraka haitafika popote. Wasabato, KKKT, Pentecost BAKWATA na wengine wote unganeni na TEC kwenye hili mwisho hauko mbali

Umoja wetu ndio mtaji wetu
Mungu ibariki Tanganyika
Mungu wabariki Watanganyika

View attachment 2723488
Mwijaku, Kitenge wamelaaniwa
 
Kwenye ukweli nuru hutawala.
Penye kasoro giza hunyemelea.
Ni suala la muda tu Mungu atatupa majibu ya kinachoendelea.
Yeyote aliyekula kiapo atende kadri ya kiapo chake.
Wananchi tumlilie Mungu kwani yupo na anatenda.
 
Back
Top Bottom