Kinachofanywa na Mchungaji Msigwa hakina tofauti na kinachofanywa na CHADEMA, nadhani kuna haja ya kubadilika

Kinachofanywa na Mchungaji Msigwa hakina tofauti na kinachofanywa na CHADEMA, nadhani kuna haja ya kubadilika

Kiuhalisia ukitoa sehemu ndogo ya watu ambayo ni watumishi wa Serikali na wanasiasa Asilimia kubwa ya wananchi wanaamini katika Hayati Magufuli na wanampenda .

Ukiingia humu jukwaani ,ukiwa ofisini na ukiwa kwenye kundi la wanasiasa utaona mnaongea lugha moja kuhusu JPM ambayo ni kama 80% siyo uhalisia wa mtaani . Mtaani hawaambii kitu kibaya kuhusu JPM wakakukubali hata ukiwa na ushahidi.

CHADEMA wanakwenda mikutano wanadai sera baada ya muda anasimama kiongozi anaanza mzungumzia vibaya hayati Magufuli kitu ambacho hapo alipo zaidi ya 80% wanaamini katika utendaji wake ,Unategemea nini ?

Vivyo hivyo kwa Msigwa Kiuhalisia ukitoa wanufaika wa mfumo wa CCM watu wanaamini katika Upinzani hususani CHADEMA mbali na mapungufu yake , kwa hiyo anaposimama na kuisema vibaya watu hawamuelewi hata wana CCM mule ndani baadhi hawamuelewi .

Hivyo CDM na msigwa kuna haja ya kubadilika mnafanya makosa yale yale ,someni .

Kama CHADEMA akisimama akinadi sera zake na kusimama na Mazuri ya JPM ambayo raia wanayaoona huko mitaani wataeleweka Sana .​
Magufuli alikuwa na mazuri yake na mabaya pia kama binadamu.
Kwa hiyo, tunatakiwa kumuenzi kwa kuiga na kusimamia yale mazuri na kuacha au kurekebisha yale mabaya.
Ni busara na haki kuendeleza yale mazuri.
 
Back
Top Bottom