Kinachofanywa na Mchungaji Msigwa hakina tofauti na kinachofanywa na CHADEMA, nadhani kuna haja ya kubadilika

Kinachofanywa na Mchungaji Msigwa hakina tofauti na kinachofanywa na CHADEMA, nadhani kuna haja ya kubadilika

Mkuu hawa watu hawawezi kukuelewa ila majibu watayapata 2025, watarudi kusema wameibiwa kura wakati kosa lao ni kutokukubali ukweli kuwa JPM anawafuasi wengi ambao wangepaswa kuwapata.
Tanzania hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Sasa hiyo 2025 unasubiri matokea gani kwenye hizo chaguzi za kishenzi? Inshort hakuna anayetishika na uchaguzi ambao tayari unafahamika ni wa matokeo ya kupangwa.
 
Acha utoto hili liko wazi ,tatizo mkikaa kwenye ka ofisi kenu wawili watatu mna hisi mnawakilisha mawazo ya watanzania wote
Angeheshimu uchaguzi ungeweza kuja na kipimo halisi cha kukubalika kwake. Hatukatai alikuwa na watu wanaomkubali sana, sasa angekaa kwa kutulia aheshimu uchaguzi ili apate kura halisi za kukubalika kwake, ila sio kwa uhayawani ule wa 2020.
 
Kiuhalisia ukitoa sehemu ndogo ya watu ambayo ni watumishi wa Serikali na wanasiasa Asilimia kubwa ya wananchi wanaamini katika Hayati Magufuli na wanampenda .

Ukiingia humu jukwaani ,ukiwa ofisini na ukiwa kwenye kundi la wanasiasa utaona mnaongea lugha moja kuhusu JPM ambayo ni kama 80% siyo uhalisia wa mtaani . Mtaani hawaambii kitu kibaya kuhusu JPM wakakukubali hata ukiwa na ushahidi.

CHADEMA wanakwenda mikutano wanadai sera baada ya muda anasimama kiongozi anaanza mzungumzia vibaya hayati Magufuli kitu ambacho hapo alipo zaidi ya 80% wanaamini katika utendaji wake ,Unategemea nini ?

Vivyo hivyo kwa Msigwa Kiuhalisia ukitoa wanufaika wa mfumo wa CCM watu wanaamini katika Upinzani hususani CHADEMA mbali na mapungufu yake , kwa hiyo anaposimama na kuisema vibaya watu hawamuelewi hata wana CCM mule ndani baadhi hawamuelewi .

Hivyo CDM na msigwa kuna haja ya kubadilika mnafanya makosa yale yale ,someni .

Kama CHADEMA akisimama akinadi sera zake na kusimama na Mazuri ya JPM ambayo raia wanayaoona huko mitaani wataeleweka Sana .​
Nakuunga mkono Mia Kwa Mia.
 
Angeheshimu uchaguzi ungeweza kuja na kipimo halisi cha kukubalika kwake. Hatukatai alikuwa na watu wanaomkubali sana, sasa angekaa kwa kutulia aheshimu uchaguzi ili apate kura halisi za kukubalika kwake, ila sio kwa uhayawani ule wa 2020.
Hivi wewe jama uchaguzi wa 2020 walikukosea nini ?
 
Back
Top Bottom