Kinachoiponza Tanzania ni mashitaka dhidi ya mwana habari Erick Kabendera, ni kama marehemu Jamal Khashoggi (Mwanahabari)

Kinachoiponza Tanzania ni mashitaka dhidi ya mwana habari Erick Kabendera, ni kama marehemu Jamal Khashoggi (Mwanahabari)

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Na huo ndiyo ukweli wenyewe. Mwana habari Erick Kabendera nje ya Tanzania ni mwana habari mwenye nguvu na mwenye uzani sawa na kina Jamal Khashoggi. Hayo mengine yalitokea yakapita kimya bila madhara makubwa. Wapo waliotekwa, wapo waliopotea, wapo walionusurika kuuawa, wapo waliouawa na wapo walionyang'anywa uwekezaji wao wa jasho na damu kwenye huu utawala wa John Pombe Magufuli. Hayo yote yalipita huku yakiangaliwa kwa mbali kidogo na subira.

Serikali ilikuja kujichanganya sana kumkamata mwana habari Erick Kabendera ambaye ni mwana habari anayehabarisha nje ya mipaka ya Tanzania, mwana habari aliykeuwa anatoa ukweli wote wa yanayoendelea Tanzania huko nje. Walijichanganya sana kumkamata na kumfungulia mashitaka ya uonevu na kubambikia.

Kukamatwa kwa Erick Kabendera kumetibua majeraha yote na sasa Tanzania ilianza kuchunguzwa kwa umakini zaidi na ndipo yanakuja haya.Na kusema kweli tutayavaa na si kwa Marekani pekee bali mlolongo wote wa mataifa ya NATO.

Mwana habari Jamal Khashoggi ambaye aliuawa kikatili ndani ya ofisi za ubalozi kwa kile kinachoelezwa kuwa alikuwa akimvua nguo kwa kumuandika mwana mfalme wa Saudi Arabia, mauaji yake yalileta sintofahamu kubwa duniani na kupelekea utawala wa Saudi Arabia kukosa imani kwa Marekani. Basi huyu Kabendera ni level zile zile za kina marehemu Khashoggi. Naamini kwa wale wanaoenda mahakamani kushuhidia kesi ya Kabendera na kuona wafuatiliaji wageni wa kesi hii tutakuwa pamoja.

Mashitaka dhidi ya Kabendera yataiponza Tanzania zaidi ya hapa!

Bahati mbaya sana na Nigeria nao wamekumbwa na tukio hilo hilo baada ya wao pia kujiingiza ku deal na mwanahabari nguli Omoyele Sowore. Nigeria wana ugaidi wa kila aina, wana matapeli duniani hakuna na yote haya wameyafanya kwa miaka mingi iweje leo? Ukitaka uhasama na dunia iliyostaharabika basi wabughudhi waandishi wanaoonekana ni threat kwako kama wewe ni mtawala.
 
Kabendera alikuwa anatumika na Acacia na baadhi ya nchi kuchafua taswira ya Tz, hii ndio sababu kubwa wanaifuatilia kesi ya Kabendera kwa ukaribu sana maana ni “asset” yao. Adhabu ya Kabendera kwa nchi nyingi ni kifo maana hana tofauti na spy au foreign agent yoyote anayetumika kuchafua nchi.

Hata wakiweka vikwazo hakuna kumuachia Kabendera hadi apate haki na stahili yake kwa kuichafua nchi ili iwe fundisho kwa nyumbu yoyote ukitumika kama foreign agents wewe ni adui wa nchi na adhabu inayokustahili ki usalama ni kuwa eliminated.
 
Tanzania inaongezwa kwenye Trump ban.

Ndugu zetu waliokuwa wanatutembelea kila mwaka watapata tabu kuja.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi tusipoangilia vizuri itaponzwa na kabila moja hivi linapenda sifa saaana,na enzi za nyerere lilijaribu kuasi historia iko vizuri inathibitisha.
Kabila hili limejazana nchi za magharibi lakini wengi wao ndio kazi za akina kabendera,
 
Back
Top Bottom