Mmesikia kelele za watawala, baada ya kupoka madaraka kwa nguvu kupitia uchaguzi bandia, baada ya kuwaua watanzania wengi waliokuwa wakipinga uchaguzi haramu, baada ya kuteka, kuwaua na kuwapoteza watanzania wengi, kwa unafiki mkubwa, sahizi wanaimba maridhiano.
Kabla ya uchaguzi, watanzania wengi wenye hekima na dhamira njema, mzee Warioba, viongozi wa dini, viongozi wa CHADEMA, na wengine wengi, walishauri sana kuwepo na mjadala wa kitaifa kuhusiiana na utekaji wa watu uliokuwa unafanywa na watawala, na pia marekebisho muhimu ya lazima kuhusiana na sheria na kanuni za uchaguzi, watawala hawa wenye kiburi na CCM yao, na mamluki wao, walikataa kata kata.
KWA NINI WANATAKA MARIDHIANO SASA BAADA YA KUPORA MAMLAKA?
Hawa watu wala hawana dhamira ya maridhiano, bali ni uhuni ule ule, wanatafuta njia ya kuhalalisha uharamia wao wa kupora mamlaka ya wananchi kuwapata viongozi kupitia uchaguzi, na pia kupakaa manukato mauaji waliyoyafanya, ili waudanganye Ulimwengu kuwa wameondokana na dhuluma, na sasa wanakubalika na Watanzania.
Watanzania tusikubali kuhadaiwa, tusikubali kuwa sehemu ya uovu wa watawala na CCM. AU na SADC wamesema Tanzania hakukuwa na uchaguzi, na sisi tunajua hakukuwa na uchaguzi bali karamu ya waovu ya kuwateketeza watanganyika kwa risasi. Maridhiano pekee ni kuwakamata na kuwafungulia mashtaka walioandaa uchaguzi bandia, walioua wananchi, na watekaji wote. Nje ya hayo, kamwe tusihadaike.