Kinachozeesha mwili ni akili

Kinachozeesha mwili ni akili

Binafsi naona watu wanaopenda Sana kutazama Taarifa za habari wanazeeka Sana ...kuliko wale wanaotazama mziki Tu mda wote au tamthilia Tu mda wote
 
Kwa muda sasa nimekuwa nikitafakari sana kwamba huenda kama binadam asingekuwa na shughuli nyingi sana zinazohitaji ubongo wake kufikiri kwa kina sana ili kupata majibu au matokeo ya kile anachokifanya, basi angedumu kwa muda/miaka mingi sana bila kuzeeka. Nina mifano michache hapa:

Nina rafiki mmoja ambae kabla ya kuajiriwa miaka mitatu nyuma alikuwa kijana kabisa wala huwezi kumfikiria kuwa na umri mkubwa kwa namna yoyote ile. Baada ya kupewa majukumu mazito ambayo mara nyingi yanahitaji matumizi makubwa ya akili, ameanza kuota mvi kwa haraka sana ndani ya mwaka mmoja tu na sura yake sasa inaonesha ni mtu wa makamo ilihali ni kijana mdogo tu.

Mfano wa pili, narejelea, muonekano wa Barack Obama kabla ya kuwa rais na baada ya kuwa rais(kama picha zilizowekwa mtandaoni ni sahihi). Mfano wa mwisho, nimewahi kuangalia pia picha za Kikwete kabla ya urais na muda mfupi baada ya kuwa rais.

Ndugu wanajamvi, kuna uwezekano jambo hili likawa na uhalisia? Kwa wakristo, rejea kwa manabii, mitume na wafalme wa zamani katika biblia miaka walioishi. Huenda kudumu kwa muda mrefu kulichangiwa na namna walivyoishi, yaani hawakuhitaki kuumiza kichwa sana kufikiria kuishi maisha yenye uhitaji wa mikiki mikiki ya akili.
Matumizi makubwa ya akili hayawezi sababisha mtu kuzeeka. Manake kuzeeka ni matokeo ya seli hai kufa na kupungua mwilini sasa kadri mtu anavyokuwa ndipo hizi seli nazo hupungua na hii haiepukiki.
Stress, matumizi ya alcohol, tumbaku, kuvuta hewa isiyo safi, ulaji mbaya na mazingira kiujumla ni vitu vinavyochangia kwa kiasi kikubwa kuua seli za mwili. Hao watu uliowataja wanaangukia kwenye moja ya hivi vitu, wewe na mimi pia.
 
Kwa muda sasa nimekuwa nikitafakari sana kwamba huenda kama binadam asingekuwa na shughuli nyingi sana zinazohitaji ubongo wake kufikiri kwa kina sana ili kupata majibu au matokeo ya kile anachokifanya, basi angedumu kwa muda/miaka mingi sana bila kuzeeka. Nina mifano michache hapa:

Nina rafiki mmoja ambae kabla ya kuajiriwa miaka mitatu nyuma alikuwa kijana kabisa wala huwezi kumfikiria kuwa na umri mkubwa kwa namna yoyote ile. Baada ya kupewa majukumu mazito ambayo mara nyingi yanahitaji matumizi makubwa ya akili, ameanza kuota mvi kwa haraka sana ndani ya mwaka mmoja tu na sura yake sasa inaonesha ni mtu wa makamo ilihali ni kijana mdogo tu.

Mfano wa pili, narejelea, muonekano wa Barack Obama kabla ya kuwa rais na baada ya kuwa rais(kama picha zilizowekwa mtandaoni ni sahihi). Mfano wa mwisho, nimewahi kuangalia pia picha za Kikwete kabla ya urais na muda mfupi baada ya kuwa rais.

Ndugu wanajamvi, kuna uwezekano jambo hili likawa na uhalisia? Kwa wakristo, rejea kwa manabii, mitume na wafalme wa zamani katika biblia miaka walioishi. Huenda kudumu kwa muda mrefu kulichangiwa na namna walivyoishi, yaani hawakuhitaki kuumiza kichwa sana kufikiria kuishi maisha yenye uhitaji wa mikiki mikiki ya akili.
Labda niulize ili kupata ufafanuzi wa ziada kuhusu hii hoja. Kuna wakati mnaweza kuwa katika level moja ya elimu, tuseme secondary au chuo, baadhi ya wanafunzi wanaanza kuota mvi au kuanza kuwa na upara, je hawa wanakuwa wanatumia aki zao zaidi ya wengine?
Na je kama matumizi ya akili ndio huzeesha, watoto wanazaliwa wakiwa na mtindio wa ubungo, hawa uwezo wa akili huwa mdogo ukilinganisha na wengine, je hawa wanachelewa kuzeeka kutokana na kuwa hawatumii akili nyingi?.
 
Kinachozeesha ni michakato miiiiingi ya kiungo husika, so sehemu itakayoanza kuzeeka ni ile inatumika sana zaidi ya kawaida[kuistressisha];
Kama unaustressisha sana ubongo, ubongo utaanza na mwili utafuata fasta,
Kama unakuuula sana basi tumbo litaanza na mwili utafata fasta,
Kama unakulana sana hivyohivyo sehemu za siri zitaanza na mwili utafuata fasta,
Imagine hata wanaolewa sana ni ini litaanza halafu ndio mwili utafata fasta,
Unakula na kunywa visumusumu basi figo[au ini] litaanza na mwili utafuata fasta,
Watu zamani walikuwa wanapigwa jua sana so ngozi ilianza halafu mwili unafata fastaa.

Hii sio concept mpya, waulize wanaomiliki gari, pikipiki au hata bajaji na baskeli. Kuna kanuni moja kwamba kikiharibika kitu hata kama ni kidoogo wewe fanya service. Usipokafanyia service basi chombo kizima[mwili mzima] utafatia kuharibika na kufa kabisa. Ikiua ka pump ukaacha kuservice inaua hadi injini vivyo hivyo kwa mwili.
Nakubali kwa asilimia 100, ukiangalia wazee waliokuwa wanafanya kazi nyingi za mikono wakifikisha umri fulani viungo vinakataa

Na asilimia kubwa ni mifupa kusuguana.
 
Back
Top Bottom