Kinachozeesha mwili ni akili

Binafsi naona watu wanaopenda Sana kutazama Taarifa za habari wanazeeka Sana ...kuliko wale wanaotazama mziki Tu mda wote au tamthilia Tu mda wote
 
Matumizi makubwa ya akili hayawezi sababisha mtu kuzeeka. Manake kuzeeka ni matokeo ya seli hai kufa na kupungua mwilini sasa kadri mtu anavyokuwa ndipo hizi seli nazo hupungua na hii haiepukiki.
Stress, matumizi ya alcohol, tumbaku, kuvuta hewa isiyo safi, ulaji mbaya na mazingira kiujumla ni vitu vinavyochangia kwa kiasi kikubwa kuua seli za mwili. Hao watu uliowataja wanaangukia kwenye moja ya hivi vitu, wewe na mimi pia.
 
Labda niulize ili kupata ufafanuzi wa ziada kuhusu hii hoja. Kuna wakati mnaweza kuwa katika level moja ya elimu, tuseme secondary au chuo, baadhi ya wanafunzi wanaanza kuota mvi au kuanza kuwa na upara, je hawa wanakuwa wanatumia aki zao zaidi ya wengine?
Na je kama matumizi ya akili ndio huzeesha, watoto wanazaliwa wakiwa na mtindio wa ubungo, hawa uwezo wa akili huwa mdogo ukilinganisha na wengine, je hawa wanachelewa kuzeeka kutokana na kuwa hawatumii akili nyingi?.
 
Nakubali kwa asilimia 100, ukiangalia wazee waliokuwa wanafanya kazi nyingi za mikono wakifikisha umri fulani viungo vinakataa

Na asilimia kubwa ni mifupa kusuguana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…