Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Kaunda jopo kwani kashinda?!nachelea kuamini hawa watu kuna walichofanya
 
Naona CCM kweli mmechokwa....hahaha.
Mpaka mnamtumia Lowassa kama njia ya kuwavuta wasomaji.
 
Wameanza kuangalia wanajipanga vipi ikitokea wanashin dwa uchaguzi. Wasipo jipanga sasa,chama kitakufa na makada wengi watakufa kwa kasi ajabu kwa sababu ya ukata na kukosa mada raka.
 

Mabaliko.... lowasa .magufuli.... uwiiiiiiiiii...
 
Hayo ni maandalizi mazuri. Hakuna sababu ya kupoteza muda baada ya uchaguzi. Wananchi wanakiu ya mabadiliko. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Miaka 50 walikua wanaishi wapi? Mnadanganywa kama watoto, mnachekelea...umeshajiuliza hilo jopo lake nani analilipa? Kwa pesa zipi? Wenye ajira siku nyingi kama waalimu mishahara yao ni shida, hawa wengine wanaajiriwa kwa kanuni zipi? Au ndo udikteta wa madaraka yasiyo na mpaka? Rais wake bado yupo, haoni ni kumdharau? Siasubiri amkabidhi ofisi ndo aanzie hapo? Yani Watanzania.. Dah Mungu tu awasaidie.
 
Mkuu lakini Mh.Magufuli hatumii chopa.

Hata wewe mwenyewe hujui kinachoendelea unapelekwa tu kiushabiki...chopa 4 zimepangwa kutumika, na mgombea atatumia itakapomlazimu. Kwahiyo ccm halali, wengine haramu.
 
Acha kusema takataka wewe,matokeo ya urais minimum mda wa kutangaza ni masaa 72.sasa wewe sijui utakua unashangilia matokeo yapi???
Wewe ni mpumbavu na lofa! Mbona huulizi EL anaposema kuwa ushindi utapatikana mapema tarehe 25/10/2015?
 
Ndg Wanajamii,

Jana na leo vyombo vya habari vimejinasibu na habari ya Mgombea wa CCM ndg Magufuli kuteuwa jopo la wataalamu kwa ajili ya mchakato wa kumwezesha kutenda kazi vizuri akiwa ikulu. Kwa taarifa za kweli na rasmi ni propaganda tu, hakuna kitu kama hicho, ni mbinu tu ya wapambe kuona kama gia hiyo inaweza kuwaingia wananchi na kuona kama kweli inalipa kama ile ya tafiti za TWAWEZA kubuma.

Wakati Makamba anatangaza hayo kwa wandishi wa habari, alishindwa kubainisha wabobezi hao wametoka katika taasisi zipi na lead consultant ni nani? Ndio maana mambo muhimu hayajabainishwa katika ushauri wao. Pia mambo mengine kama Mishahara kwa utumishi wa umma uko wazi na kuna sera na tume maalum sasa ya kusimamia mishahara.

Ni vema UKAWA KUCOUNTER ATTACK MARA MOJA Propaganda hii.
 
Piga hesabu ya saa vizuri! Uchaguzi unafanyika tarehe 25 kuanzia saa2 hadi 10. Baada ya hapo wanahesabu kura. Mwisho wa siku ni saa6 kamili usiku. Kuanzia saa 6.01 ni tarehe 26/10 ambapo ni siku nyingine na siyo asubuhi na mapema 25/10 kama unavyodai wewe! #Hapakazitu
 
Unafikiri Lowassa akishika nchi vitu vyote vinafutwa? Au yeye anaanza na watumishi wapya kila sehemu!

Nilijua analipwa pension kwa propaganda zake, kama ni mstaafu haina haja kubishana, kwanza huna changamoto za kimaisha kulingana na umri wako pia vyema ungetuacha vijana tufanye ya kwetu labda yatakuwa bora maana yenu nyinyi mlifanya ndio yametufikisha hapa.
 
Yeah: 1%Words 99%Actions. Lowassa.
Kabisa....Mungu akikupa nguvu akakunyima hekima utampiga hadi mamako...ndo ya ccm...wanapiga makofi mama zao bila haya na wanashangilia kwa push ups majukwaani.

Ivi kweli kwa hapa tz ilipo unahitaji kuunda jopo la kuchunguza vitu wakati umetawala for 50 worse years?

Nani anamshauri huyu MTU?

Hilo jopo linalipwa na nani kwa pesa gani?

Hizo milioni 50 zinazogawiwa kama Katanga zinatoka kwenye mfuko gani?

Vifo vya wajawazito na vichanga, albino na wazee...vitawahukumu!

Raisi bado yupo ofisini, kwani hana nyaraka za kumkabidhi zenye taarifa ya mafanikio na changamoto? Haoni ni tusi kwa serikali? Anaharaka ya nini?

Inasikitisha nchi ikiongozwa bila hekima!

Na tunapata tabu kwasababu wenye hekima ni wachache kuliko wasio na hekima ambao wanashangilia huu upuuzi.

Lowasa kapewa hekima, sio nguvu. Mungu amsimamie!

Mungu ikumbuke tz.

Nadhani kilichobaki sasa ni maombi tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…