Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Hicho wanachokiita jopo kipo ila sina uhakika na uwezo wao
 
Mkapa lazima ajue wapumbavu/malofa/mambumbu-mbu tutampigia lowasa kura.
 
Yaani Mgombea anatangaza hadharani kuunda 'Genge' lake tayari la kutawala katika kipindi hichi cha kampeni. So what?
Tukijua hicho kikosi chake kinatusaidia nini kwa sasa?
Tamko hilo lina uhusiano gani na kampeni kwa sasa?

Ukichunguza vizuri hii ni PROPAGANDA tu ili kutaka watanzania tuamini Magufuli ndio raisi na tusijipange kwenda kupiga kura.
Dawa yake ni ndogo sana, tuwapotezee tu.
 
Hapa kaz tu, magufuri utekeleze ahadi zako mi hapa anza kuhesabu kura yangu kwako
 
Katika kiwango cha juu cha UJUHA! Mtu ambae hana uwezo wa kushinda anaunda jopo la kumshauri! Naona ni jopo la KURUKARUKA JUKWAANI NA PUSH UPS!
 
Jopo ina tofauti gani tume tulizozoea? Acheni wajitekenye wenyewe hadanganyiki mtu.Lini CCM ikawatumia wataalam? Nape na Kinana ndiyo jopo lenye meno.
 
Kama hakutakuwa na goli la mkono Lowasa anangoja kuapishwa kuingia ikulu. Wanaompenda ni wengi na kizuri ni kuwa wamejiandikisha kupiga kura! Wana hamasa kubwa ya kwenda kupiga kura tarehe 25/10. Si mijini wala vijijini jina Lowasa liko juu!
 
Magufuli ni dawa ya hayo yote.

Nchi inaendeshwa na taasisi ya uraisi.. Si mtu mmoja... Nahodha anaweza akawa anakwepa sana miamba majini, lakini kama kuna abiria anachomoa mbao maji yaingie umahili wa nahodha kwenye kukwepa miamba hakutusaidii
 
Ccm ipo dakika za mwisho za kukata roho,mbinu zote zimebuma! Labda nkapa naye aaze kupiga pushup inaweza kuleta hamasa upande wa mazoezi lkn si kubadilisha mawazo ya wananchi ambao tunasubiri tu tar 25.
 
Mkuu, hao uliowataja ni wale wale tu...
1. Mwakyembe ametununulia mabehewa mabovu
2. Magufuli pamoja na mengine, kile kivuko cha bagamoyo ni cha miaka ya 79 hukoo, lakini bei yake imekizidi kile cha azam...

Sasa hao uliowataja bado anao huko huko CCM unadhani ataweza kuwadhibiti..?? Kumbuka kauli ya Pinda liposema .. Mafisadi wana nguvu sana, wanaweza wakaitikisa nchi.. Maana yake unaelewa..??

Haya ishu ya Kinana kusema hadharani kuwa kuwa mawaziri mizigo.. Unadhani tupo salama kwa magufuli...

Na kaulizake za kusema atakayekosea atampandia huko huko, unadha ataweza..?? Nafasi ya uraisi ya uraisi ni management zaidi badala ya kufanya yeye kwa mikono yake.. ATACHOKA.. KIMSINGI KURA YANGU NA YA FAMILIA YANGU NI UKAWA KWA NGAZI ZOTE....

Kuna mijitu ukiiambia ubaya wa CCM utawasiki, CCM imekusomesha..
Huwa nawauliza hivi, mbona wao hawakusopma, CCM haikuwepo..??
 

ccm imeishiwa pumzi haiwezi kuishi tena
 
wana maaaaaaaaaaaaaaaaaamlaka gani ya kikatiba?upumbavu kwenye media
 
Hao wasomi na wataalam si ndo hawa wanatufikisha hapa?sahvi hii ni kufa kwa nyani yaani miti yote itateleza tu,kama wataalam mifano ya dr.bana,polepole,makamba tutajisifu kweli kwamba tunawatu wanaoweza kutusaidia watz,ni ndoto za mchana kweupe,hawa sshvi ni kuchinja tu tar 25,mabadiliko lowasa ndo mpango mzima
 
Magufuli ateue jopo! Thubutu yake anazo hizo akili za kufikiria!!! Labda jopo la Makamba na Nape!!!
 
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufuli ameunda jopo maalumu la wanataaluma na wataalamu kutoka kada mbali mbali ikiwa ni maandalizi ya uundaji wa serikali yake endapo atashinda urais.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, January Makamba alisema kuwa jopo hilo la wanataaluma na wataalamu wa uchumi, biashara, utawala na sheria, kutoka kwenye taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia, na sekta binafsi, wamepewa majukumu maalumu ya kufanya mabadiliko makubwa serikalini kuanzia siku ya kwanza ambayo Magufuli atakuwa madarakani.
Makamba ameyataja baadhi ya majukumu hayo kuwa ni kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili Magufuli aweze kufanya maamuzi ya haraka kuyatatua matatizo hayo.
Majukumu mengine ambayo jopo hilo limepewa ni pamoja na kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti, kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali.
“Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya Serikali inayotekelezwa sasa, kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha Sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania,” alisema Makamba.
Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.
Kwa mujibu wa Makamba, Dk Magufuli ameazimia kuanza kazi kwa bidii na maarifa, ndiyo maana ameunda jopo hilo. Alisema jopo hilo linapaswa pia kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Tanzania. MWANANCHI
UKAWA MPO?
 
Keshashinda huyo anasubiri KUAPISHWA tu. usinisahau na mimi ni mtaalam. he he he heee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…