Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

 
mungu akupe afya njema rais wetu dr john pombe magufuli uwafikie wananchi wengi zaidi na zaidi.
 
Nasikia jamaa amepata stoke jamaa wa bao la mkono
ukiwa na akili za kilofa lazima kila utakalo sikia lazima tu uone ni kweli jaribu kua mtafiti wa mambo na pia kuyachunguza hayo mambo unayoyasikia magufuli kwa jopo hili lazima maendeleo yaonekane we kaa kupiga kelele
 
Hakuna wa kuibeba ccm kwa sasa. Hali mbaya sana. Hao wanaozunguka kumsaidia ndo wanaharibu kabisaa.
(Hivi ccm hamjausoma waraka wa askofu Zackary Kakobe??)
 
Sisiemu hamna jipya subirini bao la mkono msipojikuta mkoo bafuni na sabuni
 
Yote haya yatatimizwa Magufuli akiingia madarakani na kufungua mahakama maalumu ya wala rushwa.

Oktoba 25, mchague Magufuli kwa maendeleo bora.
OVER MY DEAD BODY.....
Nini kiliwafanya watangulizi wake washindwe....?? Kama hamjui basi hataweza...
 
Hakuna wa kuibeba ccm kwa sasa. Hali mbaya sana. Hao wanaozunguka kumsaidia ndo wanaharibu kabisaa.
(Hivi ccm hamjausoma waraka wa askofu Zackary Kakobe??)

Zachary Kakobe ndo nani? we kuwa mtulivu tukutane 25. October
 
Zachary Kakobe ndo nani? we kuwa mtulivu tukutane 25. October

Uwe hewani tu siku hiyo ndugu fesi. Sauti za mabadiliko toka kwa malofa na wapumbavu zitapasua anga zikisherehekea ushindi
 
Magufuli yupo ok, serikali yake itakuwa imara.

Magufuli hawezi kuunda serikali imara ambayo ina watu waadilifu kwasababu hao mawaziri atakaowateua wanatokana na wabunge waliopata ubunge wao kwa njia ya rushwa na ndio hao hao wanaomshauri nani wa kuwa mawaziri; mfano mzuri ni huyo January Makamba ambaye rekodi yake toka shule ya sekondari na mpaka alipogombea ubunge mara ya kwanza ni ya kutokuwa na maadili ya kutukuka!! Akiwa sekondari aliiba mtihani na katika kugombea ubunge mara ya kwanza vielelzo viliwekwa mitandaoni kuonesha kwamba alikopa fedha kwa shemeji yake mzungu na kumuahidi kuwa angezirudisha baada ya yeye kuteuliwa kuwa waziri wa madini!!

Serikali itakayoteuliwa na UKAWA iwapo mgombea wao Lowassa atashinda itakuwa na mawaziri wenye uwezo na waadilifu kwa sababu watakuwa wameteuliwa kutokana na wananchi ambao sio wabunge !!! Kumbuka kuwa ukawa wameahidi kutupa katiba itakayotokana na mapendekezo ya wananchi kama ilivyotolewa na jaji Warioba. Kuunda baraza la mawaziri sio lazima lifanyike mara baada ya kuchaguliwa bali linaweza kuahirishwa huku serikali ikiendeshwa na makatibu wakuu. Kipengele cha kuwa na mawaziri wasio wabunge kinaweza kubadilishwa na bunge under emergency legislstion mpaka hapo katiba tuitakayo itakapopatikana!!

Wale wanaompakazia Lowassa kuwa ni fisadi hivyo ataunda serikali iliyosheheni marafiki zake wafanyabiashara wanakosea kwani wakumbuke kwamba Lowassa akifanikiwa kuwa Rais atathibitiwa na katiba ya wananchi ambayo ina checks na balances ambazo hazimpi nafasi ya kufanya mambo kama atakavyokuwa anataka!! Ukisoma rasimu ya katiba ya Warioba ambayo UKAWA wameahidi kuiptisha utakuta kuwa taasisi nyingi imara zitakuwepo kuimalisha utawala bora ikiwemo MAHAKAMA ambayo mkuu wake ataidhinishwa na bunge tofauti na sasa; taasisi za kupapambana na rushwa zitakuwa huru na sio chini ya Rais hivyo kuweza kuthibiti rushwa bila kuingiliwa; viongozi wa taasisi zote nyeti itabidi wachujwe na kuthibitiwa na bunge ambalo nalo pia wajumbe wake watakuwa na ukomo!!! Hivyo ukawa wana nafasi nzuri ya kutupatia serikali bora kuliko ccm ambao wao wanataka status quo [ ccm ni vile vile!!!] Naomba kutoa hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…