Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Tunaitegemea serikali yenye mabadiliko ya kweli ya ndugu magufuli
 
Warioba na wengine ktk kamati ile ni wasomi sana lakini Maoni Yao yalikataliwa kabisa na CCM ndo maana ikazaliwa UKAWA
 
Maandalizi ya Kuleta Mabadiliko ya Haraka na ya Kweli. Pia, tunapenda kutoa taarifa kwamba, mgombea wetu, Dkt. John Pombe Magufuli, ameunda jopo la wanataaluma na wataalamu huru magwiji wazalendo wa uchumi, biashara, utawala na sheria, kutoka kwenye taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia, na sekta binafsi, kwa ajili ya maandalizi ya kufanya mabadiliko makubwa Serikalini kuanzia siku ya kwanza atakayokuwa madarakani.

Ndio asai zipi hizo? Jeshi na asasi za nje ya nchi?
 
Tunawakaribisha sana tulikuwa tunawataka kwani wao ndio chanzo cha MAISHA MAGUMU TULIYONAYO
 
Maji yamezidi unga, hakuna ugali tena sasa unapikwa uji. Tayari watanzania wameshaamua kufanya MABADILIKO. Hakuna namna tena ya kubadilisha mambo.

Jamaa wanaandaa 'ilani' mpya. wameona iliyopo haiwashawishi watanzania.
 
haya ndo mabadiliko tunayoyataka! siasa weka pemben ujuzi na elimu itawale, kazi ifanyike
Huyu ndo raisi tunayemtaka,
 
Kwani lile jopo la vigogo 32 limeshindwa kazi!?
 
hawana msaada hao zaidi ya kwenda kuwaita wananchi wapumbavu name malofa
 
Waje haraka maana hao ndio Mapapa waliohiaribu Nchi ili tuongeze hasira zetu dhidi ya ccm na Magufuli wao.
 
Hatimaye baada ya kampeni kufika maji ya shingo jaribio la kuokoa jahazi limeanza ! Hata hivyo limechelewa .
 
Back
Top Bottom