Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Wadau hakuna namna nyingine ya kuchanganyikiwa zaidi ya hii!

Labda kwa jicho moja tuone hivyo,Labda kwa jicho lingine tuone kama matokeo yalishaamuliwa kabla ya kampeni kuanza.Watoto wa mjini wanasema "CCM walikuwa wanatuejoy, walishapanga matokeo kabla ya mechi".

Soma hapa

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufuli
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufuli ameunda jopo maalumu la wanataaluma na wataalamu kutoka kada mbali mbali ikiwa ni maandalizi ya uundaji wa serikali yake endapo atashinda urais.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, January Makamba alisema kuwa jopo hilo la wanataaluma na wataalamu wa uchumi, biashara, utawala na sheria, kutoka kwenye taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia, na sekta binafsi, wamepewa majukumu maalumu ya kufanya mabadiliko makubwa serikalini kuanzia siku ya kwanza ambayo Magufuli atakuwa madarakani.
Makamba ameyataja baadhi ya majukumu hayo kuwa ni kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili Magufuli aweze kufanya maamuzi ya haraka kuyatatua matatizo hayo.
Majukumu mengine ambayo jopo hilo limepewa ni pamoja na kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti, kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali.
"Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya Serikali inayotekelezwa sasa, kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha Sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania," alisema Makamba.
Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.
Kwa mujibu wa Makamba, Dk Magufuli ameazimia kuanza kazi kwa bidii na maarifa, ndiyo maana ameunda jopo hilo. Alisema jopo hilo linapaswa pia kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Tanzania.

Huyo ndiye Magufuli, jembe @ katapila
 
Ikulu hatupeleki mgonjwa anayetetemeka mikono, hawezi hata kushika kipaza sauti kwa mkono wa kulia, anatembea kama nyani maana mwili wote unatetemeka. Ikulu hatupeleki mtu anayejinyea ovyo maana hatuna bajeti ya pampasi. Ukome kutukana tunajua udhaifu mwingi mno wa fisadi wenu lowasa.
Angalia waliotoa matusu hayo walisha r.i.p
 
tume inaundiwa tume?? wakati mwananyamala wanatibu tezi dume.....cc roma mkatoliki...viva ukawa vivaaaaaa
 
Tunapenda kuwataarifu wanachama wetu na umma wa Watanzania kuhusu masuala yafuatayo:

Mwenendo wa Kampeni za CCM

Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, na Mgombea Mwenza, Ndugu Samia Hassan Suluhu, wameendelea kufanya kampeni katika maeneo mbalimbali nchini..

Hadi jana, tarehe 10.10.2015, Dkt. Magufuli alikuwa amekwishatembelea Mikoa 22 na Majimbo 203. Amekwishafanya mikutano mikubwa rasmi 240 na mikutano 865 ya kusimamishwa na wananchi njiani, hasa wananchi wa vijijini. Dkt. Magufuli amekuwa akitumia usafiri wa barabarani, ambapo hadi sasa ametembea kilomita 31,467 kwa barabara kuu, barabara za mikoa, barabara za wilaya, barabara za mlisho (feeder roads), na barabara za mijini na vijijini.

Watu wengi wamekuwa wanajitokeza kwenye mikutano yetu. Lakini la muhimu zaidi ni hamasa na matumaini wanayopata baada ya kumuona jukwaani na kumsikiliza Dkt. Magufuli. Wananchi wanapoondoka kwenye mikutano yetu ya kampeni wanakuwa wamepata fursa ya kumsikia mgombea wetu kwa kitambo kinachotosheleza, wamemuelewa, wameelewa sera za CCM na wameshawishika kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi.

Tunaingia katika ngwe ya mwisho ya kampeni zetu. Tangu kampeni zianze hadi sasa, ushindi wa CCM unajidhihirisha. Hata hivyo, katika kujihakikishia ushindi na kuongeza kiwango cha ushindi, katika ngwe hii ya mwisho, tumeanza kampeni nzito.

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, ameanza ziara ya kampeni katika majimbo 64. Vilevile, viongozi wengine wa CCM, akiwemo Rais na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa, nao wataanza safari za kuzunguka nchi nzima kumuongezea kura Dkt. Magufuli na wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Tutatumia helikopta nne kwa ajili ya shughuli hii. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wataendelea kutumia usafiri wa gari hadi mwisho wa kampeni, isipokuwa pale tu itakapokuwa hakuna budi.

Maandalizi ya Kuleta Mabadiliko ya Haraka na ya Kweli

Pia, tunapenda kutoa taarifa kwamba, mgombea wetu, Dkt. John Pombe Magufuli, ameunda jopo la wanataaluma na wataalamu huru magwiji wazalendo wa uchumi, biashara, utawala na sheria, kutoka kwenye taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia, na sekta binafsi, kwa ajili ya maandalizi ya kufanya mabadiliko makubwa Serikalini kuanzia siku ya kwanza atakayokuwa madarakani.

Dkt. Magufuli amelipa jopo hili majukumu yafuatayo:

1. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

2. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

3. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali;

4. Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya Serikali inayotekelezwa sasa.

5. Kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha Sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania;

6. Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.

7. Kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa.

8. Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli.

9. Kutengeneza rasimu ya mpango-kazi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika;

10. Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini.

Dkt. Magufuli ameazimia kuanza kazi mara moja kwa bidii kubwa na maarifa mapya.


Imetolewa na:-

January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni


Da mwaka huu kaz ipo Mangufuli alisema anajua matatizo ya hii inchi sasa unaunda jobo la nini??

Mimi nasema watanzania tusifanye makosa ni kuwatoa tu maccm hamna mpya yale yaleeee.
 
Ikulu hatupeleki mgonjwa anayetetemeka mikono, hawezi hata kushika kipaza sauti kwa mkono wa kulia, anatembea kama nyani maana mwili wote unatetemeka. Ikulu hatupeleki mtu anayejinyea ovyo maana hatuna bajeti ya pampasi. Ukome kutukana tunajua udhaifu mwingi mno wa fisadi wenu lowasa.
Nyie watu mtaacha lini kudihaki watu, wenzio walishaacha kutoa maths km haya unataka kutangulia mbele za haki?
 
Magufuli ndio Rais wa awamu inayokuja

Mkuu bila kuegemea upande wowote ule, kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti, huko uliko au popote pale unapotaka, fanya utafiti wako binafsi uone katika watu 10 ni wangapi wako na CCM (Magufuli) na wangapi wako na UKAWA (Lowassa). Majibu utakayoyapata ni siri yako. Mwaka huu ni tofauti na chaguzi zingine zote za nyuma. Tukutane 25 October.
 
Ccm lazima wakatwe safari hii. Watauba kura lkn bado hazitawatosha
 
Ccm Ni Sikio La Kufa

Ukikuta Ccm Inapambana Na Nyoka Porini Msaidie Nyoka Ili Kuiuwa Ccm Maana Mbele Ya Safari Najua Nyoka Atakusaidia Siyo Ccm.
live bila chenga na umeamua kuwapa ccm makavu
 
Jopo la uchunguzi la mikataba feki!

mitambo ya gesi naskia ni ya mtu binafsi! big no kura yangu UKAWA
 
Hahaha! Kazi kwelikweli! Isije ikawa shuka inakumbukwa asubuhi! Huko watapokwenda hao wengine wasanii watakuwepo pia!? Huyo Kinana si alishazunguka nchi nzima ina maana hawakumuelewa!?

Watu wamechoka, wanaelewa mabadiliko tu.

Ccm wana kazi ngumu.

#kazikwelikweli
 
Mnamshangaa Magufuri wakati yeye anaelewa alikuwa anafanya kazi na si maigizo kama nyie ..kapiga kazi na kazi imeisha mtaani sahivi kaanza na kupanga kikosi tayari, nyie endeleeni kutengeneza maigizo huko serengeti
Huyu ndo Magufuri, hapa ni kazi kwa kazi ..Hapa ni kazi tu.
 
Nikisikia neno ccm nakumbuka bunge la katiba chuki inazidi hasa nikimuona yule mama mwenza..hebu jaribu kukumbuka alivyokuwa naibu mwenyekiti maneno yake

Mwenza alikuwa anatema mitusi ya laana. Naona kule ccm ukiweza kuwatusi au kuwapiga wazee unapewa motisha ya uongozi.

Ccm kwangu ni kichefuchefu.
 
Kwa miaka miwili Kinana alizurura akitafuna kodi zetu

Ni kipya kipi atawaeleza Watanzania safari hii?

Kila alikopita aliilaumu serikali ya CCM kwa kushindwa kazi

Je Magufuli hakuwepo kwenye serikali hiyo kama Waziri?

Sasa leo anapopanga kurudi kwa wananchi wale wale

Huku ni kukosa aibu, haya na dalili ya kuchanganyikiwa.

Ccm ni ile ile,
Ccm haina jipya,

#kazikwelikweli
#mabadiliko
 
Back
Top Bottom