Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Mkakati huu utawasaidia kuweza kufahamu ni maeneo yapi yenye matataizo zaidi na namna ya kuweza kuyakabili. Tunahitaji wtu wenye yhakika na wananchokifanya, sio watu wa kubabbaisha na kulaghai watanzania. Magufuli anajiamini kwenye analolifanya anajua watanania wanahitaji nini na kwa wakati gani...Magufuli for Change M4C

Hahahahaha!! M4C movement for change.
Kumbe kashahamia Chadema
 
Dr Magufuli ameanza kazi rasmi. Kama Rais tumepata. This time Watanzania hawajafanya makosa.
 
Daaah aongeze tu mishahara na kuimarisha uchumi ili fedha iwe na thamani mh Rais
 
BILA KATIBA YENYE RASIMU YA WARIOBA, TAKATAKA ZAKO HIZO HAPO CHINI NI ULAGHAI. VYEMA SASA UZINGUMZIE KATIBA SIYO KUPIGA PUSHAP, LA SIVYO TAREHE 25/10 UTALIA KILIO AMBACHO AKIELEZEKI

Dkt. Magufuli amelipa jopo hili majukumu yafuatayo:

1. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

2. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

3. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali;

4. Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya Serikali inayotekelezwa sasa.

5. Kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha Sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania;

6. Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.

7. Kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa.

8. Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli.

9. Kutengeneza rasimu ya mpango-kazi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika;

10. Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini.

Dkt. Magufuli ameazimia kuanza kazi mara moja kwa bidii kubwa na maarifa mapya.
 
Na Leo kidatu wanazima mitambo Giza lizidi kutamalaki
 
Anaandaa mikakati ya nyumbani kwake lakini si ikulu
 
Wana bodi!
Hali ya CCM ni mbaya sana. Hawakutegemea kabisa kuwa watanzania watawakataa kama inavyotokea sasa. Na katika ku-panic na kuonyesha taharuki wamejikuta wanafanya mambo yanayozidi kuwafumbua wananchi macho na kuiona CCM ni kundi la matapeli:
1; Matusi ndio imekuwa ilani yao ya uchaguzi.
2: Magufuli ameshindwa kujinadi kwa kutumia jina la CCM na badala yake anajinadi kama mgombea binafsi.
3: Na kali ya funga kazi ni hii iliyotokea leo: wamekuja na mpango wa maandalizi ya ilani mpya huku ile ya zamani wakiwa wameitupa. Hebu oneni huu utapeli:



My take: CCM wanazidi kuonyesha utapeli, ulaghai na kuwa ni wale wale wala hawakuwa wamejiandaa. Hivi kweli inaweza kuingia akilini mtu kusema Chama kilichotawala muda wote huu haya mambo kilikuwa hakiyajui na sasa ndio wameshtuka na wanaanza kuchunguza? Si ni kwasababu wameona hali ni mbaya ndio maana wanakuja na mipango mipya huku hata iliyopo kwenye ilani haijatekelezwa?

Binafsi siioni kwa mtazamo wako huo. Ni vizuri kufanya hivyo ili watekeleze vizuri yaliyomo kwenye ilani yao na ahadi za papo kwa papo wanazozitoa majukwaani - maana mgombea urais, makamu wake na wapambe wote wameenda wakiahidi! Kinachonisumbua katika hili ni dharau wanayoionyesha kwa Watanzania, kwamba wao hata tusipowapigia kura tayari wameshinda! Hii kwangu ni dharau kubwa kwa demokrasia, angalabhu wangeyafanya kimyakimya. Najua hii ni mojawapo ya mkakati wao kuwakatisha tamaa wapiga kura walio kinyume na wao lakini hawakuiangalia vyema upande mwingine
 
Nakwazwa tu na wafanyabiashara uchwara wakigeni. Raisi wangu El awaondoa Kariakoo siku ya pili ofsini. Nasubiri tamko cku ya kuapishwa.

Ofisi za biashara wilaya ya Kinondoni nk zingebinafsishwav
 
Yaani mnachunguza wakati mlisema matatizo ya watanzania mnayajuwa...!!!
Anyway baneni matumizi na ongezeni juhudi kwenye haya
1. Fungeni wote wa mishahara hewa
2. Halmashauri zenye hati chafu watieni ndani wote
3. Kamata wakwepa kodi wote
4. Futa misamaha ya kodi
Ngalikihinja umenena vema, kama matatizo ya watz kwa zaidi ya miaka 50 tuliyowapatia ridhaa ya kututawala hayajatatuliwa basi hawafai kupewa tena nafsi ya kutuongoza. Tuwape na wengine kabda twaweza sogea.
 
Wameunda na kamati ya kutatua kero za wananchi. Kana kwamba kero zimeanza leo, au ni wageni
 
Back
Top Bottom