Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

kama anaunda serikali wakati serekali halali ya JK bado ipo kikatiba basi ni uhaini.
 
labda kwa jicho moja tuone hivyo,labda kwa jicho lingine tuone kama matokeo yalishaamuliwa kabla ya kampeni kuanza.watoto wa mjini wanasema "ccm walikuwa wanatuejoy, walishapanga matokeo kabla ya mechi".

Soma hapa

mgombea urais wa chama cha mapinduzi (ccm), dk john pombe magufuli.

Mgombea urais wa chama cha mapinduzi (ccm), dk john pombe magufuli ameunda jopo maalumu la wanataaluma na wataalamu kutoka kada mbali mbali ikiwa ni maandalizi ya uundaji wa serikali yake endapo atashinda urais.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam leo, mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ccm, january makamba alisema kuwa jopo hilo la wanataaluma na wataalamu wa uchumi, biashara, utawala na sheria, kutoka kwenye taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia, na sekta binafsi, wamepewa majukumu maalumu ya kufanya mabadiliko makubwa serikalini kuanzia siku ya kwanza ambayo magufuli atakuwa madarakani.

Makamba ameyataja baadhi ya majukumu hayo kuwa ni

dkt. Magufuli amelipa jopo hili majukumu yafuatayo:

1. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

2. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

3. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika serikali;

4. Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya serikali inayotekelezwa sasa.

5. Kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa watanzania;

6. Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.

7. Kupendekeza miundo na idadi ya wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa.

8. Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli.

9. Kutengeneza rasimu ya mpango-kazi wa utekelezaji wa ilani ya ccm na ahadi alizozitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika;

10. Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini.

Dkt. Magufuli ameazimia kuanza kazi mara moja kwa bidii kubwa na maarifa mapya.

----- mtupu. Ataongoza ile nchi ya kwenye kitabu cha kusadikika cha marehemu shaban robert, lakini sio hii tanzania. Mtu anaongea bila breki, ivi ana familia??????????
 
Hiyo mtoa mada anaejiita chomoa chupi matakoni(ccm) nae kaishiwa pumzi!!!!! Magufuli aunde jopo la nguvu za Giza!!!
 
CCM kweli mna hali mbaya ile timu kampeni yenu watu 32 Imefia wapi?Mmeamua kujimaliza wenyewe Mkapa anakuja kutusaidia UKAWA kuizika rasmi ccm tarehe 25.10.2015 .

LOWASA HUYO ANAKUJA NA TANZANIA MPYA.
 
Hayo ni maandalizi mazuri. Hakuna sababu ya kupoteza muda baada ya uchaguzi. Wananchi wanakiu ya mabadiliko. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mkuu,

Nimefurahishwa na namna ulivyotoa comment yako,,imeonyeshwa wazi hufurahishwi na mambo yanayoendelea,,lakini pia huchukulii suala la uchaguzi na uendeshaji wa serikali kishabiki,,naamini na nadhani na wewe unaamini despite of wana ccm wengi wabaya na mafisadi(kama walivyokua kina lowassa,kikwete,chenge,karamagi n others) kuna wana ccm wenye nia na dhamira ya kulipaisha taifa hili,,,kina magufuli,mwakyembe,mwandosya,sitta,j.makamba na wengineo,,ninaamini era ya wana ccm walio na dhamira safi inakuja kwenye awamu hii ya 5

Tuondoe wakuu wa wilaya wrote.tuondoe mishahara ya wabunge kazi ya kujitolea
 
tupo pamoja sana! na mimi invisible fun of MAGUFULI nimeshatembea mikoa ya Mtwara, Pwani, Mwanza na Morogoro... nimeweza kushawishi na kuwabadilisha wafuasi 100 wa UKAWA kumpigia KURA YA NDIO MAGUFULI....na natumaini kila mmoja ataweza kushawishi wengine 5.... target yangu ni Kumpatia magufuli Kura 1000 + za ndio....
 
Ikiwa wamejidhihirishia ushindi, hawa wengine wanazunguka ili iweje kama si kumaliza pesa za walipa kodi bila sababu. Ushindi wenu, mna uhakika, mnaranda nini...
 
Back
Top Bottom