Benny Haraba
JF-Expert Member
- Dec 7, 2012
- 13,336
- 12,370
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mzee Kinana ametofautiana msimamo na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu mkataba wa bandari.
Kinana anasema wamejitokeza watu wameanza kuhoji, wako wanaohoji kwa nia njema ya kujenga ya uzalendo, hatuwezi kusema kila anayehoji anania mbaya, wako wanaotetea mkataba na wametoa ushauri mzuri, serikali imesema itapokea kila ushauri utakaotolewa, Chama Cha Mapinduzi kimesema serikali isikilize, kwa hiyo serikali inasikiliza ushauri, inasikiliza hoja, haya yote yatafanyiwa kazi, haiwezekani Rais akapuuza haya yote.
Lakini Chongolo yeye anasema Serikali ianze utekelezaji haraka na isisikilize kelele za wajinga wanaopinga mkataba huo.
Unyumbu ni tabia ya watu waliopewa ghamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kutumikia malengo ya kundi fulani, (conflict of interest), ama uoga, (amygdala), kuogopa viongozi wao