Kinana: CCM ni kubwa kuliko Serikali

PARY SUPREMACY

Nini maana ya chama kushika hatamu?

πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Chama kuandaa watuβœ…

πŸ‡ΉπŸ‡ΏChama ...............βœ…

πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Chama kupima mafanikio βœ…πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Chama ndicho kinaunda serikali.. kwa hiyo ni sahihi: kwa sasa CCM ndiyo maboss na wana haki ya kuisimamia serikali kuhakikisha wanatekeleza ilani yake.
Ni kweli ndo maana mwenyekiti wa CCM anaagiza viongozi wa serikali wale kwa urefu wa kamba zao maana hiyo ni sera ya CCM.
 
Jiwe alikuwa hajali hayo mambo ya kutenganisha mpaka kati ya serikali na chama chake ndio maana
Alikuwa anapokea wanachama wapya katika mikutano ya serikali,
Anafanyia vikao vya chama ofisi namba moja,
Walinzi wake wanavaa sare za chama,
Alimteua kanali wa jeshi kuwa kada wa chama,
Alimteua kada wa chama kuwa mkuu wa watumishi!,
Alitumia vyombo vya dola kuwa trepu wanachama wenzake waliokuwa wanamsema!

Mambo ni mengi, hayo ni baadhi tu tuliyoyaona kwa nje.
 
Dunia imebadilika mno.

Mambo ya chama kushika hatamu yameshapitwa na wakati.
Ili chama kishike dola, kishinde chaguzi zake
Lazima kiwe kwenye mfumo huu wa ccm
Yaani chama alafu $

Ova
 
Kinana anajisahau kuwa yeye ni makamu mwenyekiti, maana yake anasubiri kupangiwa kazi na mwenyekiti. Mtendaji mkuu ni katibu mkuu
 
Kinana anajisahau kuwa yeye ni makamu mwenyekiti, maana yake anasubiri kupangiwa kazi na mwenyekiti. Mtendaji mkuu ni katibu mkuu
Kwani lengo la ccm ni nini?

Wao wanataka waendele kushika $

Ova
 
Kwani lengo la ccm ni nini?

Wao wanataka waendele kushika $

Ova
hujanielewa, Kinana ni makamu mwenyekiti, hana sauti kwenye chama kama alivyokuwa katibu. Yeye sasa hivi ni wa kusubiri kupangiwa majukumu pale mwenyekiti anapokuwa hana nafasi ya kutekeleza baadhi ya mambo.
 
anamaanisha ccm ikiiba rasilimali za nchi ambazo ni mali za wananchi, basi serikali haiwezi kumuajibisha yule mwanachams wa ccm aliyeiba
 
anamaanisha ccm ikiiba rasilimali za nchi ambazo ni mali za wananchi, basi serikali haiwezi kumuajibisha yule mwanachams wa ccm aliyeiba
 
Ibara ya 34 (1) (2) (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko wazi:

34 (1) Kutakuwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano na pia juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara.

"mambo yote"

...


Nchi inaongozwa na katiba wala sio chama. Na katiba imeweka wazi kuwa Serikali ndio yenye mamlaka katika mambo yote, Kinana anazingua.


Yesu ni Mwokozi
 
Baada ya kuwa Rais, akaamua kuachana na ilani na mambo ya chama, nini kitafuata kikatiba


JESUS IS LORD
Hawezi kuachana na Ilani huku akijitambulisha kama mwanachama wa chama husika cha siasa. Ukishasema ww ni mwanaccm maana yake unafuata ilani ya ccm, kama ufanyayo hayapo ndani ya ilani basi utarekebisha hiyo ilani ili yawepo. Labda uulize akijivua unanachama ambapo jibu lake unalo tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…