Kinana kuongea na mamlaka bodaboda wabebe abiria zaidi ya 1 (mshikaki)

Muwa mtamu

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2020
Posts
847
Reaction score
1,599
Nimeshangaa kuona na kusikia Kinana akiwaambia bodaboda kuwa ataiambia mamlaka ya usimamizi usalama barabarani waondie zuio la mishkaki yaani kubeba hadi abiria 3.

Sababu kuu anasema hii itaongeza kipato kwa waendesha boda boda.

Kibaya zaidi akasema kuwa...kuna shida gani kama abiria wenyewe wametaka kubebwa hadi watatu.

Huu sio uongozi kwani wote tunafahamu jinsi boda boda zinapoteza maisha ya watu wengi.

Kiongozi asiyejali maisha ya raia huyo ni muuaji

========
Your browser is not able to display this video.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amesema CCM inakwenda kuzungumza na Serikali kuangalia sheria ya kuzuia usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda kuruhusia kubeba abiria zaidi ya mmoja (mshikaki)

Kinana amesema hayo wakati akipokelewa na Viongozi, Wanachama wa CCM na Wananchi wa Bariadi mkoa wa Simiyu, ikiwa ni mendelezo wa ziara yake ya kuangalia uhai wa chama, utekelezaji wa llani ya CCM na kuongea na Wananchi katika maeneo mbalimbali.

Una mtazamo gani juu ya kauli hii?.

Pia soma:
- Polisi: Bodaboda msizidishe abiria zaidi ya mmoja
 
Hakuna shida yeyote. Kama ajali tunaona magar yanavyo pata ajali na kuuwa watu mbona serikali haizui kubeba abilia zaid ya mmoja. Kama abilia mwenyewe wamelizika acha wapebwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…