Elections 2010 Kinana na Dr Slaa - Live Star TV

Elections 2010 Kinana na Dr Slaa - Live Star TV

Nimemuangalia mtangazaji huyu wa star tv leo akiendesha mahojiano na Dk Slaa,
nilichokiona ni kwamba huyu mtangazaji alikuwa akiongea na slaa kwa kumtegatega hivi au kumwekea maneno mdomoni lakini slaa alikuwa makini mno kulitambua hilo.....na hadi akafikia hatua ya kumkemea kuwa kama hataki kusikiliza hoja zake kwanini ana muuliza na kwanini alimualika?......Mabuga akanywea na kwa wataalam wa kusoma lugha ya macho ni kwamba pia aliogopa na kubabaika!
Ushauri,.....
Ni mara nyingi paul mabuga amekuwa akitoa maneno ya kumfanya Slaa aonekane kama ni mtu ovyo ovyo, sasa sijui ni upeo wake(Mabuga) unaamini hivyo, au anatumwa??.......Paul usiwe hivyo wenye akili watakudharau mnoo!!.., kama ndivyo ulivyo, hiyo kazi acha rudi kwenye kazi yako ya ualimu wa shule ya msingi...
DK Slaa ni mtu makini mno,.....
Paul asirudie kuongea na watu makini kama Slaa kirahisi rahisi au bila kutumia akili kama mabavyo angeweza/anaweza au anavyoongea na watu aina ya Jakaya Kikwete, Masanja Mkandamizaji, Makamba, Kingwendu, Kinana, Joti..nk
 
Ila slaa karuka viunzi mwanzo nilihisi kama dr atashindwa kummudu nikataka kuacha kuangalia(nna roho laini) ila muda ulivyozidi slaa akachanganya akanogesha nikaona kuangalia peke yangu sio ishu nikaanza kuita watu tuwe wengi!
 
Dr.Slaa is preseindential material sio mtut wa kucheza viduku..so mtangazaji anajua anaongea na level ya kina kingwangala
 
Baada ya uchaguzi, JK tusimzuie kuendelea kuwa Raisi wa famili yake maana hata yeye alikwisha kutupasha ya kuwa URAISI ni suala la kifamilia..............................................GO DR. SLAA........GO TO IKULU
 
Mwingine ni Doto wa StarTV na yule mnyoa "O" mwenzie hua siwaelewi kabsaa hasa jumamosi na kipindi chao kile
 
Watarudia leo saa 5 usiku, lakini nahic nimbinu nyingine ya ccm kumpunguzia kura slaa, kwan wanamuuliza maswal akitaka kujibu tu wanasema mda hautoshi,lakin kinana anajieleza mwenyewe mpaka anachoga bila kukatishwa. Inakera kwakwel, lakin kunamtu amepiga cm na kulizungumzia hli, mtangazaji aibu imemjaaa....
 
Sasa Kinana ndio mgombea wa CCM au?

Mgombea wa CCM anahitaji aandaliwe majibu kwa maandishi. Haya mahojiano ya kumkutanisha na Dr. Slaa hayatatoa fursa hiyo hivyo bora aingie mtini tu. Wanajua kuwa hata kama Kinana atachemsha watasema kuwa siyo mgombea.
 
Ila slaa karuka viunzi mwanzo nilihisi kama dr atashindwa kummudu nikataka kuacha kuangalia(nna roho laini) ila muda ulivyozidi slaa akachanganya akanogesha nikaona kuangalia peke yangu sio ishu nikaanza kuita watu tuwe wengi!

Hamna lolote yule mavuga asingeweza chochote kwa slaa, sanasana kajifunua tu upeo wake kuwa hautoshi kuwa mwandishi/mtangazji....siku nyingi anajifanya anajua kilakitu!!
 
Unajua mimi nilifikia hatua ya kukasirika, unajua wenzetu ulaya wanapokuwa wanaongea na Contestant huwa wana heshima sana, lakini huyu jamaa Mabuga seems hana protokol yoyote, kwanza alikuwa hajui anaongea na nani mpaka Dr.Slaa akamkumbusha by gesturing, halafu yeye upeo wake mdogo, bado hajafikia level ya kuhoji wagombea Uraisi, yaani ulikuwa ukiangalia utagindua hilo, anauliza maswali utafikiri anaongea na mtoto wa chekechea, the guy is too ollusional, hana point kabisa, mpaka kuna jamaa mmoja akaamua kumwambia kabisa, naona pale aliona aibu kweli kweli.

Slaa Go Baba, tukomboe na huu ujinga wakina Kinana
 
Wadau mlio karibu na startv tuombeeni waonyese replay jioni tulio wengi tupo makazini. Nina hamu ya kuona kipindi hicho, and if not possible tupatiwe japo youtube.
 
Dr.Slaa is too much for kinana,ilitakiwa upande wa kinana kungekuwa na mtu kumi jamii ya Magufuli.Dr.Slaa ni zawadi ya Mwenyezi Mungu kwa Tanzania.Hii ni tunu ya TAIFA LETU
2010 HATUDANGANYIKI.
 
Wakati tukisubiri hisani ya Tangibovu wa Youtube kutundika mdahalo wa Dr. Slaa na Kinana ktk StarTV , tujikumbushe sera za CHADEMA kama zilivyotundikwa na Tangibovu:
 
Last edited by a moderator:
Kilicho nishangaza nipale nilipo muona anamuuliza swali drslaa lakin hataki ajibu, eti mda hautoshi lakin kinena anaongea upuzi wake mpaka anaacha mwenyewe bila hata kukatishwa! aah! Wametia aibu juzi niliwambia startv imepoteza dira watuwalifikiri na tania, ila leo imejidhihirisha, naye yule christina hafai kuwa mwandishi wa habari kabisa labda kusoma magazeti tu asubuhi, yaan kinana hajamuuliza follow up questions hata moja zaidi ya kujichekesha kwa msomali da! Kwli kazi ipo.Yaan anashindwa hatakumuambia mda umeisha mpaka wanaamua kumkatia ,da! aibu tupu. Ila bado dr slaa anatisha.
 
Slaa anaweza, anapanga point sana.yaani hawa CCM kila kitu wao hawawezi! eti haiwezekani kuwa na mawaziri 20! ajabu kweli kweli.
 
Toeni wito kwa watanzania wapenda maendeleo kuwa wagombea wote wa nafasi mbali mbali wanaojificha ficha wasipewe kura wana ajenda za siri kwa watanzania ambazo hawataki wazijue. Wao wanataka kwenda katika majukwaa ya kisiasa nakuongea bila kuulizwa maswali.

Inabidi wagombea wa mtindo huu wakataliwe na jamii ya kitanzania. Huwezi kumpa kazi mtu ambaye hakufanya usahili.
 
Back
Top Bottom