Wandugu, kwanza mimi nilipata mashaka tangu awali niliposikia kuwa kutakuwa na mahojiano 'live' kwenye kituo cha StarTv. Sababu ni moja tu, kituo hicho kinamilikiwa na kada wa sisi m anayejipachika cheo cha Dr. kama ilivyo kwa kinara wao 'njaa kali'. Kama hivyo, ndivyo, ninyi mlitarajia nini???? Hicho chama ni mabingwa (duniani) kwa uchakachuaji. Wasingekubali mahojiano yamnufaishe Rais wetu Mtarajiwa Dr. Slaa badala ya fisadi wao. Lakini kwa mtazamo wangu wamenoa kwani kwa mtu msomi wa karba ya Slaa hiyo ndiyo ilikuwa fursa muafaka ya kuonesha usomi wake. Alibaini mwelekeo wa 'watangazaji njaa' na kuwa-control vizuri. Angekuwa amebanwa hivyo 'msomali', angepanda hasira za kiharamia.
Wandugu, tusikatishwe tamaa na mbinu za kifisadi wenye maajenti hadi kwenye vyombo vya habari. Mwaka huu ni wetu na nchi inarudi mikononi mwetu wanyonge. Tukaze buti na kampeni zetu kwa ndugu na jmaa ziendelee kwa nguvu zote ili hatimaye tuwaondoea mafisadi warudi kuongoza familia zao, kama walivyosema kuwa urais ni suala la kifamilia.
Paul Mabuga, anza kutafuta nchi utakayoishi baada ya Rais wetu mpya kuapishwa mbele ya umati mkubwa wa wazalendo Jijini Dar.
Pipoooooooooooooz ...........