Kinana: Tusipendeleane, tusibebane

Kinana: Tusipendeleane, tusibebane

Niliona hiyo clip.
Kama ni ya karibuni, wameshtuka; akili zinawarudia!
Hakuna jipya hapo. Mnapangwa kijanja mdhanie chama chao hakina tatizo na uongozi wa chama hauna tatizo bali serikalini kuna tatizo.
Kwani serikali inaongozwa na chama gani?
Anatuliza upepo tu.
 
Hakuna jipya hapo. Mnapangwa kijanja mdhanie chama chao hakina tatizo na uongozi wa chama hauna tatizo bali serikalini kuna tatizo.
Kwani serikali inaongozwa na chama gani?
Anatuliza upepo tu.
Mkuu ulisikiliza hiyo clip?
 
Kuna kikao cha kimkakati cha wabunge wa CCM kilifanyika huko Dodoma kupitisha hayo makolokolo ya DP world, Je Mzee Kinana nakulijua hilo? kama alilijua alichukua hatua gani kama mkuu wa chama?
Yeye mwenyewe ni mguu ndani mguu nje
 
Mkuu ulisikiliza hiyo clip?
Sina haja ya kusikililiza.
Hiyo mbinu anaitumia mara ya pili.
Kuna wakati awamu ya Kikwete hali ilikuwa mbaya sana huyu Kinana akaanza kuongea maneno kama haya kubadili upepo.
Umemsahau nani alisema kuna mawaziri mizigo?
 
Msomali amewalikbia al shababu na Kuja kutusumbua hiku
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM komredi Kinana amesema Chama tawala ni Lazima kiwe na Nguvu ya kuishughulikia Serikali badala ya kuwa sehemu ya walalamikaji kama Wananchi wa Kawaida

Kinana amesema watapeleka pendekezo kwenye Halmashauri Kuu ya CCM ili Chama kujitoa Tamko Waziri fulani hafai basi Kesho yake asubuhi tu awe ameshatumbuliwa, haiwezekani kulea Mawaziri Wavivu Hiki kitakuwa Chama gani kisicho na Nguvu

Aidha Kinana amesema tabia ya Wabunge kupitisha kila Kitu kinacholetwa na Serikali ifike mwisho na Serikali ielezwe Wazi kwamba Watendaji wake ni Wavivu

Mzee Kinana amesema hayo kwa hasira sana kwenye mkutano wa hadhara ambapo Wananchi walimshangilia sana

Chanzo: Clip ya Kinana kwenye ukurasa wa twitter wa Ananilea Nkya

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Mkuu, nasikiaga hao huwa ni cream na wanafanyiwa vetting? Sasa wanakuwaje tena wavivu?
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM komredi Kinana amesema Chama tawala ni Lazima kiwe na Nguvu ya kuishughulikia Serikali badala ya kuwa sehemu ya walalamikaji kama Wananchi wa Kawaida

Kinana amesema watapeleka pendekezo kwenye Halmashauri Kuu ya CCM ili Chama kujitoa Tamko Waziri fulani hafai basi Kesho yake asubuhi tu awe ameshatumbuliwa, haiwezekani kulea Mawaziri Wavivu Hiki kitakuwa Chama gani kisicho na Nguvu

Aidha Kinana amesema tabia ya Wabunge kupitisha kila Kitu kinacholetwa na Serikali ifike mwisho na Serikali ielezwe Wazi kwamba Watendaji wake ni Wavivu

Mzee Kinana amesema hayo kwa hasira sana kwenye mkutano wa hadhara ambapo Wananchi walimshangilia sana

Chanzo: Clip ya Kinana kwenye ukurasa wa twitter wa Ananilea Nkya

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Huyu siasa imeshamshinda ajikite tu kwenye ile biashara yake ya ujangiri naona tembo wamekuwa wengi hadi wanakuwa tishio kwa binadamu atusaidie katika eneo hilo.
 
Ule usemi wa "nyani haoni kundule" umedhihirika pale Katibu Mkuu wa CCM, Abdallahaman Kinana alipowachana wanachama wa CCM katika mkutano alioufanya hapo jana mjini Kigoma kwa kuwaambia wanachama wa chama hicho waache kupendeleana wala kubebana kwani kwa kufanya hivyo tutazalisha makundi mengi ndani ya chama hicho, kitu ambacho sio afya kwa chama na pia kwa kufanya hivyo kunaweza kuchangia kuchukiwa kwa chama na kupelekea upinzani kupata nguvu!

Kinana anasahau kuwa ndani ya chama hicho (hasa ngazi ya juu) wamekuwa wakibebana na kupendeleana hasa pale ambapo kumekuwa kukifanyika madudu ya kukichafua na kukipaka matope chama. Rejea orodha ya mafisadi iliyotajwa na CCM, Rejea orodha ya mawaziri mizigo iliyotajwa na Kinana mwenyewe, n.k. Ni hatua gani madhubuti zilizochukuliwa na chama kwa watu hao? Huko sio kubebana? Huko sio kupendeleana?

Kauli hii ya Kinana ya "Tusipendeleane, Tusibebane" inaonesha kana kwamba CCM inatufanyia usanii.
Hii mbinu imepitwa na wakati,nafikiri chama changu pendwa cha CCM tumeshindwa kuongoza nchi kwa weledi,sababu ni kuleana,

Kuna watoto wanaojiita baba zao wallipigania hii nchi ndio tatizo kubwa sana,hawana uwezo kuendesha majukumu makubwa wanayokabidhiwa na ni wezi pia
 
Mstaafu anaporudishwa kazini, ni muda Kwa vijana kujitafakari.
 
...
Kauli hii ya Kinana ya "Tusipendeleane, Tusibebane" inaonesha kana kwamba CCM inatufanyia usanii.

Hii yote ni siasa tu.

It's all about Politics and Power. Politicians use People to get in Power and use Power to make People keep them in Power.

Hicho ndicho anachofanya Kinana
 
Back
Top Bottom