Tetesi: Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara

Tetesi: Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara

Status
Not open for further replies.
Kama hali iko hivyo basi futeni kesi ya Gwajima,maana alichosema hakina tofauti sana na hiki.Vinginevyo ccm kinabaki kuwa chama chenye wanafiki wengi.
Gwajima alikuwa anamshambulia rais mstaafu, siyo Luhwavi
 
Wakati wa kampeni alisisitiza "chagua mimi na serikali ya mimi itakuwa so and so" sasa chama alichokiweka pembeni leo anakitaka kwa hamu awe mkulu mpaka wanatumika wakina Bulembo na Lizaboni kushinikiza lazima awe yeye mwenye kigoda.
Bahati mbaya wale aliokuwa anawadharau Leo ndio wameshika mpini na asipoangalia JK akisema tuu kura ni za siri basi amejitahidi sana ni 37% na hiyo ndio aibu.
NKM msidhani ni yeye mwenyewe, katumwa na vigogo ajifunge bomu na moto tutauona.
Kweli "waacheni wafu wazikane" ilikuwa kauli iliyofanyiwa utafiti
 
Wakati wa kampeni alisisitiza "chagua mimi na serikali ya mimi itakuwa so and so" sasa chama alichokiweka pembeni leo anakitaka kwa hamu awe mkulu mpaka wanatumika wakina Bulembo na Lizaboni kushinikiza lazima awe yeye mwenye kigoda.
Bahati mbaya wale aliokuwa anawadharau Leo ndio wameshika mpini na asipoangalia JK akisema tuu kura ni za siri basi amejitahidi sana ni 37% na hiyo ndio aibu.
NKM msidhani ni yeye mwenyewe, katumwa na vigogo ajifunge bomu na moto tutauona.
Kweli "waacheni wafu wazikane" ilikuwa kauli iliyofanyiwa utafiti
Inashangaza sana mnaolia ni UKAWA, ni mwenyekiti wa CCM siyo UKAWA. Tulizeni mizuka.
 
View attachment 365938
N.K/Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi

Wadau amani iwe kwenu,

Hivi karibuni, tumeshuhudia harakati kadhaa za baadhi ya wanasiasa wa ndani na nje ya CCM wakipaza sauti zao kutaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa Chama hicho ili kumrithi Dr Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kustaafu rasmi wadhifa huo Julai 23.

Awali kulikuwa na figisu figisu nyingi kuwa chama hakina fedha za kuendeshea Mkutano Mkuu ili tu lengo lao litimie. Thanks kwa jitihada zilizofanywa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula ambao wamehakikisha kuwa fedha zinapatikana na mkutano Mkuu unafanyika Julai 23.

Hata hivyo, tunapoelekea Julai 23, yapo Mambo kadhaa yanaendelea ndani ya CCM ambayo kwa hakika yanaweza kuvuruga utamaduni ambao imejiwekea wa kukabidhiana madaraka ya Uenyekiti pindi Rais anapomaliza muda wake. This time, zipo harakati za chini kwa chini zinazoendeshwa ili Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti na Magufuli abaki kwenye cheo cha Urais tu.

Binafsi baada ya kuona kuwa vuguvugu hilo linazidi, ikabidi niingie chimbo ili kumnasa anayeinjinia mkakati huo. Hakika nilichokibaini kinanishtua sana. Mchawi sasa kajulikana. Ni Rajab Luhwavi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ambaye ametwaa madaraka hayo tarehe 9 Julai 2015 mara Baada ya Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi hiyo wakati wa mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Mtakumbuka kuwa Luhwavi alikuwa Msaidizi wa Rais kwenye Masuala ya Siasa kabla ya nafasi hiyo kumuachia Martin Shigela Julai 2015.

Hoja za Luhwavi kutaka Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni za kitoto sana. kwamba, Magufuli hakijui chama na hivyo yeye pamoja na genge lake wanaamini kuwa atakiharibu badala ya kukiimarisha. Hofu yao imeongezeka hasa kutokana na (kwa mtazamo wao) teuzi alizofanya Rais mpaka sasa kutozingatia kigezo cha Ukada wa CCM.

Hofu nyingine ya Luhwavi ni kupoteza madaraka ndani ya CCM. Luhwavi anaamini kuwa ikiwa Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa CCM, hatakuwa na wadhifa wowote ndani ya chama na kwamba hata hiyo nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu ataipoteza.

Pia Luhwavi ana hofu kubwa ya kufikishwa Mahakamani kutokana na kufuja fedha nyingi zilizotengwa wakati wa kampeni. Inaelezwa kuwa Luhwavi alikihujumu chama kwa kupeleka fedha kidogo kwenye majimbo ya uchaguzi tofauti na ilivyoidhinishwa na chama. Inadaiwa kuwa kwa baadhi ya mikoa, fedha hizo hazikwenda kabisa na hivyo kufanya baadhi ya wagombea kujigharamia hali iliyochangia kushindwa kwao.

Nani anampendekeza Luhwavi awe Mwenyekiti wa CCM? Hili lipo dhahiri. Luhwavi anataka Jakaya Kikwete aendelee kwenye wadhifa huo. Matarajio ya Luhwavi ni kwamba, ikiwa Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, atamteua yeye (Luhwavi) kuwa Katibu Mkuu kujaza nafasi ya Katibu Mkuu wa sasa Abdulrahman Kinana ambaye ametangaza kuachia nafasi hiyo baada ya Mkutano Mkuu wa Julai 23.

Mpaka sasa, Luhwavi amezunguka kwenye mikoa kadhaa ya Tanzania Bara kuhamasisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wasiridhie hoja ya Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM. Inasemekana kuwa mpunga wa kutosha umetembea kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ili wamkwamishe Rais Magufuli.

Hata hivyo, inaonekana dhahiri sasa kuwa mkakati wa Luhwavi na Timu yake umegonga mwamba. Mwenyekiti wa sasa Jakaya Kikwete amesema hataongeza hata sekunde moja na kwamba dhamira yake ya kwenda kulala usingizi baada ya Magufuli kushinda Urais iko pale pale. Hana mashaka hata kidogo na Rais na anawabeza wale wanaodhani kuwa Magufuli hana uzoefu wa kutosha kuongoza chama. Kwamba, kama amechaguliwa kuwa Rais wa nchi, atashindwaje kuongoza chama?

Nani walio nyuma ya harakati hizo? Nitaendelea kuwajuza kwa kadri tunavyokaribia Julai 23. Stay with me. Niwapongeze tu na kuwatia moyo baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Dar es Salaam, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma ambao wamenipa ushirikiano wa kutosha wakati ninafuatilia jambo hili mpaka mchawi amejulikana. Mikoa hii ni miongoni mwa mikoa ambayo Luhwavi alitembelea kufanikisha mkakati wake.
Nilipoona N*pe anabwaga manyanga mapema nilijua ujio wa Magufuli hapo Lumumba ni tishio na nilitegemea sarakasi kama hizi.BTW chama chetu kina utamaduni na kwa desturi hizo uenyekiti kwa Magufuli ni jambo la LAZIMA si kuviziana na kubembelezana.
 
Huyu jamaa anatakuwa na maslai ya kifasadi au atakuwa na genge la wahuni anawalinda! Achunguzwe na ikibainika awe wa kwanza kuswekwa ndani ya magereza ya mafisadi inayotarajiwa kujengwa ktk ya ziwa victoria!
 
Inashangaza sana mnaolia ni UKAWA, ni mwenyekiti wa CCM siyo UKAWA. Tulizeni mizuka.
Mbona sie ndio waumini wa Mzee wa mizuka ndio akamate manyanga ili hicho kikundi aka chama akipelekeshe kama makuruta wa Ruvu JKT mpaka wasambaratike!
Hakuna chama chochote cha SIASA duniani kiliwahi kupelekwa kijeshi kikabaki kuwa chama tena. Chama ni hiari na maridhiano ndani ya vikao. Tumbuatumbua ni serikali tuu
 
Mkuu kwani hofu yenu JPM akiwa mwenyekiti wa CCM, CHAGADEMA mtasambaratika? Chagadema mtaendelea kuwepo ila kama misukule, Mtei na Mkwe wake wataendelea kuiongoza SACCOSS
kwani Luwhavi ni CHADEMA?....sisi hatuna shida na hilo lichama lenu ambalo ni li scraper sasaivi...wafu mzikane tu
 
Kama unayo zungumza ni ya kweli yanaendana na yale aliyo Sema bishop gwajima, kwa nini gwajima anashutumiwa kw uchochezi?
kw nini na wewe usiwajibike kw hili?
 
hahahahaaa kuna vitu huwa nacheka sana nikisikia maana najifunza kitu kama watu wanafuja fedha za sirikali hadi wanakuja kufuja na chama basi muda si mrefu tutasikia mtu analaumiwa kufuja hadi za familia yake mweeeh

me dont.......
 
Tar 23 July lazima watu watoane meno ya sebuleni Dodoma
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom