Tetesi: Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara

Status
Not open for further replies.
Wewe huyo huyo uliwahi kupinga kwamba hakuna kitu kama hicho, sasa unatuletea hii taarifa ili tufanye nini?
Huyo ndiyo Lizaboni. One who can never be trusted. Baada ya kukosa kila mahali sasa anatafuta kiki kwenye chama chao. Amazing.
 
Huyu jamaa anatakuwa na maslai ya kifasadi au atakuwa na genge la wahuni anawalinda! Achunguzwe na ikibainika awe wa kwanza kuswekwa ndani ya magereza ya mafisadi inayotarajiwa kujengwa ktk ya ziwa victoria!
Anatofauti na Magufuli si ndio fasheni ya CCM
 
kiujumla kumuachia jpm uenyekiti wa ccm ni kwa wanaccm imani kukosa ujasiri wa kutetea chama chao. lakini wangelikuwa majasiri wasingelikubali kamwe...
 
View attachment 365938
N.K/Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi
Wadau amani iwe kwenu,

Hivi karibuni, tumeshuhudia harakati kadhaa za baadhi ya wanasiasa wa ndani na nje ya CCM wakipaza sauti zao kutaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa Chama hicho ili kumrithi Dr Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kustaafu rasmi wadhifa huo Julai 23.

Awali kulikuwa na figisu figisu nyingi kuwa chama hakina fedha za kuendeshea Mkutano Mkuu ili tu lengo lao litimie. Thanks kwa jitihada zilizofanywa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula ambao wamehakikisha kuwa fedha zinapatikana na mkutano Mkuu unafanyika Julai 23.

Hata hivyo, tunapoelekea Julai 23, yapo Mambo kadhaa yanaendelea ndani ya CCM ambayo kwa hakika yanaweza kuvuruga utamaduni ambao imejiwekea wa kukabidhiana madaraka ya Uenyekiti pindi Rais anapomaliza muda wake. This time, zipo harakati za chini kwa chini zinazoendeshwa ili Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti na Magufuli abaki kwenye cheo cha Urais tu.

Binafsi baada ya kuona kuwa vuguvugu hilo linazidi, ikabidi niingie chimbo ili kumnasa anayeinjinia mkakati huo. Hakika nilichokibaini kinanishtua sana. Mchawi sasa kajulikana. Ni Rajab Luhwavi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ambaye ametwaa madaraka hayo tarehe 9 Julai 2015 mara Baada ya Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi hiyo wakati wa mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Mtakumbuka kuwa Luhwavi alikuwa Msaidizi wa Rais kwenye Masuala ya Siasa kabla ya nafasi hiyo kumuachia Martin Shigela Julai 2015.

Hoja za Luhwavi kutaka Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni za kitoto sana. kwamba, Magufuli hakijui chama na hivyo yeye pamoja na genge lake wanaamini kuwa atakiharibu badala ya kukiimarisha. Hofu yao imeongezeka hasa kutokana na (kwa mtazamo wao) teuzi alizofanya Rais mpaka sasa kutozingatia kigezo cha Ukada wa CCM.

Hofu nyingine ya Luhwavi ni kupoteza madaraka ndani ya CCM. Luhwavi anaamini kuwa ikiwa Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa CCM, hatakuwa na wadhifa wowote ndani ya chama na kwamba hata hiyo nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu ataipoteza.

Pia Luhwavi ana hofu kubwa ya kufikishwa Mahakamani kutokana na kufuja fedha nyingi zilizotengwa wakati wa kampeni. Inaelezwa kuwa Luhwavi alikihujumu chama kwa kupeleka fedha kidogo kwenye majimbo ya uchaguzi tofauti na ilivyoidhinishwa na chama. Inadaiwa kuwa kwa baadhi ya mikoa, fedha hizo hazikwenda kabisa na hivyo kufanya baadhi ya wagombea kujigharamia hali iliyochangia kushindwa kwao.

Nani anampendekeza Luhwavi awe Mwenyekiti wa CCM? Hili lipo dhahiri. Luhwavi anataka Jakaya Kikwete aendelee kwenye wadhifa huo. Matarajio ya Luhwavi ni kwamba, ikiwa Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, atamteua yeye (Luhwavi) kuwa Katibu Mkuu kujaza nafasi ya Katibu Mkuu wa sasa Abdulrahman Kinana ambaye ametangaza kuachia nafasi hiyo baada ya Mkutano Mkuu wa Julai 23.

Mpaka sasa, Luhwavi amezunguka kwenye mikoa kadhaa ya Tanzania Bara kuhamasisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wasiridhie hoja ya Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM. Inasemekana kuwa mpunga wa kutosha umetembea kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ili wamkwamishe Rais Magufuli.

Hata hivyo, inaonekana dhahiri sasa kuwa mkakati wa Luhwavi na Timu yake umegonga mwamba. Mwenyekiti wa sasa Jakaya Kikwete amesema hataongeza hata sekunde moja na kwamba dhamira yake ya kwenda kulala usingizi baada ya Magufuli kushinda Urais iko pale pale. Hana mashaka hata kidogo na Rais na anawabeza wale wanaodhani kuwa Magufuli hana uzoefu wa kutosha kuongoza chama. Kwamba, kama amechaguliwa kuwa Rais wa nchi, atashindwaje kuongoza chama?

Nani walio nyuma ya harakati hizo? Nitaendelea kuwajuza kwa kadri tunavyokaribia Julai 23. Stay with me. Niwapongeze tu na kuwatia moyo baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Dar es Salaam, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma ambao wamenipa ushirikiano wa kutosha wakati ninafuatilia jambo hili mpaka mchawi amejulikana. Mikoa hii ni miongoni mwa mikoa ambayo Luhwavi alitembelea kufanikisha mkakati wake.
Wafu wanazikana. Sisi wengine inatuhusu nini?
 
Tarehe 23 July 2016 watu watatoana macho kwa kugombea vyeo haaa haaa.
 
Lizaboni,nilitaka kujua aliyerithi mikoba ya ukwasi wa Lowassa na kuanza kugawa fedha. Anatoa wapi hizo fedha za kuwagawia wajumbe.
 
Maneno yako ndio alitabiri Gwajima! Leo umeongea mCCM kumbe yalikuwa na ukweli baadhi ya Maneno ya Gwajima!
 
Wewe unasemaje? Kwamba Naibu Katibu mkuu wa chama Taifa hatoboi kwa mwanachama wa kawaida ambaye hana nafasi hata ya mwenyekiti wa kitongoji? Hapa ushindani si ni ndani ya chama?
Au unatudhibitishia kuwa kwenu serikali mnayoiunda mdiyo ina nguvu kuliko chama katika mambo ya chama? Hii statement yako ni ya aibu sana kama mwanachama. Au ndio sababu hata kwenye kikao cha Kamati kuu kule Dodoma Magu akamtuma Naibu spika kuhudhuria eti anamwakilisha Spika wakati utaratibu huo haupo na kina Kinana wakabaki kununa tuu?

Mbona kiila uchanguzi wa mwenyekiti wa CHADEMA unapofika wagombea wengine huzuiwa ili Mbowe pekee agombee bila kupingwa?
 
Hahahahahaaaaaaa! Ni kazi ya mikono yangu hiyo Mkuu. Hutapata mahala pengine nje ya hapa JF. Lizaboni ni wa level nyingine Mkuu
Hivi sheria ya mtandao haifanyi kazi hapa ................!!

Hii kitu ingetolewa na Yericko, nafikiri tungesikia mengine ................!! Uchochezi, uongo n.k.
 
Ukiyafuatilia sana yanayoendelea ndani ya CCM utachoka mwenyewe. Kila mmoja amejitia msemaji na mchunguzi ndani ya chama. Leo unaongea hiki kesho unaongea kile ili mradi uonekane unaijua ccm nje ndani. Huo ni wakati wakukipigania chama kuanika kinachoendelea ndani yaCCM nikuwataka wengine waitumie hiyo kama silaha kuendelea kutengeneza makundi. Jifunze kile ulichokisoma pale Kivukoni Lizaboni
 
Hilo la Kumtukana Pengo si kweli sababu Baba asko Pengo alishatutangazia sisi waumini wake kuwa amemsamehe Gwajima tena akanukuu maneno ya Bwana wetu Yesu Kristu kuwa "ee Baba Wasamehe Kwani hajui watendalo". Baba Askofu Pengo alitwambia amemsamehe Gwajima kwani hajui alitendalo. Mimi nazidi Kusisitiza Mwambie Sirro asimsumbue Baba Askofu Gwajima kwa kusema Ukweli kuwa kuna watu wanatembea nchi nzima kuwashawishi wana ccm wasimpe Magufuli uenyekiti.
Gwajima ni zaidi ya Intelejensia
 
Hahahaha nasikia kesho kutwa anataka kuitisha mkutano wa waandishi wa habari kujikosha eti maandalizi ya mkutano yamekamilika na wapo tayari kumpokea mwenyekiti mpya! Nimecheka sana ...!Hivi unajua hili bandiko limewaharibia watu sasa wengi wataanza kujikosha! Mi naomba wamfate Lowasa kabisa!
Mnajitia moyo wakati mnajua ukweli kuwa sasa ccm ni vipande vipande tu
 
Mimi naendelea kusubiri update mkuu @Lizabon, habari zako Mara huwa zina chembechembe za ukweli ndani yake.!
 
View attachment 365938
N.K/Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi
Wadau amani iwe kwenu,

Hivi karibuni, tumeshuhudia harakati kadhaa za baadhi ya wanasiasa wa ndani na nje ya CCM wakipaza sauti zao kutaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa Chama hicho ili kumrithi Dr Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kustaafu rasmi wadhifa huo Julai 23.

Awali kulikuwa na figisu figisu nyingi kuwa chama hakina fedha za kuendeshea Mkutano Mkuu ili tu lengo lao litimie. Thanks kwa jitihada zilizofanywa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula ambao wamehakikisha kuwa fedha zinapatikana na mkutano Mkuu unafanyika Julai 23.

Hata hivyo, tunapoelekea Julai 23, yapo Mambo kadhaa yanaendelea ndani ya CCM ambayo kwa hakika yanaweza kuvuruga utamaduni ambao imejiwekea wa kukabidhiana madaraka ya Uenyekiti pindi Rais anapomaliza muda wake. This time, zipo harakati za chini kwa chini zinazoendeshwa ili Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti na Magufuli abaki kwenye cheo cha Urais tu.

Binafsi baada ya kuona kuwa vuguvugu hilo linazidi, ikabidi niingie chimbo ili kumnasa anayeinjinia mkakati huo. Hakika nilichokibaini kinanishtua sana. Mchawi sasa kajulikana. Ni Rajab Luhwavi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ambaye ametwaa madaraka hayo tarehe 9 Julai 2015 mara Baada ya Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi hiyo wakati wa mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Mtakumbuka kuwa Luhwavi alikuwa Msaidizi wa Rais kwenye Masuala ya Siasa kabla ya nafasi hiyo kumuachia Martin Shigela Julai 2015.

Hoja za Luhwavi kutaka Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni za kitoto sana. kwamba, Magufuli hakijui chama na hivyo yeye pamoja na genge lake wanaamini kuwa atakiharibu badala ya kukiimarisha. Hofu yao imeongezeka hasa kutokana na (kwa mtazamo wao) teuzi alizofanya Rais mpaka sasa kutozingatia kigezo cha Ukada wa CCM.

Hofu nyingine ya Luhwavi ni kupoteza madaraka ndani ya CCM. Luhwavi anaamini kuwa ikiwa Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa CCM, hatakuwa na wadhifa wowote ndani ya chama na kwamba hata hiyo nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu ataipoteza.

Pia Luhwavi ana hofu kubwa ya kufikishwa Mahakamani kutokana na kufuja fedha nyingi zilizotengwa wakati wa kampeni. Inaelezwa kuwa Luhwavi alikihujumu chama kwa kupeleka fedha kidogo kwenye majimbo ya uchaguzi tofauti na ilivyoidhinishwa na chama. Inadaiwa kuwa kwa baadhi ya mikoa, fedha hizo hazikwenda kabisa na hivyo kufanya baadhi ya wagombea kujigharamia hali iliyochangia kushindwa kwao.

Nani anampendekeza Luhwavi awe Mwenyekiti wa CCM? Hili lipo dhahiri. Luhwavi anataka Jakaya Kikwete aendelee kwenye wadhifa huo. Matarajio ya Luhwavi ni kwamba, ikiwa Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, atamteua yeye (Luhwavi) kuwa Katibu Mkuu kujaza nafasi ya Katibu Mkuu wa sasa Abdulrahman Kinana ambaye ametangaza kuachia nafasi hiyo baada ya Mkutano Mkuu wa Julai 23.

Mpaka sasa, Luhwavi amezunguka kwenye mikoa kadhaa ya Tanzania Bara kuhamasisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wasiridhie hoja ya Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM. Inasemekana kuwa mpunga wa kutosha umetembea kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ili wamkwamishe Rais Magufuli.

Hata hivyo, inaonekana dhahiri sasa kuwa mkakati wa Luhwavi na Timu yake umegonga mwamba. Mwenyekiti wa sasa Jakaya Kikwete amesema hataongeza hata sekunde moja na kwamba dhamira yake ya kwenda kulala usingizi baada ya Magufuli kushinda Urais iko pale pale. Hana mashaka hata kidogo na Rais na anawabeza wale wanaodhani kuwa Magufuli hana uzoefu wa kutosha kuongoza chama. Kwamba, kama amechaguliwa kuwa Rais wa nchi, atashindwaje kuongoza chama?

Nani walio nyuma ya harakati hizo? Nitaendelea kuwajuza kwa kadri tunavyokaribia Julai 23. Stay with me. Niwapongeze tu na kuwatia moyo baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Dar es Salaam, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma ambao wamenipa ushirikiano wa kutosha wakati ninafuatilia jambo hili mpaka mchawi amejulikana. Mikoa hii ni miongoni mwa mikoa ambayo Luhwavi alitembelea kufanikisha mkakati wake.

dhidi ya UKAWA mnalo jeshi la polisi linawasaidia.

sasa hapa wenyewe kwa wenyewe..msaada utatoka wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom