Tetesi: Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara

Tetesi: Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara

Status
Not open for further replies.
Mwaka huu lazima mlogane kudadeki ! Imeamriwa kura ni siri , na uhakika ni kwamba 80% ni kura za hapana , 10% ndiyo na 10% za maruhani !
Wanajidanganya hao,hivi unafikiri kuna panya anaweza kumzuia JPM,hvyo vikao vyao hata wakafanye chooni watajulikana tu,kama mamvi alishughulikiwa hyo lukaku sijui ni Mdgo sana,muacheni JPM arekebishe chama.
 
JK huwa anawajua sana wajinga wajinga kama Luhwavi. Kinachokwenda kumkita Luhwavi hakina tofauti na kilichomkuta Lowassa. JK anatumia taaluma aliyoipata jeshini kuwaangamiza maadui wa CCM.
Mnamnyanyasa Luhwavi kisa ni mzanzibar
 
Mkuu Lizaboni unataka kuaminisha umma wa JF kuwa wewe ni mwandishi ambaye ni Neutral Ground? kwamba hata za ndani kwako unawapakulia umma wa JF? Au kuna kitu unanyemelea kwa mkuu wa kaya.
 
Hahahahahaaaaa! Mkuu, nimekupata. Ndio maana nimemalizia kwa kuwashukuru wajumbe wote wa Mkutano Mkuu kwenye mikoa niliyoorodhesha ambao wamenipa support ya kutosha. Sikuweza kutaja mmoja mmoja kwa vile nitajaza server maana ni wengi
Na si busara kutaja chanzo cha kupatia taarifa
 
hakuna mtu mshenzi kama huyo Rajab Luhavi.
hajielewi kabisa.
kwenye mchakato wa uchaguzi majimboni kuna rafu zilikua zinachezwa tunampigia sm kumjuza anasema haimuhusu. yaani ni mpuuzi wa kiwango cha phd. ngoja Ngosha aje kumnyoosha.

ivi ni mswahi wa wapi vile?
 
Wanajidanganya hao,hivi unafikiri kuna panya anaweza kumzuia JPM,hvyo vikao vyao hata wakafanye chooni watajulikana tu,kama mamvi alishughulikiwa hyo lukaku sijui ni Mdgo sana,muacheni JPM arekebishe chama.
Na Magu atawanyoosha sana. Kikwete aliambiwa awashughulikie waliokisaliti chama. Mpaka sasa kimyaaaa. Subiri Magu akae kwenye kiti
 
Ewee mwenyezimungu kiharakishe kife cha CCM,kwani ameshaugua muda mrefu bila kupata nafuu ewe mwenyezimungu ipokee dua yangu "AMEN"
Maombi ya kutaka CCM ife yalifanywa na:
1. Kakobe
2. Mwingira
3. Gwajima
4. Mtikila

wewe cheo chako kwenye dini ni kipi? Maana hao maombi yao hayajasikilizwa
 
chama kipya hicho kimezaliwa?nawaona mmeshaanza kugawanyika ndo mwisho wenu umeshakaribia
Chama kimezaliwa upya. Wasaliti wanapaswa kwenda kutafuta maficho yao CHADEMA
 
Duh! Mkuu! Mbona umeenda mbali sana?

Nisipokutania Wewe Mwana CCM mwenzangu tuliyepambana humu na " Nyumbu " wakati wa KAMPENI mwaka jana hadi Mpendwa wetu Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akashinda Urais nitamtania nani Mkuu? Hata siku moja sitoweza " kukuvunjia " heshima humu na nakuomba tu kuwa na AMANI kabisa na Mimi kwani NAKUKUBALI pengine kuliko unavyodhani au unavyonihisi. Hivi ninaanzaje " kumchukia " au kumpiga " dongo " mwana CCM mwenzangu tena ALIYETUKUKA kama Wewe? Tupo " pamoko " Mkuu ondoa shaka.
 
hakuna mtu mshenzi kama huyo Rajab Luhavi.
hajielewi kabisa.
kwenye mchakato wa uchaguzi majimboni kuna rafu zilikua zinachezwa tunampigia sm kumjuza anasema haimuhusu. yaani ni mpuuzi wa kiwango cha phd. ngoja Ngosha aje kumnyoosha.

ivi ni mswahi wa wapi vile?
Ningekuwa mimi ndo Luhwavi, hakika ningejiuzulu kabla ya Julai 23
 
Nisipokutania Wewe Mwana CCM mwenzangu tuliyepambana humu na " Nyumbu " wakati wa KAMPENI mwaka jana hadi Mpendwa wetu Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akashinda Urais nitamtania nani Mkuu? Hata siku moja sitoweza " kukuvunjia " heshima humu na nakuomba tu kuwa na AMANI kabisa na Mimi kwani NAKUKUBALI pengine kuliko unavyodhani au unavyonihisi. Hivi ninaanzaje " kumchukia " au kumpiga " dongo " mwana CCM mwenzangu tena ALIYETUKUKA kama Wewe? Tupo " pamoko " Mkuu ondoa shaka.
Hahahahahaaaaa! Ni ekupata Mkuu. Unanikumbusha enzi zile kwenye story za akina Jimmy Apson Mwang'onda. Ulinieleza mambo mengi sana mkiwa mnasoma pale Shule ya Msingi Mbuyuni. Hakika wewe ni wa next level
 
Nilijua tu watetezi wa Luhwavi mtaingia kichwa kichwa. Mmeshagundulika na mkakati wenu hautafanikiwa
Endelea kubinuwa makalio tunakwambia Magufuli sio Mwenyekiti material akae na uraisi chama hapaswi kuwa kwa sababu hakuna siasa mpaka 2020 wewe lilia mkate wako ndio akili yako uliyonayo kujikomba kubeba wanaume kuwafuta viatu huna lingine yaani kibanadamu wewe ni maiti
 
Wadau amani iwe kwenu.

Hivi karibuni, tumeshuhudia harakati kadhaa za baadhi ya wanasiasa wa ndani na nje ya CCM wakipaza sauti zao kutaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa Chama hicho ili kumrithi Dr Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kustaafu rasmi wadhifa huo Julai 23.

Awali kulikuwa na figisu figisu nyingi kuwa chama hakina fedha za kuendeshea Mkutano Mkuu ili tu lengo lao litimie. Thanks kwa jitihada zilizofanywa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula ambao wamehakikisha kuwa fedha zinapatikana na mkutano Mkuu unafanyika Julai 23.

Hata hivyo, tunapoelekea Julai 23, yapo Mambo kadhaa yanaendelea ndani ya CCM ambayo kwa hakika yanaweza kuvuruga utamaduni ambao imejiwekea wa kukabidhiana madaraka ya Uenyekiti pindi Rais anapomaliza muda wake. This time, zipo harakati za chini kwa chini zinazoendeshwa ili Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti na Magufuli abaki kwenye cheo cha Urais tu.

Binafsi baada ya kuona kuwa vuguvugu hilo linazidi, ikabidi niingie chimbo ili kumnasa anayeinjinia mkakati huo. Hakika nilichokibaini kinanishtua sana. Mchawi sasa kajulikana. Ni Rajab Luhwavi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ambaye ametwaa madaraka hayo tarehe 9 Julai 2015 mara Baada ya Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi hiyo wakati wa mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Mtakumbuka kuwa Luhwavi alikuwa Msaidizi wa Rais kwenye Masuala ya Siasa kabla ya nafasi hiyo kumuachia Martin Shigela Julai 2015.

Hoja za Luhwavi kutaka Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni za kitoto sana. kwamba, Magufuli hakijui chama na hivyo yeye pamoja na genge lake wanaamini kuwa atakiharibu badala ya kukiimarisha. Hofu yao imeongezeka hasa kutokana na (kwa mtazamo wao) teuzi alizofanya Rais mpaka sasa kutozingatia kigezo cha Ukada wa CCM.

Hofu nyingine ya Luhwavi ni kupoteza madaraka ndani ya CCM. Luhwavi anaamini kuwa ikiwa Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa CCM, hatakuwa na wadhifa wowote ndani ya chama na kwamba hata hiyo nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu ataipoteza.

Pia Luhwavi ana hofu kubwa ya kufikishwa Mahakamani kutokana na kufuja fedha nyingi zilizotengwa wakati wa kampeni. Inaelezwa kuwa Luhwavi alikihujumu chama kwa kupeleka fedha kidogo kwenye majimbo ya uchaguzi tofauti na ilivyoidhinishwa na chama. Inadaiwa kuwa kwa baadhi ya mikoa, fedha hizo hazikwenda kabisa na hivyo kufanya baadhi ya wagombea kujigharamia hali iliyochangia kushindwa kwao.

Nani anampendekeza Luhwavi awe Mwenyekiti wa CCM? Hili lipo dhahiri. Luhwavi anataka Jakaya Kikwete aendelee kwenye wadhifa huo. Matarajio ya Luhwavi ni kwamba, ikiwa Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, atamteua yeye (Luhwavi) kuwa Katibu Mkuu kujaza nafasi ya Katibu Mkuu wa sasa Abdulrahman Kinana ambaye ametangaza kuachia nafasi hiyo baada ya Mkutano Mkuu wa Julai 23.

Mpaka sasa, Luhwavi amezunguka kwenye mikoa kadhaa ya Tanzania Bara kuhamasisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wasiridhie hoja ya Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM. Inasemekana kuwa mpunga wa kutosha umetembea kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ili wamkwamishe Rais Magufuli.

Hata hivyo, inaonekana dhahiri sasa kuwa mkakati wa Luhwavi na Timu yake umegonga mwamba. Mwenyekiti wa sasa Jakaya Kikwete amesema hataongeza hata sekunde moja na kwamba dhamira yake ya kwenda kulala usingizi baada ya Magufuli kushinda Urais iko pale pale. Hana mashaka hata kidogo na Rais na anawabeza wale wanaodhani kuwa Magufuli hana uzoefu wa kutosha kuongoza chama. Kwamba, kama amechaguliwa kuwa Rais wa nchi, atashindwaje kuongoza chama?

Nani walio nyuma ya harakati hizo? Nitaendelea kuwajuza kwa kadri tunavyokaribia Julai 23. Stay with me. Niwapongeze tu na kuwatia moyo baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Dar es Salaam, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma ambao wamenipa ushirikiano wa kutosha wakati ninafuatilia jambo hili mpaka mchawi amejulikana. Mikoa hii ni miongoni mwa mikoa ambayo Luhwavi alitembelea kufanikisha mkakati wake.

Ndugu yangu Lizaboni mbona hii kitu ulikataa kata kata hakuna leo unamtwisha zigo Rajabu kwakuwa si team Majipu.
 
Utakufa wewe utaacha CCM
Lizaboni jambo usilolojua ni kwamba CCM ni kama nyati aliepigwa risasi kadhaa (ndio haya matukio yote)na UKAWA.Kilichopo sasa hivi ni mwindaji UKAWA anafuatilia matone ya damu ajichinjie mzoga wake.Ni suala zima la timing tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom