Tetesi: Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara

Status
Not open for further replies.
Tangu nimejiunga humu sijawahi kuona kaka Mkubwa lizaboni akisema uongo... Hebu tusubirie
 
Lini fomu za uchaguzi wa Mwenyekiti zitatolewa CCM ? Kabla ya kumhukumu Luhwavi
 
CCM bana, yaani hakuna anaemuamini mwenzake aisee! Na kama msipokua makina mtaingia kusiko muda sio mrefu. Kuna watu walitafuna zile shule za jumuiya ya wazazi, wakikumbuka tar 23 ni tumbo la kuhara ghafla.
Btw, wezi wote na wahujum uchumi wapo ccm na ndo ndo JPM aliowasema kua "nchi imefika ilipo kwa sababu ya majizi"

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Acheni uzoefu uchukue nafasi ukipewa urais na uwenyekiti wa chama unapewa mbona ni kawaida tuu au ni huo mwendo kasi unawatisha wala msiwe na wasiwasi mtauweza tuu.
 
Lizabon kwani huyo Mzee kakukosea nini? au kakosana na boss zako maana haya mawe uliyomtumia yamejaa chuki kubwa
 
Kwa staili ile ile...kukiwa na issue nyumbani anakula kona...katafuna kona nyingine nimesikia...yuko kusini.
 
View attachment 365938
N.K/Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi
Wadau amani iwe kwenu,

Hivi karibuni, tumeshuhudia harakati kadhaa za baadhi ya wanasiasa wa ndani na nje ya CCM wakipaza sauti zao kutaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa Chama hicho ili kumrithi Dr Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kustaafu rasmi wadhifa huo Julai 23.

Awali kulikuwa na figisu figisu nyingi kuwa chama hakina fedha za kuendeshea Mkutano Mkuu ili tu lengo lao litimie. Thanks kwa jitihada zilizofanywa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula ambao wamehakikisha kuwa fedha zinapatikana na mkutano Mkuu unafanyika Julai 23.

Hata hivyo, tunapoelekea Julai 23, yapo Mambo kadhaa yanaendelea ndani ya CCM ambayo kwa hakika yanaweza kuvuruga utamaduni ambao imejiwekea wa kukabidhiana madaraka ya Uenyekiti pindi Rais anapomaliza muda wake. This time, zipo harakati za chini kwa chini zinazoendeshwa ili Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti na Magufuli abaki kwenye cheo cha Urais tu.

Binafsi baada ya kuona kuwa vuguvugu hilo linazidi, ikabidi niingie chimbo ili kumnasa anayeinjinia mkakati huo. Hakika nilichokibaini kinanishtua sana. Mchawi sasa kajulikana. Ni Rajab Luhwavi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ambaye ametwaa madaraka hayo tarehe 9 Julai 2015 mara Baada ya Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi hiyo wakati wa mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Mtakumbuka kuwa Luhwavi alikuwa Msaidizi wa Rais kwenye Masuala ya Siasa kabla ya nafasi hiyo kumuachia Martin Shigela Julai 2015.

Hoja za Luhwavi kutaka Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni za kitoto sana. kwamba, Magufuli hakijui chama na hivyo yeye pamoja na genge lake wanaamini kuwa atakiharibu badala ya kukiimarisha. Hofu yao imeongezeka hasa kutokana na (kwa mtazamo wao) teuzi alizofanya Rais mpaka sasa kutozingatia kigezo cha Ukada wa CCM.

Hofu nyingine ya Luhwavi ni kupoteza madaraka ndani ya CCM. Luhwavi anaamini kuwa ikiwa Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa CCM, hatakuwa na wadhifa wowote ndani ya chama na kwamba hata hiyo nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu ataipoteza.

Pia Luhwavi ana hofu kubwa ya kufikishwa Mahakamani kutokana na kufuja fedha nyingi zilizotengwa wakati wa kampeni. Inaelezwa kuwa Luhwavi alikihujumu chama kwa kupeleka fedha kidogo kwenye majimbo ya uchaguzi tofauti na ilivyoidhinishwa na chama. Inadaiwa kuwa kwa baadhi ya mikoa, fedha hizo hazikwenda kabisa na hivyo kufanya baadhi ya wagombea kujigharamia hali iliyochangia kushindwa kwao.

Nani anampendekeza Luhwavi awe Mwenyekiti wa CCM? Hili lipo dhahiri. Luhwavi anataka Jakaya Kikwete aendelee kwenye wadhifa huo. Matarajio ya Luhwavi ni kwamba, ikiwa Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, atamteua yeye (Luhwavi) kuwa Katibu Mkuu kujaza nafasi ya Katibu Mkuu wa sasa Abdulrahman Kinana ambaye ametangaza kuachia nafasi hiyo baada ya Mkutano Mkuu wa Julai 23.

Mpaka sasa, Luhwavi amezunguka kwenye mikoa kadhaa ya Tanzania Bara kuhamasisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wasiridhie hoja ya Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM. Inasemekana kuwa mpunga wa kutosha umetembea kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ili wamkwamishe Rais Magufuli.

Hata hivyo, inaonekana dhahiri sasa kuwa mkakati wa Luhwavi na Timu yake umegonga mwamba. Mwenyekiti wa sasa Jakaya Kikwete amesema hataongeza hata sekunde moja na kwamba dhamira yake ya kwenda kulala usingizi baada ya Magufuli kushinda Urais iko pale pale. Hana mashaka hata kidogo na Rais na anawabeza wale wanaodhani kuwa Magufuli hana uzoefu wa kutosha kuongoza chama. Kwamba, kama amechaguliwa kuwa Rais wa nchi, atashindwaje kuongoza chama?

Nani walio nyuma ya harakati hizo? Nitaendelea kuwajuza kwa kadri tunavyokaribia Julai 23. Stay with me. Niwapongeze tu na kuwatia moyo baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Dar es Salaam, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma ambao wamenipa ushirikiano wa kutosha wakati ninafuatilia jambo hili mpaka mchawi amejulikana. Mikoa hii ni miongoni mwa mikoa ambayo Luhwavi alitembelea kufanikisha mkakati wake.
Endeleeni kuparurana tu
 
Kumekucha.
Bundi wa Mwendo kasi azidi kutamalaki Lumumba kwa Madoido kabisa.
Hiyo siku ya kikao watatafunana wenyewe kwa wenyewe sie yetu macho halafu polisi watueleze kama intelejensia yao fake haikuiona hii dalili ya fujo au ipo kwa ajili ya wapinzani
 
Lizabon haaminiki haeleweki anasaka madaraka kwa gharama yoyote
Mi namshangaa kwa fitina na majungu anayoeneza humu. huyu anategemea kufaidika kwa figisufigusu la tarehe 23. Kwanza njo huku kwenye kampeni ya sirro tukuulize vizr
 
Ni kawaida kwa wana ccm kuchafuana kila kunapokaribia mkutano mkuu Vita ya sasa ni ukatibu mkuu Na siyo uenyekiti sasa wanatumia kila mbinu kuchafuana msishangae mpaka 23 watu kuita press Na kuanza kusemana bila uoga kuwa mwanachama Wa ccm lazima mishipa ya aibu ikutoke na huu ndio msimu Wa ela kwa wale vijana watukana watu
 
Kama kina lizabon. Amejipanga kupiga hela kwenye figisufigisu hili analoandaa
 
Mkuu 2020 ni mbali wanapambana watu wao wawe Na vyeo katika chama ili wapate Kula usishangae wakijifanya wehu kutukana watu na viongozi wao
 
View attachment 365938
N.K/Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi
Wadau amani iwe kwenu,

Hivi karibuni, tumeshuhudia harakati kadhaa za baadhi ya wanasiasa wa ndani na nje ya CCM wakipaza sauti zao kutaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa Chama hicho ili kumrithi Dr Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kustaafu rasmi wadhifa huo Julai 23.

Awali kulikuwa na figisu figisu nyingi kuwa chama hakina fedha za kuendeshea Mkutano Mkuu ili tu lengo lao litimie. Thanks kwa jitihada zilizofanywa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula ambao wamehakikisha kuwa fedha zinapatikana na mkutano Mkuu unafanyika Julai 23.

Hata hivyo, tunapoelekea Julai 23, yapo Mambo kadhaa yanaendelea ndani ya CCM ambayo kwa hakika yanaweza kuvuruga utamaduni ambao imejiwekea wa kukabidhiana madaraka ya Uenyekiti pindi Rais anapomaliza muda wake. This time, zipo harakati za chini kwa chini zinazoendeshwa ili Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti na Magufuli abaki kwenye cheo cha Urais tu.

Binafsi baada ya kuona kuwa vuguvugu hilo linazidi, ikabidi niingie chimbo ili kumnasa anayeinjinia mkakati huo. Hakika nilichokibaini kinanishtua sana. Mchawi sasa kajulikana. Ni Rajab Luhwavi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ambaye ametwaa madaraka hayo tarehe 9 Julai 2015 mara Baada ya Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi hiyo wakati wa mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Mtakumbuka kuwa Luhwavi alikuwa Msaidizi wa Rais kwenye Masuala ya Siasa kabla ya nafasi hiyo kumuachia Martin Shigela Julai 2015.

Hoja za Luhwavi kutaka Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni za kitoto sana. kwamba, Magufuli hakijui chama na hivyo yeye pamoja na genge lake wanaamini kuwa atakiharibu badala ya kukiimarisha. Hofu yao imeongezeka hasa kutokana na (kwa mtazamo wao) teuzi alizofanya Rais mpaka sasa kutozingatia kigezo cha Ukada wa CCM.

Hofu nyingine ya Luhwavi ni kupoteza madaraka ndani ya CCM. Luhwavi anaamini kuwa ikiwa Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa CCM, hatakuwa na wadhifa wowote ndani ya chama na kwamba hata hiyo nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu ataipoteza.

Pia Luhwavi ana hofu kubwa ya kufikishwa Mahakamani kutokana na kufuja fedha nyingi zilizotengwa wakati wa kampeni. Inaelezwa kuwa Luhwavi alikihujumu chama kwa kupeleka fedha kidogo kwenye majimbo ya uchaguzi tofauti na ilivyoidhinishwa na chama. Inadaiwa kuwa kwa baadhi ya mikoa, fedha hizo hazikwenda kabisa na hivyo kufanya baadhi ya wagombea kujigharamia hali iliyochangia kushindwa kwao.

Nani anampendekeza Luhwavi awe Mwenyekiti wa CCM? Hili lipo dhahiri. Luhwavi anataka Jakaya Kikwete aendelee kwenye wadhifa huo. Matarajio ya Luhwavi ni kwamba, ikiwa Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, atamteua yeye (Luhwavi) kuwa Katibu Mkuu kujaza nafasi ya Katibu Mkuu wa sasa Abdulrahman Kinana ambaye ametangaza kuachia nafasi hiyo baada ya Mkutano Mkuu wa Julai 23.

Mpaka sasa, Luhwavi amezunguka kwenye mikoa kadhaa ya Tanzania Bara kuhamasisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wasiridhie hoja ya Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM. Inasemekana kuwa mpunga wa kutosha umetembea kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ili wamkwamishe Rais Magufuli.

Hata hivyo, inaonekana dhahiri sasa kuwa mkakati wa Luhwavi na Timu yake umegonga mwamba. Mwenyekiti wa sasa Jakaya Kikwete amesema hataongeza hata sekunde moja na kwamba dhamira yake ya kwenda kulala usingizi baada ya Magufuli kushinda Urais iko pale pale. Hana mashaka hata kidogo na Rais na anawabeza wale wanaodhani kuwa Magufuli hana uzoefu wa kutosha kuongoza chama. Kwamba, kama amechaguliwa kuwa Rais wa nchi, atashindwaje kuongoza chama?

Nani walio nyuma ya harakati hizo? Nitaendelea kuwajuza kwa kadri tunavyokaribia Julai 23. Stay with me. Niwapongeze tu na kuwatia moyo baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Dar es Salaam, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma ambao wamenipa ushirikiano wa kutosha wakati ninafuatilia jambo hili mpaka mchawi amejulikana. Mikoa hii ni miongoni mwa mikoa ambayo Luhwavi alitembelea kufanikisha mkakati wake.
Lizaboni wewe lini umeanza kuhubiri siasa za woga namna hii?
Team JPM mna shida sana, inaonesha uwezo wenu wa kujiamini ni mdogo mno, hamuwezi kutangaza sera kwa intimidation! Bungeni kuna mtu anatishia watu, mtaani watu wanaogopa na chamani kote mnaishi kwa kutishana, kubaguana na kulumbana bila ya sababu za msingi!
Just imagine, mtu kasema jamaa hafai, ktk siasa kinachofuata ni wewe kumuita mchawi! JPM afight back kwa kunadikunadi mikakati yake, haiingii akilini huku mnahubiri awamu hii hakuna kubebwa huku nyinyi mkitaka mbebwe!
Hongera zake huyo Naibu katibu anayechallenge nafasi ya mwenyekiti! Ningemshauri next move aweke bayana kuwa yeye anataka kumchallenge JPM ktk nafasi hiyo, sio lazima JK aendelee kuwa mwenyekiti!
Binafsi si mchukii JPM Ila penye mapungufu aambiwe na tunapoona anafaa tuseme! Nchi haiwezi kungia wazimu wa kuimba na kusifu kila kitu hata kama tukidhani sio sifa stahili!
Please acheni kusema watu vibaya au umetumwa?
 
Ni sawa na kudhani unaweza toa CPU bado ukatumia computer. Hoja inaweza kuwa na ukweli lakini its not handled careful.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom