Tetesi: Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara

Tetesi: Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara

Status
Not open for further replies.
Lizaboni kuna ukweli fulani hukuueleza hapa, ama kwa makusudi ama kwa bahati mbaya kwamba katika miezi ya mwanzo ya mkakati huo m/kiti anayeondoka alikuwa bega kwa bega na Rajabu Luhwavi katika mpango huu, na katika hali ya kawaida Luhwavi asingeweza kuuinjinia mpango ambao bosi wake anayempigania hajakubali kuendelea kukikalia kiti hicho.

Kwa sababu JK anajua sana kucheza na akili za watu mbayu wayu alikuwa akipiga ndogo ndogo huku akitegea kuona reaction ya wananchi, wanaCCM na wajumbe wa mkutano mkuu huku Luhwavi yeye akijiamini, akichanja mbuga kuwarubuni wajumbe, lakini JK alivyodokezwa na watu wake upinzani unavyoongezeka alijitoa kimya kimya bila kumpa dokezo naibu katibu mkuu wake aliyedanganyika akidhani anaungwa mkono.

Ilitokea bahati mbaya sana kwa Luhwavi baada ya askofu Gwajima kuhudhuria katika moja ya mikutano yake ya siri akitegemewa atasaidia kumshambulia Magufuli kuhusu kupewa uwenyekiti lakini badala yake Gwajima alianza kuanika njama za baadhi ya viongozi wa CCM kumnyima uenyekiti Magufuli.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hata mkiondoa kabisa hiyo nafasi ya uenyekiti ni sawa tu.
 
wewe ni wakala wa nani mkuu acha unafiki subiri tarehe 23 uone huu ni muda wa mabadiliko ndani ya chama Magufuli Magufuli hawezi kuwa mwenyekiti hana uzoefu wa uongozi wa kutosha labda apewe umakamu mwenyekiti ajifunze kwanza.
Mtanyooka tu na jamaa zako ambao ni mafisadi jpm atakabidhiwa chama na chama kinasukwa upya hakuna kuchana na wezi mafisasi kama nyie.
 
Duh hivi inawezekana kweli?just thinking loud
 
Mangiri naona mnararuana. Mambo hayo kamuulize mama ako uone kama ana rinda hata moja.
Mama yako yupi sasa mkubwa au mdogo maana najua unao wengi niambie ni yupi,kiukweli mafisadi mmeshikwa pabaya sana mtalala bila nguo tu chezea magufuli wewe.
 
Taarifa za uongo hizi wanajamvi zipuuzeni..sio lazima rais awe mwenyekiti wa chama ni vizuri kumpunguzia mzigo...unamuonea tu luhwavi...hata Mwandosya alishawahi kupinga Magufuli kuwa mwenyekiti wa chama....Huwezi ongoza chama wakati hata tawi hujawahi kuongoza Magufuli asipewe chama atakivuruga
Hivi Mwandosya bado ni mwana ccm?
 
Tunaomba Mheshimiwa KINANA aendelee na u SG, kwa muda wa miaka miwili, ili amsaidie Mheshimiwa Magufuli kusafisha chama. Kinana ni mtumishi asiye na uchu wa hana magenge. Brother the country and the party needs you.
 
Huyu anataka kupata kick tu hana jipya...subir ukuu wa,wilaya
 
This is exactly what the right bishop, Gwajima, said lakini sasa mmmmhhhhhh akaitwa mchochezi.
 
Si useme umekopi kwa Gwajima mliyemtuhumu kwa uchochezi
 
Hawa CCM ikifika nyakati kama hizi kila mtu uwa anavutia pande zake ili mradi kutengeneza mazingira flani hivi ya kutoaminiana.
 
b22de1982d0267b2e4f0a3304bc7bd87.jpg


Pesa za kampeni alizozipiga, ngoja JPM awe Mwenyekiti atazichojoa tu
 
Kwani mlivyosema mafisadi wameshatoka CCM mlikuwa mnamaanisha nini? Ama ni ugomvi wa vyeo tu?
 
Mimi ninapoikumbuka kauli ya Luhwavi wakati wa kampeni kuwa siyo lazima Rais awe Mwenyekiti wa chama na kusema kuwa mkutano mkuu wa Chama ndiyo utaamua, huwa nina mashaka na hii kauli yake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom