maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Lizaboni kuna ukweli fulani hukuueleza hapa, ama kwa makusudi ama kwa bahati mbaya kwamba katika miezi ya mwanzo ya mkakati huo m/kiti anayeondoka alikuwa bega kwa bega na Rajabu Luhwavi katika mpango huu, na katika hali ya kawaida Luhwavi asingeweza kuuinjinia mpango ambao bosi wake anayempigania hajakubali kuendelea kukikalia kiti hicho.
Kwa sababu JK anajua sana kucheza na akili za watu mbayu wayu alikuwa akipiga ndogo ndogo huku akitegea kuona reaction ya wananchi, wanaCCM na wajumbe wa mkutano mkuu huku Luhwavi yeye akijiamini, akichanja mbuga kuwarubuni wajumbe, lakini JK alivyodokezwa na watu wake upinzani unavyoongezeka alijitoa kimya kimya bila kumpa dokezo naibu katibu mkuu wake aliyedanganyika akidhani anaungwa mkono.
Ilitokea bahati mbaya sana kwa Luhwavi baada ya askofu Gwajima kuhudhuria katika moja ya mikutano yake ya siri akitegemewa atasaidia kumshambulia Magufuli kuhusu kupewa uwenyekiti lakini badala yake Gwajima alianza kuanika njama za baadhi ya viongozi wa CCM kumnyima uenyekiti Magufuli.