Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya


Tatizo akidi haitatimia bungeni
 
Wote tunajua moja ya vitu ambavyo Rais anaapa vizuri kuvilinda siku anapokabidhiwa nchi in Katiba.

Ivi chombo gani kinatakiwa kumwajibisha pindi anapo ivunja katiba ya jamhuri ya Muungano?

Na je nani mwenye mamlaka ya kutambua kuwa Rais amevunja katiba hatua zichukuliwe?

Je baada ya kustafu kosa la kuvunja katiba linaweza kumfikisha mahakamani Rais was Jamhuri ya muungano?
 
Ni muda mrefu watu wamekuwa na malalamiko juu ya Rais aliyemadarakani na ilishawahi kujadiliwa Bungeni juu ya kumshtaki au kutomshtaki aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu.

Hata hivyo kwa mujibu wa Ibara ya 46(1) na (3) ya Katiba yetu ya 1977 ni marufuku kumshtaki Rais kwa kosa alilofanya akiwa madarakani wakati bado anaongoza Ib. 46(1) na baada ya kuondoka madarakani Ib. 46(3).

Pamoja na kwa chini ya Ibara 46A kunauwezekano wa kumshtaki Rais wakati na baada ya uongozi wake, utaratibu huu ni mgumu sana kutimiza masharti yake haswa ukizingatia uwiano wa vyama Bungeni.

Je, ni wakati sasa wa kubadilisha msimamo huu haswa wakati huu wa sera za uwajibikaji? je, hatutaondoa amani ya moyo kwa Rais aliyemadarakani inayomsaidia kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
 
Haya yameandikwa na aliyekuwa Mbunge Mzalendo aliyepigania nchi hii na hatimaye kutishiwa hata maisha na mwishowe kupokwa ushindi wake wa Ubunge. Prof David Kafulila. Hawa ndiyo waliopaswa kuwa Maprofesa ukiachana na wale ma Pro-pesa.

Anasema bado watanzania wanamlilia JPM aokeo hasara tunayoingia ya Bilion 7 anazolipwa Singasinga kila mwezi ambazo ina maana kwa miezi miezi kumi na mbili ni tsh bil 84 tungeweza kununua ndege mpya kila mwaka ikiwa tunataka ndege. Lakini tungeweza kubomoa nyumba zilizopo buguruni kwa mnyaman halafu tukaanza kujenga mji wa kisasa pale na kuwapatia wananchi na nyingine kupangisha kila mwaka.

Hapo ukiacha Bil 305 alizopewa na ikulu ya kikwete pamoja na viongoz wengine nadhan ikiwa ni mgao. Kukosekana kwa nguvu katika Bunge letu,maslah binafs,kukosa uzalendo n.k kunafanya lishindwe kumwajibisha rais fisadi,mfujaji au mwizi. Hapa tudai katiba nzuri.

CAG na TAKUKURU walithibitisha pesa za ESCROW hazikuwa za singa singa. Kikwete peke yake na watu wako waliofaidika na pesa hizi walisimamia kidete kusema ni za singasinga.

Jambo hili tu lilitosha kumchunguza ndugu kikwete. Lakini anadunda tu mitaani mpaka leo hii. Na ndio maana kwa uzalendo Gen Ulimwengu alisema huyu jamaa alipaswa achunguzwe au awekwe ndani.

Inaumiza sana wakati serikali inawakamua wananchi kodi /damu mpaka tone la mwisho wakati kuna ambao walipaswa walipe hizo pesa. Ni Afrika tu mgonjwa wa malaria anatolewa damu ili iwe sadaka kwa miungu ambao wameshakunywa sana damu mpaka wanaamua hii wanayopata wawe wanaoga.
 
Huu uzi Life Span yake JF ni Masaa kadhaa.
Umejaa uchochezi na uchonganishi na pia unafungua mageti yanayoelekea Kisutu
#Hatuna_Milioni_7
 
Watalindwa kwa nguvu zote, halafu yeye anataka sisi tumuombee
 
Turbo prof. Ibrahim h lipumba "TUTAJITOA KWENYE HUU UKAWA"
 
Kuna vitu vingine ukifikiria vinaumiza sana. Vijana inabidi tujifunze kuwa wazalendo katika umri huu wa sasa ili tabia nzuri ikomae ndani yetu. Pia tusome kwa bidii tupate maarifa ya kutosha Kwasababu hawa wazee wanataka siku wakifa wawe wametuachia nchi ambayo ni 00
 
Ila kwa sasa wanakamua damu kwa wagonjwa kweli kukusanya kodi.... yaani magari yaliyo isha kuwa scraped tangu 2008 unayalipia motor vehicle na kodi leo...
 
Hata akiondolewa kinga unadhani atashitakiwa? labda chama cha upinzani ndio kiwe katika utawala ila kama chama chake ndio kinaongoza nchi bado ataendelea ku enjoy maisha mazuri.
CCM ni chama cha mafisadi ndio maana wote katika system lazima waekwe watu ambao ni wanachama wa CCM na wenye kadi za CCM ili kuwalinda viongozi wa CCM
DPP ni Mwana CCM
Takukuru ni Mwana CCM
Msajili wa vyama ni Mwana CCM
IGP ni Mwana CCM
Mwenyekiti wa NEC ni Mwana CCM
Mwanasheria na Naibu wake ni Mwana CCM
 
WaTz mnapenda kumshitaki Nyani kwa Tumbiri ili aonekane mwizi wa mahindi tu lakini mkijua hawezihata kukemewa . Katiba pendekezwa ya Waryoba ilikuwa imefungia kinga zote za kijingaza rais ndaniya jeneza tayari kwenfakuzikwa. Hamtaki kumsema Tumbiriwenu chaujanja aliyefungua jeneza hilo kwa lugha ya porojo na hata kusababisha vijana eetu kurushiana makonde na viti kutetea kufunuliwa kwa jeneza hilo. Hamkumlaani Kikwete kwa kudai eti mnampenda na kumsifu kuwa kiongozi bora. Mbona alihofia zaidi kuondolewa kwa kinga hizo? Angeacha mkamshitaki Mkapa wenu na sisi tukamshitaki Kikwete wetu ndiyo mngejua yupi alikuwa fisadi ndani ya Ikulu. Aliyerukia kuzuia Katiba ya Waryoba ndiyo ana kesi kubwa ya kujibu kwa waTz.
 
Ďu
Duh! Hii namubaliana nayo 100% kama niliandika mimi. Lazima ilikuwa saa sita usiku na nilikuwa nimechelewa kulala. Lakini wakuu huo ndiyo fact!
 
Katika katiba yetu ya Tanzania,kuna kinga maalum ya Rais kutoshtakiwa. Kinga hii uhusu Rais anapomaliza muda wake wa uongozi kutoshtakiwa kwa makosa aliyoyatenda akiwa madarakani,katika kutekeleza wajibu wake

Mambo mengi yanayofumuka sasa yameanza kwenye awamu zilizopita. Wastaafu wetu wasingekuwa na kinga wangechunguzwa,kuhojiwa na hata kuburuzwa mahakamani. Mengi yangejulikana na kurekebishwa kwa tawala zilizopo na zijazo. Ingekuwa somo

Madudu yote ya sasa yamezaliwa na yaliyopita. Katiba yetu inatulazimisha kuamini na kufuata methali: yaliyopita si ndwele,tugange yajayo. Katiba yafanya wakuu kujisahau.

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Songea,Ruvuma)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…