Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

sasa kama spika anafikilia hivi, je wabunge wa CCM kweli wana uwezo wa kubadili sheria ya madini kweli kwa manufaa ya Taifa.

Kama ni Taifa kwanza, hawa L, S ni nani hadi wanaonekana wao wakiguswa Taifa limeguswa.

huyu spika ndo Jana kaongea kwa majonzi au alikuwa anamuogopa Rais tu na kumuadaa.

bado sana ndani ya ccm kupata mtu mwingine kama JPM, bado sana sana tu.
Leo eti Chenge bado Mwenyekiti wa bunge, spika, naibu, katibu wa bunge, Waziri Mkuu wote wanaangalia tu badala ya huyu kuwa korokoroni.

we are not yet serious
 
Ulitegemea Nini!
Ndugai anatetea ugali wake lazima afanye anachofanya kuwaridhi mabwana zake
[HASHTAG]#HappyAnniversaryToMeInJF[/HASHTAG]
Usikwepe hoja.
Mkapa.
Kikwete
Sumaye
Lowasa.
Je upo tayari hiyo team yote ishtakiwe?
 

Mwingine yupo Bungeni tena ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini
 
Huyo naye anastahili apandishwe kizimbani kwa kulifanya bunge kuwa kitengo cha MACCM na kuliendesha kihuni. Wanagawana rushwa Bungeni haya MACCM ya milioni 10 kila mmoja ili kupitisha muswaada uchwara wa kuminya habari nchini. Spika kimyaaa, Naibu spika kimyaaaa, Waziri Mkuu Kimyaa. Yanapitisha mikataba ya kifisadi iliyojaa ufisadi wa hali ya juu kwa dharura utadhani kuna haraka ya kufanya hivyo halafu leo yanaweweseka yanataka tumsifie Magufuli! Tumsifie huyu kwa lipi wakati zaidi ya miaka 20 alikuwemo Bungeni na ndani ya Serikali kupitisha hiyo mikataba ya wizi wala hakutia neon hata kwa sekunde moja. Hili nalo la MACCM kugawana rushwa MACCM bado yanamtafuta mchawi aliyewaroga ili yagawane rushwa kufanya uhuni wao.


 
!
!
Aisee..... Usitegemee lolote toka kwa wazee wa ndiooooooo.... Wamechanganyikiwa hawajui washike wapi
 
Kinachowauma chadema ni kwamba kila mti wanaogusa, ukiangushwa unaangukia hadi nyumba yao!
 
Huyu jamaa anaqualify kuwa ni janga la taifa. Kwa akili ile na kiti kile na madaraka yale itakula kwetu. Vote of no confidence kwa Ndugai on grounds of incompetence and partisanship ifanyike kuondoa hii balaa
 
"Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena," amesemaNdugai.

Chanzo: Mwananchi


Hii ya Mwaka.
Duh! Naona spika anahitaji kupunzika. Hivi anadhani Upinzani hawajui kama Lowasa na Sumaye wako huku?
Kwa hiyo 40milioni ya watanzania waumie kisa kuna pande mbili Marais vs Mawaziri Wakuu. Huku kunaitwa kufikiri kimasilahi binafsi .
 
CHADEMA hata kama wasingewapokea hao bado tu wangepondwa...Ni kawaida opposition kuitwa majina yoyote na rulling party

Ni kweli ila waliokuwa wanaponda ili kujikinga kwani wasingeweza kukaa kimya bila kujitetea, na wananchi walikuwa na imani sana na upinzani ule. Sasa leo cdm inapata wapi nguvu ya kupambana na ccm wakati waongoza mashambulizi wa cdm ni Sumaye na Lowassa!!? Cdm ilikubalika kwa kunyooshea mkono ufisadi na mafisadi, leo hii si tunakufa na tai shingoni kwa kukumbatia watu ambao hawajawahi kukubali sera zetu, hawajawahi kusupport upinzani hata kwa bahati mbaya. Hao wako cdm kwa ajili ya madaraka tu ila kiroho bado wapo ccm. Kwa taarifa yako leo hii Magufuli ni rais wa nchi hii kutokana na upinzani uliokuwa na nguvu, ilionekana ndio mwanaccm mwenye afadhali ya kupambana na upinzani, kubali kataa.
 
Ni vema Speaker wa Bunge letu Tukufu akatambua kuwa hao anaosema wapo Upinzani na hivo waweza kuathiriwa na hoja ya Mbunge wa Kilombero hawana KINGA. Kama wana makosa, ni juu ya vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua stahiki. Hawawezi kulindwa ili kuwalinda viongozi walio na kinga. Mheshimiwa wetu huyu ameonyesha udhaifu wa ajabu kwa kauli yake hii.
 
Si juzi wameimba wana imani nao?! Au washasahau mara hii!!!!
 
Mbunge anataka marais wastaafu washtakiwe, supika anatuchanganyia madesa, mawizir wakuu sijui wanatoka wapi? ikifika wakati wanatakiwa kuwajibishwa wawajibishwe tu bila kujali wapo chama kipi, kwani wao kwenda upinzani wamewekewa kinga ya kutoshtakiwa? hii spika nina mashaka na uwezo wa akili yake
 
Usikwepe hoja.
Mkapa.
Kikwete
Sumaye
Lowasa.
Je upo tayari hiyo team yote ishtakiwe?
Kwani huyo Sumaye na Lowassa wana kinga gani ya kushtakiwa mpaka aseme hivyo? haki ya nani kumbe Bunge tunalilaumu bure bali ni kuwa lina kiongozi mbumbumbu kabisa. Aliyemuambia kuwa Wapinzani hawataki Sumaye ashtakiwe kama kakosea nani?
Nadhani yale matibabu ya India waliondoa nati kadhaa kichwani mwake
 
Reactions: BAK
Bado MACCM yako busy kutafuta namna ya kukingiana vifua! Watu wa ajabu sana hawa! Sasa wanawatisha CHADEMA eti wakipandishwa kizimbani mafisadi Mkapa, Kikwete na wengineo ndani ya MACCM basi na hao waliohamia Chadema watapandishwa kizimbani! Hivi ni lini CHADEMA walitoka kauli ya kupinga hao waliohamia Chadema kama walihusika na makosa yoyote yale ndani ya Serikali wasipandishwe Kizimbani?

Hizi ZERO BRAINS zinaiangamiza nchi yetu.

Asitafute sababu na visingizio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…