Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya


Tatizo bush atukani watu kama huyu Rais wa Malofa anaita watu wapumbavu kisa amewaibia
 
Tukubali tu ukweli. Tujiulize:-

Kama sisi kweli sio MALOFA NA WAPUMBAVU kwa nini tulitunga sheria ya kumlinda mtu aliyetuibia matrilioni na kututukana juu ?
 
Naunga mkono hoja yako,kuna umuhimu wa kuacha kulindana taifa letu ni changa ili tufike mbali lazima tuthubutu.
Kuleana leana kuna tufilisi.
 
Ndiyo maana hata NSSF menejimenti yote ilifuakuzwa lakini MD wake akateuliwa kazi nyingine. Kamchezo mzuri sana.
 
Ndio maana tunasema kinga inayompa kibur kikatiba iondolewe!
Hivi sheria hiyo ya kinga ikiondolewa, itaanza kutumika kwa nani?
Aidha, napenda kujua kama sheria hii au kifungu hiki katika katiba kilitungwa kwa lengo lipi? Je, lengo hilo limepitwa na wakati na kama ni ndio, je utaratibu wa kukiondoa ukoje? Nani wa kukiondoa?
 
Tukubali tu ukweli. Tujiulize:-

Kama sisi kweli sio MALOFA NA WAPUMBAVU kwa nini tulitunga sheria ya kumlinda mtu aliyetuibia matrilioni na kututukana juu ?
Sheria hiyo walitunga hao ccm na walipitisha wenyewe

Ova
 
Nimesoma vipengele vyote humu ndani ila vyote naona havina msingi vimeegemea kwenye chuki na sio hoja wekeni hoja watu kuwa na Mali au matajir au kunufaika na nchi yao kwa kufanya kazi sion kosa wote hao mliowataja niwatanzania na wamefanya kazi na hayo mafanikio yao nikutokana na kaz ,kumbukeni pia wamewaajir watanzania wenzetu kifupi msiwe na chuki jengen hoja

Mungu pamoja nasi
 
Kibaka anachomwa moto....
Jizi kubwa namna hii linakula a/c...
Nyumbani a/c, kwenye gari a/c, kila aendako a/c
Hiyo ndio tofauti kubwa kati ya vijibaka na jizi mkapa

Tehe, leo upepo wa shutuma umelekea kwa chinga😉😀
 
Wanasema No One is Above The Law lakini tunajua Pakiwa na mtu ambaye hawezi shtakiwa maana yake huyo yupo above the law
Kwa Watanzania wote, wawe watumishi wa umma, wana siasa, wakulima, wafanya biashara, tuungane wote na kupeana elimu.
Kila mtu ajue kuwa mafisadi wakubwa ni wale waliopewa madaraka makubwa.
Katiba ipatikane au kinga iondolewe!!
 
Kukionekana dalili za upinzani kuingia magogoni kitabadilika.
Hilo litatokea, kwa sababu ilishatokea kabla. Kama mnakumbuka vema, siku za nyuma wakati chama cha CUF kilikua na wabunge wengi na kutengeneza kambi rasmi ya upinzani bungeni, CUF wakushirikiana na CCM waligoma kuwapa madaraka wapinzani wenzao akina UDP, NCCR na Chadema. baada ya mambo kugeuka na Chadema kufanya majority ya wabunge, CCM walitaka walibadili vipengele ili Chadema wawashirikishe madaraka wapinzani wenzao. Hii ni kabla ya mpango wa UKAWA.
 
Wanatengenezewa wigo wa kufanya lolote na pia hali hii inawafanya viongozi hao kuwa miungu watu! Hakika siku kinga zikiondolewa tutaheshimiana! Watawaheshimu raia wanaowaongoza na waliopata kuwaongoza!
Kinga inawaruhusu kufisidi nchi wakiwa madarakani na baada ya kutoka madarakani,
Kinga inawaruhusu watukane na kuwatovukia adabu raia waliowapa ajira huku ikiwanyima haki raia kupata haki zao za kulindwa dhidi ya kudhihakiwa na kudhalilishwa.
Kinga kwa viongozi waliotuongoza na kutumia ofisi kwa manufaa yao zinapaswa kuondolewa ili adabu na nidhamu za utumishi bora zichukue nafasi yake, vinginevyo tutapiga deki huku tunaingiza matope ndani!
wameshastaafu wanafuata nini majukwaani? (mbona Daniel Arap Moi na viongozi wa kariba yake hatujawahi kuwaona wakipanda majukwaani?)
Hivi Tanzania tuna matatizo gani?
 
Kwintara Kwinyira amezindua kampeni yake (Social media campaign) ya kupinga UKUKU nchini. UKUKU means Umoja wa Kukubali kila kitu bila Kuhoji. Kuna watu kazi yao ni kuunga mkono kila kitu ili mradi kimesemwa na kiongozi wake.

Tabia hii imeshamiri sana kwa wafuasi wa CCM. They dont reason at all. Ila mradi kiongozi kasema wao ni NDIOO.

Godbless Lema anasema tatizo sio wao, tatizo ni akili zao. UTG wanaita huo ni uzwazwa, lakini Kwinyara anasema ni UKUKU. Kukubali kila kitu bila kuhoji ni UKUKU.

Watu walewale waliosema JK aongezewe muda, kwa kuwa amesaidia sana taifa, ndio haohao wanaokazana sasa JPM aongezewe muda na kusema JK aliharibu nchi. UKUKU.!

Watu walewale wanaoshangilia viongozi wa upinzani wakikamatwa kwa kufanya mikutano ya siasa, ndio haohao wanaoshangilia CCM ikifanya mikutano. UKUKU.!

Watu walewale wanaopitisha mrabaha wa 04% kwa makofi na kusema unatosha, huku wakiwazomea wapinzani waliposema hautoshi, ndio haohao wanaoshangilia kufikishiwa 06%. Mnashangiliaje kupandishwa kwa kitu mlichosema kinatosha? UKUKU.!

Na kwa sasa wapinzani wanasema 06% hazitoshi, wao wanasema inatosha. Akija Rais baada ya JPM akaziongeza tena watashangilia na kumuita mzalendo. UKUKU.!

Watu walewale walioshangilia Ngeleja kurudisha hela TRA ndio haohao wanaoshangilia TRA kuzikataa. UKUKU.!

Walioshangilia JK aliposema pesa za Escrow si za umma, ndio haohao wanaomshangilia JPM kusema pesa zilikua za umma. UKUKU.!

Nchi hii imeharibiwa na hawa KUKU. Kila kitu wanakubali tu bila kuhoji. Kataa UKUKU, kataa kuwa KUKU, kataa viongozi MAKUKU.!

U = Umoja wa
KU = kukubali kila kitu bila
KU = kuhoji.

Tuma kwa watanzania wengi kadri uwezavyo, wajue KUKU wanaoharibu nchi yao. Tusiwaachie kuku nchi yetu. Kataa UKUKU kwa nguvu zote, kataa kuwa KUKU, kataa viongozi MAKUKU.!

 
Hii nayo ni thread? Au mipasho ya mwambao?
 
Hao ni wale ambao hata maana ya dhana ya UZALENDO hawaifahamu!!!

katika hali ya ajabu kabisa, wanadhani Uzalendo ni kuunga mkono kila kinachotoka kwenye mikono na midomo ya serikali hata kama ni cha kijinga!!!

Hawa wanadhani Uzalendo ni kutetea uongo wa serikali kwa sababu tu uongo huo unawahusisha watu wa nje!!

Kwamba, serikali ikisema 1+1=11 basi useme NDIYOOOOOOO vinginevyo utakuwa sio mzalendo!!

Hawa wanadhani ujinga na uju'ha ni sehemu ya uzalendo!!!

Wasichojua ni kwamba, Uzalendo ni loyalty ya mtu kwa nchi yake na sio kwa serikali yake!! Mzalendo wa kweli ataiunga mkono serikali endapo tu serikali husika inafanya jambo lenye manufaa kwa nchi na sio porojo au propaganda!!!

Wasichojua ni kwamba, Mzalendo wa kweli akiona serikali inatumia ujinga wa wananchi kuwalaghai na kuwadanganya, lazima atasimama kidete na kusema wazi wazi kwamba SERIKALI INASEMA UONGO NA KUWADANGANYA WANANCHI WAKE!!!!

Wasichojua ni kwamba, Mzalendo wa kweli yupo tayari kupambana na serikali kwa nguvu zote endapo anaona serikali inafanya jambo la kijinga na pengine lenye kuhatarisha maslahi mapana ya nchi!!!
 
Huo ndio ukweli mkuu, ni rahisi sana kuupongeza utawala huu kuliko kuutetea.

Kuitwa mwanaccm ni kipimo tosha cha IQ, asubuhi wataunga mkono kilichotamkwa kwa mishipa yote jioni wataunga mkono tena kwa mbwembwe kukanushwa kwa kile kilichosemwa asubuhi.

Kwa kifupi ukiwa huko uache kureasoan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…