Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

******** atakuwa wa kwanza kushitakiwa kwa uvunjaji wa haki za binadamu.
 
kwa tz hii na maiti hawa wanaoitwa wananchi ni vizuri kuota
 
Tutaanza na huyu huyu !
Miaka miwili tu chato imekuwa vile. Pia kivuko ,risasi nje nje,maiti kila kona,bajeti haijulikani!
LAZIMA ATAELEZA!
 
Ufisadi hauna chama,kabila,rangi,cheo.Hata huko upinzani kuna mafisadi,wakwepa kodi,wauza mihadarati,matapeli,majizi n.k.Unapompa kimada wako nafasi ya ubunge kisa ni kimada wako au kimada wa rafiki yake tayari huo ni ufisadi,unapodai nyumba ya shirika la umma ni yako wakati unajua sio yako tayari ni ufisadi,unapokuwa na mimali isiyoelezeka wakati hujawahi kuwa mfanyabiasha hata siku moja huo ni ufisadi
 
CCM ndipo kuna Ufisadi wote, mawaziri wengi hasa wa kike zipo tetesi kibao, ununuzi wa ndege kwa cash, ujenzi Chato Airport, viwanja vinginevyo vya ndege, bomba za gesi, mafuta, ujenzi wa reli kote kuna Ufisadi pia zipo 10% za Wajanja wachache huko CCM , una Dili nyingi wamepiga ikiwemo kivuko cha Dsm-Bagamoyo , uuzaji nyumba za serikali akajiuzia nyumba kibao na zingine akagawa kwa hawala na mdogo wake ambao hawakuwa watumishi wa umma.
 
Labda kama wewe ni mtoto mdogo.... Miaka yote tangu enzi za Hayati Baba wa Taifa zilipokuwa zinatolewa tuhuma za ukabila/udini/ukanda haijawahi kuwa ktk mtazamao unaouwaza.
Ziliangaliwa higher positions za ufanyaji maamuzi na ndio malalamiko yakaibuka. Huwezi kusema mbona manesi wanatoka kabila zote, au walimu, n.k. Nakushauri fuatilia historia vizuri na tafuta hata hotuba za Baba wa Taifa na vitabu vyake usome.

Pia mimi sikuzungumzia mambo ya Chadema, endelea kuvaa u-CHADEMA/u-CCM uone kama utaelewa kitu
 
Kwani tunatafuta afadhali mkuu?
 
Eti umesema yeye ni binadamu sio malaika wakati yeye mwenyewe amesema mungu atanteua awe kiongozi wa malaika
 
Ukiona mwanaume kila siku anasimulia habari za wanaume wenziye kila siku ujue siyo Riziki
 
Mkuu hapo umekosea. Heshima si utumwa. Ni vizuri tuiheshimu taasisi ya URAISI hata kama hukubalini naye.
Ni MTANZANIA mwenzetu na wala si hivyo usemavyo.
Tujadili hoja badala ya matusi na kubezana. Ama vipi mkuu?
Ni kweli usemacho! Lakini wao ndo wanapandikiza haya mambo, wangejibu hoja za askofu Niwemugizi, kakobe na mwanafunzi Nondo badala ya kuwaita uhamiaji!
 
Kwa katiba yetu haiwezekani labda wakati ukifika wa kuweka hilo unalotabiri. Kweli ndege tumeziona Je, vipi kipato cha mtu wa chini kokoje nacho
 
Ni kweli usemacho! Lakini wao ndo wanapandikiza haya mambo, wangejibu hoja za askofu Niwemugizi, kakobe na mwanafunzi Nondo badala ya kuwaita uhamiaji!
Nakuelerwa mkuu. Wakati mwingine wanahitaji kuchukuli mambo kwa utaratibu isionekane kama ni visasi.
Pengine ni maamuzi ya watu wa ngazi za chini. Inahitajika Magufuli kama rais awaambie "Msiniharibie serikali yangu kwa kuwaita watu wanaotoa maoni eti ni Wahamiaji"
Nakuelewa kabisa,
 
Ukiona mwanaume kila siku anasimulia habari za wanaume wenziye kila siku ujue siyo Riziki
Mkuu umeniacha kwenye mataa. Umeongea kwa mafumbo sijakuelewa.
Samahani lakini. Una maana gani.
Ni mimi ama ni mtu mwingine ?
 
Tutaanza na huyu huyu !
Miaka miwili tu chato imekuwa vile. Pia kivuko ,risasi nje nje,maiti kila kona,bajeti haijulikani!
LAZIMA ATAELEZA!
Chato ni Tanzania ama ni Uganda?
Kivuko kimefanya nini?
Mengine SIYAJUI mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…