Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

mkuu kwa uchumi tulionao, wabunge wa sasa hawata mtetea mtu, km mtu fisadi atakatwa tu, tena magufuli anahasira nao sanaa

Kwa uchumi tulionao unamaanisha nini mkuu?
 
 
Mkapa Ni zaidi ya shetani.asilimia kubwa watz tunateseka kwa sababu yake,huyu jamaa ana Roho mbaya sana.

Una chuki binafsi ww, ni mwendawazimu pekee anaeweza kuponda utawala wa Mkapa na akasifia utawala wa Kikwete
 

Kwa huyo nadhani ni kumpa msamaha tu kama wale waliotajwa kwenye vitabu vya ibada
 
Watanzania kila siku na kila kukicha tunalalamika juu ya wizi,rushwa na ufisadi wa viongozi.Malalamiko haya kwa hivi sasa ndio yameteka media na ndio imekuwa ni agenda ya kitaifa.

Hata hivyo,utashangaa hakuna media yoyote, Taasisi yoyote,wanaharakati wowote wale wala mitandao ya kijamii inayojaribu kuendesha harakati za kupinga na kutaka kuondolewa kwa kipengele cha katiba kinachotoa kinga ya raisi kutoshitakiwa mahakamani kwa makosa aliyoyafanya awapo madarakani na hata baada ya kustaafu.

Kama sikisei,hata katiba ya Warioba na katiba inayopendekezwa badao imebeba kipengele hiki!!

Maswali ninayojiuliza.

Hivi kweli tunajitambua?

Hivi kweli tuko serious?

Tunataka mpaka nini kitokee ndio tujue hii kinga inatugharimu?

Kama tumeridhika na uwepo wa kinga hii,tuna haki gani au tuna uhalali gani wa kulalamika?

Watanzania wenzangu, ni nani kalutuloga?

Kama ni "limbwata",litakuwa ni limbwata la aina gani hili?
 
Hata katiba ya warioba ubovu wake ulikuwa ni iyo kinga ya Rais
 
Sasa hili neno kwamba no one is above the law inatakiwa lirekebishwe liseme no one is above the law except the ones with hiyo kinga.
 
Napata kigugumizi mtu anayepinga katiba mpya
 
kipengele hicho kikiondolewa Raisi kazi yake itakuwa kushinda mahakamani badala ya kufanya kazi za kiraisi,Wahuni utasikia leo wamemfungulia kesi mahakama ya kisutu,kesho anatakiwa mahakama kuu kanda ya mwanza keshokutwa anatakiwa mahakani songea nk.Kufuta hiyo sheria ni ujinga mtupu.Kuiweka ni kumwezesha afanye shughuli zake asikae anakesha mahakamani.Ukiruhusu kwa viinchi vyetu hivi kila siku watu watakuwa wanamburuza raisi hata kwa vitu vya kijinga tu mara kanichukulia mke wangu au mume wangu n.k

Raisi sio sawa namwanachama Chapombe wa UKAWA ambaye kutwa anatakiwa mahakamani kwa kesi za kunywa viroba bila kulipa
 
Sisi ni watu wa kulalamika kila kukicha kuhusu ufisadi na wakati mwingine tunawalalamikia sana waliopata kuwa maraisi wa nchi hii.

Kwanini malofa:Nani kati yetu humu JF,vyombo vya habari,wapinzani,Tume ya Warioba na hata Bunge la katiba wameonyesha umuhimu wa kujadili na kupinga kinga hii ya raisi?

Ni lini tumewahi kuwa na mjadala wa kitaifa juu ya hii kinga ya raisi na madhara yake?

Ni lini umewahi kuwasika ITV,Channel 10,Star tv,TBC1,Azam tv n.k,wakiwa na mada kuhusu kinga ya raisi ya kutoshitakiwa mahakani?

Kwenye Bunge la Katiba hii ilikuwa ni hoja ya msingi?

Katiba ya Warioba iliondoa kinga ya raisi?

Mara ya mwisho kusoma makala au habari katika gazeti lolote inayohusu kinga ya raisi ni lini?

Mkapa alituita baadhi yetu malofa ila naona alipaswa kuwa more general kwa kuwahusisha na watu wa chama chake pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…