Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Malofa ni wabunge wa ccm pamoja na Vibaraka wao kwakua wao ndio walio kataa katiba ya Warioba. Ila siyo sisi wana Ukawa
 
Sheria huanza kuwaathirii wale watakaokosa baada ya sheria kuanzishwa! Kikwete keshakwepa hapo kama ana mauzauza yoyote!
wakati wa kutungwa sheria huwa inaruhusiwa kuweka kipengere kitakachosomeka "Sheria hii pia itashughulika na makosa yaliyofanywa miaka 20 kabla ya kuanza kutumika kwake".
 
Tupindishe kidogo sheria tum-pin huyu jamaa wa msoga... kazingua kwakweli
 
Hili jambo kila siku nalisema na nitaendelea kulisema as long as niko hai.

Leo hii nimejitokeza kuwaomba waandishi wa habari kutumia kalama zenu kuhamasisha mijadala ya kitaifa kutaka kinga hii iondolewe.

Inasikitisha jambo hili halipewi uzito ili hali ni jambo la hatari kubwa na kibaya zaidi hata Katiba pendekezwa bado imebeba hii kinga ya raisi.

Hivi kinga ya raisi nini msingi wake?

Kinga ya raisi ni kwa faida ya nani?

Hivi raisi ni muhimu kuliko nchi?

Pasipo nchi raisi atatoka wapi?

Sometimes huwa nahisi labda vyombo vya habari, wamiliki wake pamoja na waandishi wenyewe, huenda wamejenga hofu/nidhamu ya woga juu ya kuwa na vipindi au mijadala juu ya jambo hili katika vyombo vyao vya habari.

CC: Pasco , Manyerere Jackton , Bulembo wa Star tv,Masako wa ITV,Albert Kilala wa Channel 10 na wengineo wengi.
 
Last edited by a moderator:
Hilo swala la kisheria ulitakiwa umpelekee mbunge wako apeleke hoja bungeni
Sheria hiyo iliwekwa ili kuzuia raisi asiwe kutwa anashinda mahakamani kujibu makesi badala ya kufanya kazi za uraisi.Fikiria ana kesi bukoba,songea,kigoma,dodoma,arusha zote anatakiwa ahudhurie kazi atafanya lini
 
Hilo swala la kisheria ulitakiwa umpelekee mbunge wako apeleke hoja bungeni
Sheria hiyo iliwekwa ili kuzuia raisi asiwe kutwa anashinda mahakamani kujibu makesi badala ya kufanya kazi za uraisi.Fikiria ana kesi bukoba,songea,kigoma,dodoma,arusha zote anatakiwa ahudhurie kazi atafanya lini
Ndio maana hatuendelei!!
 
Ndio maana hatuendelei!!

Jisemee nafsi yako kuwa ndio maana hujaendelei. Hujatumwa na mtu mwingine umsemee.Au kuna kikao kilikaa kukuchagua uwasemee? Kilikaa wapi na nguvu ya kukaa kilitoa wapi.
 
Jisemee nafsi yako kuwa ndio maana hujaendelei. Hujatumwa na mtu mwingine umsemee.Au kuna kikao kilikaa kukuchagua uwasemee? Kilikaa wapi na nguvu ya kukaa kilitoa wapi.

Madai ya katiba mpya yalianzia Bungeni?Wanaposema vyombo vya habari ni muhimili wa nne wa dola unaelewaje?
 
Hili jambo kila siku nalisema na nitaendelea kulisema as long as niko hai.

Leo hii nimejitokeza kuwaomba waandishi wa habari kutumia kalama zenu kuhamasisha mijadala ya kitaifa kutaka kinga hii iondolewe.

Inasikitisha jambo hili halipewi uzito ili hali ni jambo la hatari kubwa na kibaya zaidi hata Katiba pendekezwa bado imebeba hii kinga ya raisi.

Hivi kinga ya raisi nini msingi wake?

Kinga ya raisi ni kwa faida ya nani?

Hivi raisi ni muhimu kuliko nchi?

Pasipo nchi raisi atatoka wapi?

Sometimes huwa nahisi labda vyombo vya habari, wamiliki wake pamoja na waandishi wenyewe, huenda wamejenga hofu/nidhamu ya woga juu ya kuwa na vipindi au mijadala juu ya jambo hili katika vyombo vyao vya habari.

CC: Pasco , Manyerere Jackton


Kinga ya Rais ina maana sana kama Rais ni mwadirifu, kwaani Rais anafanya maamzi mengi makubwa kwa niaba na maslahi ya taifa, mfano kipindi cha Mwl Nyerere alifanya maamzi makubwa ambayo baadae angweza kushtakiwa, alibinafisisha taaisis nyingi za kidini zikawa shule za umma, nyumba nyingi zikawa mali ya umaa, viwanda na makampuni mengi ya wazungu yakawa mali umma.

Kuna matajiri waling'ang'ania ardhi yz umma. lkn Rais alibadili matumizi ya ardhi kwa manufaa ya umma km asingekuwa na kinga angweza kufikishwa mahakamani.

na nk. Nitarudi.
 
Magufuli kasema katika kutumbua majipu hakuna jiwe litaachwa bila kupinduliwa. Safi sana kama ni kweli, lakini bado kuna mahali atakwama tu napo ni pale penye sheria ya kinga ya marais wawapo mafarakani na waondokapo.Hicho kimekuwa kichaka kikubwa sana cha madhambi mengi maana hapo kuna wanaokosa lakini mwamvuli huo unawalinda.

Ni kama vile sheria hiyo imetoka kwa MUNGU kuwa ukishapata msamaha wake ni nani wa kuhoji tena? Nchi nyingi zimesha ibadili sheria hiyo na kubakiza vipengele vile vinavyohusu makosa atendayo kwa manufaa ya usalama wa nchi pekee kwanini sisi hatubadiliki?

Magu amekuwa akisema tumuombee kwa Mungu, nadhani Mungu atasikia sala zetu kama nayeye mwenyewe atakuwa na dhamira safi kwa kubadili sheria ile ili hata yeye akigeuka awe nguzo ya chumvi.

Huwezi mwambia Mungu " tusamehe dhambi zetu kama tunavyo wasamehe wanaotukosea" na ukategemea msamaha wake wakati umemtapeli kwani wewe hujasamehe.Hata tukimuomba Mungu amsaidie JPM afanye kazi kwa haki wakati haki nyingine kaikalia hataki kuirekebisha kwani itamgusa mwenyewe maombi hayo ni kazi bure.

Aruhusu mchakato wa kubadili vipengele vya sheria
 
Wewe ukipewa urais leo unaweza kuwa na jeuri ya kufanya hicho unachotaka yeye kama rais akifanye?. Mantiki ya kuondoa kinga ya rais inaeleweka.

Lakini jaribu katika hisia zako, wewe kugeuka kuwa rais wa awamu ya tano, halafu ujiridhishe ni jinsi gani hicho unachokiongea kilivyo na ugumu wa kutekelezeka. Yaani kila rais atakayekuwa anaingia madarakani itabidi afanye kazi kwa presha kubwa sana.

Hao wanaomzunguka wawe na haki ya kuishi kwa amani bila ya presha halafu yeye pekee ndio awe mtu wa kutakiwa kuishi kama malaika. Wazungu waliotutawala waliweza kutekeleza hayo uliyoyaandika baada ya miaka mingi kupita.

Sio kitu rahisi kutekelezeka kwetu sisi Tanzania. Kenya walibadili katiba lakini mpaka kesho rushwa inawatesa.
 
Kwa kuwa Majipu yamekuwa mengi sana bandarini, sekta ya madini, utumishi, usafirishaji, ujenzi. Rais Magufuli akaamua kuweka kinga za Marais wawili zijadiliwe au kuondolewa na Bunge. Unahisi wabunge wa chama cha CCM watamuunga mkono?

Mind you nao pia wengi walishiriki deal chafu kama ile ya polisi billion 37 inamhusisha mtoto wa mkuu wa majipu?

Tujadili kizalendo sio kujivika uzalendo kama CCM huku unajipu wilaya umejimilikisha tenda zote Mkurugenzi kawa kama mfanyakazi wa familia yako.
 
Each person should face justice kama mtume Noah alipojaribu kumtetea mtoto wake kwa Mwenyezi Mungu Kwasababu ya maasi yake dhidi ya Allah
Mwenyezi Mungu alikataa. How many poor Tanzanian died for lack of medicine while few people steal billions. All thieves after being convicted in court of justice whatsoever is he must go to the jail. And hereafter they will face final court of Allah.
 
Hicho kitu hata yeye binafsi hawezi Fanya!! Kwani Majipu ya sasa ni halisia kwa maana ya majipu au anaweka timu yake?
 
Ili kuleta uwajibikaji kuanzia Ikulu mpaka ofisi ya serikali mtaa, nawashauri wabunge wa CCM na wale wa UKAWA kuungana pamoja na kuifutilia mbali kinga ya Raisi.

Marekebisho hayo pia yaruhusu hata maraisi waliostaafu huku wakiwa na hii kinga nao waweze kushitakiwa iwapo kutakuwa na tuhuma zinazowahusu na zinazostahili wao kufikishwa mahakamani.

Ni matumaini yangu kuwa Magufli atakuwa wa kwanza kuunga mkono hoja/hatua hii kama kweli anaamini katika usawa na anataka kuridisha nidhamu serikalini.

Tujifunze kutoka Afrika kusini kwani inawezekana watu aina ya Zuma waliwahi ishi pale magogoni au wakaja kuishi siku zijazo.

NB:Nimeleta habari kuunga mkono wazo la mwandishi,Prudence Karugendo katika makala yae katika gazeti la Mwanahalisi la leo iliyoko katika ukurasa wa 14 wa gazeti hilo.Makala hiyo mwandishi ameipa kichwa cha habari kinachosomeka: "JPM atumbue kinga ya maraisi wastaafu."

Tofauti na alivyopendekeza mwandishi Karugendo,mimi nimeona ni vizuri hoja hii ianzie Bungeni moja kwa moja badala ya kusubri serikali ndio ipeleke hoja hiyo Bungeni ili kumtomjenga raisi uadui unaoweza kujitokeza baina yake na watangulizi wake.

"KILA MTU ABEBE MZIGO WAKE."
 
Back
Top Bottom