Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kiondolewe ili Kikwete ashitakiwe kwa kuhujumu uchumi wa nchi.
wakati wa kutungwa sheria huwa inaruhusiwa kuweka kipengere kitakachosomeka "Sheria hii pia itashughulika na makosa yaliyofanywa miaka 20 kabla ya kuanza kutumika kwake".Sheria huanza kuwaathirii wale watakaokosa baada ya sheria kuanzishwa! Kikwete keshakwepa hapo kama ana mauzauza yoyote!
Ndio maana hatuendelei!!Hilo swala la kisheria ulitakiwa umpelekee mbunge wako apeleke hoja bungeni
Sheria hiyo iliwekwa ili kuzuia raisi asiwe kutwa anashinda mahakamani kujibu makesi badala ya kufanya kazi za uraisi.Fikiria ana kesi bukoba,songea,kigoma,dodoma,arusha zote anatakiwa ahudhurie kazi atafanya lini
Ndio maana hatuendelei!!
Jisemee nafsi yako kuwa ndio maana hujaendelei. Hujatumwa na mtu mwingine umsemee.Au kuna kikao kilikaa kukuchagua uwasemee? Kilikaa wapi na nguvu ya kukaa kilitoa wapi.
Hili jambo kila siku nalisema na nitaendelea kulisema as long as niko hai.
Leo hii nimejitokeza kuwaomba waandishi wa habari kutumia kalama zenu kuhamasisha mijadala ya kitaifa kutaka kinga hii iondolewe.
Inasikitisha jambo hili halipewi uzito ili hali ni jambo la hatari kubwa na kibaya zaidi hata Katiba pendekezwa bado imebeba hii kinga ya raisi.
Hivi kinga ya raisi nini msingi wake?
Kinga ya raisi ni kwa faida ya nani?
Hivi raisi ni muhimu kuliko nchi?
Pasipo nchi raisi atatoka wapi?
Sometimes huwa nahisi labda vyombo vya habari, wamiliki wake pamoja na waandishi wenyewe, huenda wamejenga hofu/nidhamu ya woga juu ya kuwa na vipindi au mijadala juu ya jambo hili katika vyombo vyao vya habari.
CC: Pasco , Manyerere Jackton
Madai ya katiba mpya yalianzia Bungeni?Wanaposema vyombo vya habari ni muhimili wa nne wa dola unaelewaje?