Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Ndugai amesema hayo leo (Jumanne) bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali kusema haiwezekani mawaziri na watendaji wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya Rais.
----
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewakumbusha wabunge wa upinzani wanaotaka marais wastaafu washtakiwe kuhusu sakata la mchanga wa madini, wakumbuke wanao mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao watahusika pia.

"Haiwezekani mzee wangu (Andrew) Chenge na (Nazir) Karamagi walipitisha mikataba hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu. Kinga ya Rais kushtakiwa iondolewe ili wahojiwe," amesema Lijualikali.

Baada ya hoja hiyo ya Lijualikali inayofanana na ya Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Ndugai aliwakumbusha juu ya mawaziri wastaafu walionao kwenye chama chao.

"Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena," amesemaNdugai.

Chanzo: Mwananchi
Ndugai ni mthenge sana,kama hao mawaziri wanajinai waliyoifanya nao washitakiwe,hofu ya Ndubwanga ni nini?
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewakumbusha wabunge wa upinzani wanaotaka marais wastaafu washtakiwe kuhusu sakata la mchanga wa madini, wakumbuke wanao mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao watahusika pia

Huyu naye hamnazo kabisa, kwahiyo swala ni kuogopa kuwashitaki mawaziri wakuu wawili na siyo kutafuta haki waliyopunjwa watanzania
 
Baada ya hoja hiyo ya Lijualikali inayofanana na ya Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Ndugai aliwakumbusha juu ya mawaziri wastaafu walionao kwenye chama chao.

Kwahiyo Ndungai yupo kwa maslahi ya hao mawaziri wakuu/huruma kwa upinzani zaidi au wapiga kura
 
Msaada hv kuna sheria yoyote ya kumshtak rais na wazir wke kama hipo naombeni vifungu
 
Nina amini tunafanyiwa mazingaombwe kama mazingaombwe mengine. Siasa katika ubora wake, Katika masakata kama haya huu si mwanzo bali kinacho tafutwa hapa ni mwisho wake ktk kucheza na akili za watz. Hivi utanzishaje sakata kama hili hari ukijua rais mstaafu haguswi? Wakati huyohuyo rais ndo jicho, kichwa na roho ya nchi na yote yamefanyika chini yake? Labda wana sheria watwambie majukumu na mipaka ya madaraka ya rais. Kweli leo mtwambie ACCACIA haikusajiriwa ila ilikuwa inalipa kodi si maajabu haya? Kama ni swala la mda basi tuseme tumefika mwisho na hatutetei maslai ya rais wala waziri wala katibu, kama ni utashi basi sheria zifumuliwe kwa dharula nakutengenezwa zenye meno ili ziume kote. Leo umpe Ndugai akafumue sheria na Chenge ndo mwenyekiti unadhani watakuja na nini? Rais wangu JPM hapa masikio ya Watz yanasubiri matokeo ya hili lililoanzishwa ili wajue ama kweli ni maslai yao au ni yaleyale maigizo? Ushauri swala kinga ya raisi ifike sehemu tuseme na lenyewe liondolewe na kama kuna haja ya kuendelea nalo iwe kwa viongozi wote wastaafu ili tuache kusingiziana.
 
Poa tu kila anayehusika Abebe msalaba wake Kama mbwai na iwe mbwai hakuna!!
 
Ndugai amesema hayo leo (Jumanne) bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali kusema haiwezekani mawaziri na watendaji wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya Rais.
----
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewakumbusha wabunge wa upinzani wanaotaka marais wastaafu washtakiwe kuhusu sakata la mchanga wa madini, wakumbuke wanao mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao watahusika pia.

Ndugai amesema hayo leo (Jumanne) bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali kusema haiwezekani mawaziri na watendaji wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya Rais.

"Haiwezekani mzee wangu (Andrew) Chenge na (Nazir) Karamagi walipitisha mikataba hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu. Kinga ya Rais kushtakiwa iondolewe ili wahojiwe," amesema Lijualikali.

Baada ya hoja hiyo ya Lijualikali inayofanana na ya Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Ndugai aliwakumbusha juu ya mawaziri wastaafu walionao kwenye chama chao.

"Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena," amesemaNdugai.

Chanzo: Mwananchi
Mbona hamtaki Sumaye na Lowasa washitakiwe?
 
Awe CHADEMA awe CCM awe CUF awe ACT awe CHAUMA awe JAHAZI asilia nk shitaki tu mkitaka hata tuje wananchi tuwatandike viboko tuko tayari bila kutazama zura zai wala vyama vyao we ndugai vp 🙂
 
Tuna lispika la radio ,sio spika wa Bunge.hivi kweli kayasema haya au kalishwa maneno,Kama ni kweli basi hatuna spika,tuna kada wa chama alie jivisha ngozi ya speaker
 
Spika ana mawazo ya kijinga kabisa. Sasa kama marais wastaafu wakishtakiwa itazuia nini hao mawaziri wakuu wastaafu kushtakiwa kama nao walihusika kwa namna moja au nyingine kutuingiza katika mikataba ya kijinga? Kwa hiyo wanaogopa kuwaondolea kinga hao wastaafu kwaajili ya mawaziri wakuu wastaafu??!!! Mambo mengine mtu mzima tena kiongozi haifai kuyasema wakati huu wa machungu
 
Waliohusika wote washtakiwe wawe wamehama ccm kwenda chama kingine hata wakiwa wamejiuzulu nafasi ktk chama cha siasa, washtakiwe maana now karamagi sidhani hata kama ni mwana ccm tena wote wafikishwe mbele ya pilato, tunajenga Tanzania hatjengi chama chochote cha siasa.
 
Umeona sasa,ccm ni ileile.

Tume huru idaiwe mapema ccm itoke vinginevyo watanzania mtapata tabu sana.
 
Mkuu huko kwenye upande wa ccm huko siko wala sijawahi kuwepo. Naiongelea cdm kwani ndio niliyoipigania na kuijua. Hiyo ilikuwa na kupata ushawishi na nguvu bila kuwepo Lowassa au Sumaye. Leo inatia simanzi kuona haiba na nguvu ya chama kupotea kutokana uwepo wa hao jamaa ambao hawajawahi kuwa na mchango wowote.
Watu kutoka chama kingine kwenda chama kingine kwangu mimi sioni baya,ila kamauwajibishaji utaanza na Akina mkapa na kikwete je lowasa apone kisa kaenda chadema?chadems sio kichaka cha kujifichia waalifu.nenomoja ni ivi kuwajibishwa wote waliousika na Ndugaianausika.
 
Hikma ya kinga ya marais wastaafu naitafakari bado sijaona mapungufu yake. Ni hikma kubwa sana, mtu akiwa Rais wa Tanzania wa aina hii ya Tanzania tuliyo nayo sasa kumtikisa ni kulitikisa taifa zima, kama hutaki una acha, hata hivyo Rais mara nyingi ana shauriwa na wataalamu mbalimbali, kwa mfano wataalamu wa sheria. Sasa kama Rais kashauriwa na mwanasheria akamuingiza chaka yeye afanye je?

Kwani mfano wanasheria walio andaa hii mikataba wote ni marehemu? Mpaka tufikie kutafuta Marais wastaafu ambao wana kinga tayari na walishauriwa tu.

Na washawasha!
Na hao washauri waunganishwe kwenye kesi tumechoka
 
Back
Top Bottom