Kinga ya bunge dhidi ya mh:Pinda

Kinga ya bunge dhidi ya mh:Pinda

What you have noted is absolute true(in eye of the law).
Mr.Pinda is in breach of constitutional provisions( rule of law) of the Constitution of the United Republic of Tanzania,1977(as amended time to time). Being the case then according to constitutional principles; the constitution is the mother law.All laws in the country must be in-conformity to the constitution of that country. It should be noted further that, in a situation where any law(Acts,Rules,Regulations,Orders) is in conflict with the constitutional provision, then automatically the constitutional provision prevails. In this case, the constitutional provision is on rule of law by all colors must prevail over the provisions of immunity of the parliamentarians when in parliament, as provided in that particular act.

WHEREFORE the case against Mr.Pinda sustains
.

Hapo hakimbii mtu!
i have liked your post simply because of that statement in red there.
 
wanaojiita wanaharakati wa LHRC ni makada wa chadema niliwaona kwenye ITV ni wachagga, je unategemea watatumia weledi kujua kama mbunge akisema bungeni anashtakiwa au maamuzi yake ataongozwa ubavicha?

itakuwa umenusa unga wa idd azan ww
 
Wanaharakati wanaonekana kuweweseka na kauli ya Waziri mkuu kwa kuwa wao ni washawishi wakubwa kwa watu kuandamana, na kwa kauli ya waziri mkuu wanajiona wao nao watakuwa wahanga wa kauli hiyo, Hivi hawajui au wamesahau kuwa mbunge hatashitakiwa kwa kauli yoyote aliyoitoa bungeni. Pinda aliongelea bungeni, mimi naona wanatakiwa waombe muongozo wa spika kwa kutumia wabunge na sio kwenda mahakamani, hapa itakula kwao.

Kwahiyo hata akiua ndani ya bunge harusiwi kushitakiwa? Jitambue ndugu pigania nchi yako.
 
wanaojiita wanaharakati wa LHRC ni makada wa chadema niliwaona kwenye ITV ni wachagga, je unategemea watatumia weledi kujua kama mbunge akisema bungeni anashtakiwa au maamuzi yake ataongozwa ubavicha?
Wewe msukule yaelekea una mzia na wachaga. Utakonda sana na akili zako rojo rojo za kushikiwa hapo Lumumba.
 
Ndungai namshangaa kwa kuwashangaa wanasheria eti hawajui sheria
kasahau every rule has an exception.
kauli ya Pinda imevunja katiba na imekiuka haki za binadamu
The court will deliver a ruling on whether hiyo kinga anaaply kwake
kulingana na tamko lake..
nawasihi wanasheria waendelee na mchakato wao wa kufungua kesi husika.
 
Katiba ndio sheria mama,sheria nyingine zooote zinatokana na katiba,kwa mantiki hiyo basi kama sheria inakinzana na katiba kwa vyovyote vile katiba itasimama juu ya hiyo sheria.

Labda ukiwaambia wewe hao wanaotetea kwamba ana kinga labda watakusikia, vinginevyo inabidi warudi darasani au wakalipie tuition ya somo la sheria ili wajue kwamba sheria zote hutokana na matakwa ya wanacchi (katiba mama).

sijui ni lini wananchi walimruhusu mtu yeyote anayefanya kazi kwa masharti yao (Pinda na serikali yake) awe juu yao kisheria na kuwakandamiza bila wao kumchukulia hatua. Ni mambo ya ajabu sana kwa wale wanaotetea kwamba ana kinga...

Kinga hailidi uhalifu, Kinga haichochei mtu , watu au waandamanaji kupigwa, hata maandamo yenye ni haki ya binadamu - rejea right to self assembly...

Yaani mtu nimchague mimi halafu aje kunitafutia majambazi ya kunipiga na kunikansdamiza kwa minajili gani? lazima nimwadabishe tu kwa vyovoye vile , iwe mahakamani au hata msituni... iko siku hata Pinda mwenyewe ataonja joto ya jiwe...na huu ndio mwanzo wenyewe kwa kumuonjesha joyo hiyo...
 
Kusema raia wapigwe tuu ni kuvunja katiba ya nchi ambayo ni sheria mama. Kanuni zinasema kinga ya Bunge inapatikana pale Mbunge atakaposema chochote bila kuathiri masharti mengine ya katiba. Kwani Mbunge akizungumzia jambo la kuhamasisha uhaini Bungeni ataendelea kupata kinga ya Bunge? Hapana. Hivyo hivyo kwa kauli ya Pinda iliyovunja katiba kama waziri mkuu anastahili kushtakiwa.
Hata kama kesi hiyo atashinda,lakini ujumbe utawafikia watawala kuwa kauli zao ni muhimu kuzitathimini kabla ya kuzitoa kwa huwa zinachukuliwa kwa uZito wa kipekee. Tumesikia huko Mtwara watu wamepigwa na kuambiwa tunatekeleza agizo la PM. Madhara ndiyo hayo yameanza na yasipochukuliwa hatua kama hiyo ya wanasheria basi kipigo kitaendelea maana itakuwa kama ni sheria imepita ya kipigo,taifa la aina gani hilo?
 
Munishi aliimba dawa ya ndoa ni msamaha tu.....Naye apigwe tu...... si aombe radhi kwa watanzania yaishe?" tell my people that i love them and they must continue the strungle,my blood will nourish the tree that will bear the fruit of freedom.aluta continue".....Solomom Mahlanga.
 
Wanaharakati wanaonekana kuweweseka na kauli ya Waziri mkuu kwa kuwa wao ni washawishi wakubwa kwa watu kuandamana, na kwa kauli ya waziri mkuu wanajiona wao nao watakuwa wahanga wa kauli hiyo, Hivi hawajui au wamesahau kuwa mbunge hatashitakiwa kwa kauli yoyote aliyoitoa bungeni. Pinda aliongelea bungeni, mimi naona wanatakiwa waombe muongozo wa spika kwa kutumia wabunge na sio kwenda mahakamani, hapa itakula kwao.

Soma hii hapa toka Tanzania Daima 31/07/2013 inaweza kukusaidia

UAMUZI wa Kituo cha Haki za Binadamu wa kumshitaki mahakamani Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kauli yake ya kuagiza wananchi wapigwe, imelitikisa taifa kiasi cha kuisukuma ofisi ya Bunge kumkingia kifua.
Huku idadi kubwa ya taasisi na wanasheria mashuhuri wakiungana na kituo hicho katika kumfungulia Waziri Mkuu Pinda mashitaka yanayotarajiwa kufunguliwa kesho jijini Dar es Salaam, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema jana kuwa hawezi kushitakiwa popote kutokana na kuwa na kinga ya kibunge inayomlinda.
Katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano, Ndugai alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge, na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama, au mahali pengine nje ya Bunge.
“Ninashangaa sana wanasheria hawa, tena ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, wameacha kabisa kufuata sheria, sasa naona wanafanya siasa, wanatafuta umaarufu tu na mahakama haitaweza kusikiliza kesi hiyo,” alisema Ndugai.
Hata hivyo, utetezi huo wa Ndugai, umepingwa na wanasheria wengi waliohojiwa wakisema kuwa tamko la Pinda linavuka mipaka ya kinga za kibunge, na hivyo anaweza kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zinazomkabili.
Mkurugenzi wa asasi ya kiraia ya kufuatilia mwenendo wa Bunge, Marcus Albany pamoja na kukipongeza Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa hatua hiyo, alisema tamko la Waziri Mkuu Pinda ni la hatari na lenye madhara makubwa kwa usalama wa nchi.
Albany alisema waziri mkuu anapaswa kuongezewa mashitaka kwa sababu kauli yake inagusa kosa jingine kwa kulitangazia taifa kuwa serikali iliyoko madarakani imechoka.
“Waziri Mkuu hakusema piga tu peke yake, bali alisema pia serikali imechoka, hili nalo ni kosa jingine kwa Waziri Mkuu kulitangazia Bunge kuwa serikali imechoka halafu hataki kujiuzulu, hivyo ashitakiwe tu,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema wataungana nao kituo hicho katika mashitaka hayo kwa sababu yana uzito mkubwa na athari kwa taifa ikiwa hakutachukuliwa hatua dhidi ya kiongozi huyo kwa sababu yanaweza kuleta maafa makubwa.
Mwanasheria wa kituo hicho, Harold Sungusia alisema utetezi wa Ndugai umejaa siasa zaidi na ametafsiri kimakosa kifungu hicho cha katiba kinachompa kinga mbunge.
“Pinda hataepuka kikombe hiki, ni lazima wafike mahakamani ili mahakama ndiyo iseme kama Pinda alikosea au la.
“Sisi tulijua kuwa watajiegemeza katika kipengele hicho cha kinga ya Bunge, lakini tunaenda mahakamani kuiomba mahakama ituambie kama kinga dhidi ya Bunge inamlinda mtu anayevunja katiba, tunataka mahakama ituambie kama mtu anayesema watu wapigwe ni sahihi au la,” alisema Sungusia.
Alisema katiba ndiyo sheria mama ambayo Waziri Mkuu Pinda aliivunja kwa tamko lake la hatari na linaloweza kusababisha vurugu na umwagaji wa damu. Hivyo hawatarudi nyuma kumfikisha mahakamani.
Aliongeza kwamba kipengele cha katiba alichoshikilia Ndugai bado kinasisitiza kuwa bila kuathiri katiba, na Waziri Mkuu Pinda hakuvunja kanuni za Bunge tu, alivunja katiba aliyoapa kuilinda, na hivyo kipengele ambacho Bunge kinang’ang’ania kipo kinyume cha katiba, na katiba inasisitiza bila kuathiri.
“Chukulia kuwa ikatokea siku moja mbunge ama kiongozi mkubwa kabisa akasema wanawake wote wabakwe, asichukuliwe hatua kwa kuwa alisemea bungeni?
“Ikitokea waziri akaamuru watu wauawe asishitakiwe kwa kigezo kuwa alisemea bungeni? Tunataka mahakama ndio itoe tafsiri ya kifungu hicho,” alisema.
Mwanasheria mwingine maarufu ambaye jina lake linahifadhiwa kutokana na dhamana aliyonayo serikalini, alisema kuwa sheria ya haki na wajibu inayotekelezwa na mahakama ya mwaka 1994, inatoa mwanya kwa Waziri Mkuu kushitakiwa hata kwa alichokisema bungeni.
“Hii ni kwa kutumia madaraka ya Mahakama Kuu ya kutengua uamuzi unaolalamikiwa, ili mamlaka husika itoe amri nini kifanyike au mahakama ilazimishe jambo fulani lisifanyike (Prerogative of certiorari, mandamus et Prohibimus),” alisema mwanasheria huyo.
Alisema Pinda alikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 13(2) inayosema: “Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka sharti lolote ambalo ni la kibaguzi ama wa dhahiri au taathira yake.
“Kifungu cha nne cha ibara hiyo hiyo kinasema ‘ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi’. Pinda alitoa kauli hiyo akiwa anatekeleza kazi yake kama kiongozi wa serikali bungeni.
“Katiba Ibara ya 13 (6) (e) inaonya kuwa ‘ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha’. Pia Ibara ya 16 ya Katiba inasema ‘kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi ya nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na pia heshima na hifadhi ya maskani na mawasiliano yake binafsi’,” alisema.
Akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, bungeni Dodoma aliyetaka kujua serikali inavyoshughulikia tuhuma za vyombo vya dola kutuhumiwa kuwapiga wananchi kama ilivyotokea Mtwara na kwingineko, Pinda alijibu:
“Ni lile lile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu. Hakuna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndiye jeuri zaidi, watakupiga tu. Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine, maana tumechoka.”
Tamko hilo lililoshangiliwa na wabunge karibu wote wa CCM huku wale wa upinzani, wakitikisa vichwa vyao kwa masikitiko lilizua malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania wa kada mbalimbali, na wengine kwenda mbali zaidi wakimtaka kiongozi huyo kujiuzulu.
Ikiwa atafikishwa mahakamani, itakuwa tukio la kwanza katika historia ya Tanzania kwa Waziri Mkuu kushitakiwa kutokana na matamshi yake bungeni, ama akiwa nje ya Bunge.
 
Kwa hiyo mtu hata kama atawatusi Watz kama alivyofanya pinda bado atahdesabiwa kuwa anakinga? Kazi kwelikweli!
Wanaharakati wanaonekana kuweweseka na kauli ya Waziri mkuu kwa kuwa wao ni washawishi wakubwa kwa watu kuandamana, na kwa kauli ya waziri mkuu wanajiona wao nao watakuwa wahanga wa kauli hiyo, Hivi hawajui au wamesahau kuwa mbunge hatashitakiwa kwa kauli yoyote aliyoitoa bungeni. Pinda aliongelea bungeni, mimi naona wanatakiwa waombe muongozo wa spika kwa kutumia wabunge na sio kwenda mahakamani, hapa itakula kwao.
 
wanaharakati wanaonekana kuweweseka na kauli ya waziri mkuu kwa kuwa wao ni washawishi wakubwa kwa watu kuandamana, na kwa kauli ya waziri mkuu wanajiona wao nao watakuwa wahanga wa kauli hiyo, hivi hawajui au wamesahau kuwa mbunge hatashitakiwa kwa kauli yoyote aliyoitoa bungeni. Pinda aliongelea bungeni, mimi naona wanatakiwa waombe muongozo wa spika kwa kutumia wabunge na sio kwenda mahakamani, hapa itakula kwao.
unataka kutetea nini hapa ,huku uraiani hakuna mwongozo wa spika ni sheria hadi mh.pinda asipindishe kauli zake zenye utata kwa taifa .
 
wanaojiita wanaharakati wa LHRC ni makada wa chadema niliwaona kwenye ITV ni wachagga, je unategemea watatumia weledi kujua kama mbunge akisema bungeni anashtakiwa au maamuzi yake ataongozwa ubavicha?

wewe toa udini fa.la wewe,jibu hoja kwa akili timamu ,hv nyie watz mkoje?mbona ni mambo ya ku2mia akili ndogo tu,huwez kutamka maneno ya hovyo bungeni kisa wewe ni waziri mkuu,
 
Kinga ya mbunge ni pale anapoongea jambo akiwa ndani ya bunge, na pinda ni mbunge na ameongelea ndani ya bunge.Kinga ipo palepale.

Hakuna kinga ya kipumbavu kiasi hicho. Kwamba Waziri mkuu na wabunge wanaruhusiwa kuvunja katiba ya nchi yetu wakiwa bungeni? Otherwise unadhani ni nini kitegemewe pale kesho mbunge atakapouliza kuhusu kinadada wanaovaa ovyo? Kwamba waziri asemeje? wabakwe tu?

Tuwe tunafikiria impact ya maneno yetu. Hakuna kinga ya mtu anayevunja Katiba ya Jamhuri hata akaongelee kuzimu au Mbinguni. Wala siyo sababu kwa PM kuivunja wakati aliapa kuilinda tena hadharani.
 
Kinga ya mbunge ni pale anapoongea jambo akiwa ndani ya bunge, na pinda ni mbunge na ameongelea ndani ya bunge.Kinga ipo palepale.

mkuu khairun tufanye kama vile mimi mbunge na nitoe kauli kuwa "wanawake wote wabakwe" nikiwa ndani ya bunge. je nilindwe kwa sbb nimetamka maneno nikiwa bungeni? kumbuka katiba ya nchi ndio iliyounda bunge!
 
pinda ama awajibike mwenyewe ama awajibishwe, he has only two options there.
 
Back
Top Bottom