Mbunge wa Ikungi Magharibi, Elibariki Kingu akichangia hotuba ya Wizara ya Mambo ya Nje leo Mei 26, 2026, Bungeni Dodoma
"Ni Rais huyu Daktari Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani jambo la kwanza alilolifanya, Rais wetu—wabunge naomba tuwe na kumbukumbu. Ninaomba tuweke kumbukumbu sawa duniani ili kusudi tusije tukaruhusu heshima ya taifa letu, heshima ya Rais wetu ikachezewa na mataifa baadhi kwa maslahi ambayo yanaweza yakafanya Rais wetu na nchi yetu na viongozi wetu wakawa ni wanyonge.
Mheshimiwa Spika, nataka nikukumbushe katika kulinda uhuru wa kidemokrasia, katika mambo ya nje, Rais Samia alipoingia madarakani akiwa Rais, ndiye Rais wa kwanza alikwenda kuwatembelea hata wapinzani waliokuwa wametoroka na kukimbia taifa hili.
Mheshimiwa Spika, Rais Samia alipoingia madarakani, kuna baadhi ya wanasiasa hawakuwa hata na pasipoti. Rais Samia alitoa maelekezo wakapewa mradi hati za kidiplomasia kuwa huru kuzunguka duniani.
Mheshimiwa Spika, Rais Samia alipoingia madarakani kwa kulinda uhuru wa vyama vya siasa Tanzania, alifungua, aliondoa katazo la mikutano yote ya hadhara iliyokuwa imekabili vyama vya kisiasa Tanzania. Vyama vyote vikapewa uhuru wa kufanya mikutano ya siasa."