Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Sielewi kwanini wapinzani wamekuwa waongo hivi, kila uchaguzi wanadai wameibiwa kura kwa sababu ya kukosa tume huru ya uchaguzi, lakini sijawahi kuona juhudi zozote zinazofanya kuhakikisha nchi imepata tume huru ya uchaguzi.

Pia sijui kwanini wanakubali kuingia kwenye uchaguzi huku wakijua kuwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Wapinzani mtadai lini tume huru ya uchaguzi?
Wewe ndiyo tatizo sera zako mbofu. Tume iliyopo ni huru. Tatizo ni wewe hupati kura za kutosha.
 
Sijakukatalia kuwa mfumo hauko sawa ki ushindani sasa wapinzani wameridhika nao ndio maana wanakubali kuingia kwenye uchaguzi kila wakati la sivyo tuseme hatuna upinzani wa kweli.
Njia sahihi za kutafuta jambo hilo kwa hapa Jf ni UCHOCHEZI !!.
 
Kwa sasa wapinzani kazi yao kubwa ni kumtoa Lissu na Lema kila siku mahabusu!
Dada nakuhakikishia 2020 Tume itakuwa hii hii ya Lubuva sababu upinzani TZ umekufa!Sana sana watu wakianza kudai katiba mpya Lowassa ataibuka na kusema hataki siasa za kiuharakati
CCM imeisha shinda easily 2020

Kaka Malafyale nafurahia kwa mchango wako ila tutatofautiana sana kwa kudhani kuwa upinzani kazi yao ni kumtoa Lissu na Lema mahabusu...kama utaweza kufikiri mbali kwa maneno mengine tunaita an Eagle vision utagundua kwamba upinzani unaimarishwa sana na utendaji wa serikali ya awamu ya tano kwa kutumia methodology ya ubabe au Ruling rather than leading...hali hii utengeneza upinzani mkubwa ndani ya chama husika na kwa wananchi. sasa kama kuna mtu anayefikiria ccm inaweza kushinda kwa urahisi 2020 atakuja kushangaa sana.. ni heri kuwa na visible opposition kuliko invisible opposition.
 
Upinzani umekufa
Kama hata UKUTA umewashinda kwa vitisho uchwara wataweza kudai katiba mpya inayo kuja na mikiki mikiki ya mapambano na vyombo vya dola?
Lowassa na Sumaye wameua sana upinzani!

Kwani upinzani ni vyama au ni watu?
 
Lakini wapinzani ndio wamekuwa wakilalamika kuibiwa kura, siamini kama wangeweza kuingia kwenye uchaguzi wowote bila tume huru...tunao viongozi wa dini ambao wangeweza kusaidia ila wapinzani wa Tanzania wameshindwa kabisa kudai jambo la msingi ambalo ni tume huru ya uchaguzi
Hivi unadhani hata wapinzani wakigoma kuingia kwenye Uchaguzi mpaka iundwe tume Huru Chaje atashindwa kuitangazia ushindi CCM kama alivyofanya kwa uchaguzi wa marudio kule visiwani.

Ndio maana upinzani wanadai RASIMU YA KATIBA YA JAJI WARIOBA ndio ipitishwe ili mambo yaende vizuri kwenye nchi yetu na chaguzi zisiwe na ukakasi tena.

Haiwezekani ukamnyima bosi wako ushindi wakati unajua kabisa yeye ndiye anayekulipa mshahara .
 
Unadai vp iyo tume huru kwa mtu ambaye anakwambia katiba si kipao mbele kwake
 
Kwani upinzani ni vyama au ni watu?
Watu wanahitaji forums za kuwaunganisha na ndiyo kinacho kosekana kwa watu wanao ipinga CCM
Hawa akina Lowassa hamna kitu
Hawawezi badili kitu sababu wao ni kama CCM tu
 
Umpingea ukweli kwa sababu hata tukisema vyama vyote vya upinzani visusie uchaguzi hawa jamaa wanaweza wakaunda vya vingine ili kupata ushahidi kwa uchaguzi ulikuwa wa kidemokrasia.
Maana yangu ilikua hakuna tofauti yoyote ya vyama vya Tanzania maana wanasiasa wanapishana tu kuelekea wapi watapata nafasi ya kupiga deal. Mtu wa kweli hawezi kuishi miaka 40 akisifia chama chake kama kada mkuu halafu leo aingie upande mwingine akikandie chama ambacho yeye alikua mmoja wapo wa ukandamizaji wa demokrasia. Na huko upinzani ni yaleyale wanatafuta karata trufu itakayowasaidia na wao wakakalie kiti ili nao wale keki ya taifa
 
Unadai vp iyo tume huru kwa mtu ambaye anakwambia katiba si kipao mbele kwake
Kwasasa naungana naye katiba si kipaumbele watu warekebishwe kwanza halafu katiba ije nenda kamsikilize prof Lumumba kwanza utaelewa nini maana yake maana hapa tulipofika mahakama inatakiwa kuungana na serikali kumaliza matatizo ya rushwa ndipo mambo mengine yafuate
 
Sielewi kwanini wapinzani wamekuwa waongo hivi, kila uchaguzi wanadai wameibiwa kura kwa sababu ya kukosa tume huru ya uchaguzi, lakini sijawahi kuona juhudi zozote zinazofanya kuhakikisha nchi imepata tume huru ya uchaguzi.

Pia sijui kwanini wanakubali kuingia kwenye uchaguzi huku wakijua kuwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Wapinzani mtadai lini tume huru ya uchaguzi?
Kwa ulizo lako inaonyesha wazi wapinzani hawana haja yaushindi Wanafasi ya urais ila nidanganya Toto tu wanafanya kuaminisha watanzania kuwa wapo makini kutaka kuongoza nchi.kumbe nia yao kubwa ni ruzuku na maslahi binafsi.kama kweli wapo makini basi wasinge shiriki kwenye chaguzi zote kushinikiza kuundwa tume huru,maana hichi ndicho chombo chenyekusimamia zoezi zima la chaguzi na kutoa matokeo yake.niwazi vyama vya upinzani wanajua kuwa bila tume huru hakuna uchaguzi huru, lakini chakushangaza wamekuwa wakishiriki chaguzi miaka yote nakuishia kushindwa vibaya kwa nafasi ya uraisi.kwa akiri yakawaida tu wanajua hakuna ushindani sawa pasipo mwamuzi huru! ni mtazamo wangu kuwa hawa ni wapinzani maslahi ,ndio maana hata mazuri yanayofanywa na serikali iliyopo madarakani waliowengi wamekuwa wakipinga,
 
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya, vyama vya upinzani visahau kushinda urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Kauli ya Kingunge imekuja siku moja baada Rais John Magufuli kumteua Jaji Themistocles Kaijage kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya Jaji Damian Lubuva kufikia muda wake wa kustaafu.

Kwa muda mrefu, NEC imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kutokuwa huru kwa sababu ya uongozi wake wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, huku sheria zikikataza matokeo ya nafasi ya urais kupingwa mahakamani.

Mbali na mwenyekiti kuteuliwa na Rais, wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo ni wakurugenzi wa wilaya ambao pia huteuliwa na Rais kwa kuwa NEC haina wafanyakazi wake kote nchini.

Akizungumza katika mkutano wa kuwafariji vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushtakiwa kwa makosa yaliyohusu Uchaguzi Mkuu uliopita, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliwatia moyo vijana hao, akisema hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.

Kingunge, aliyetumia muda mrefu kueleza historia ya maisha yake katika siasa na jinsi alivyopambana katika harakati za kudai uhuru, alisema hali ya sasa ni mbaya kuliko wakati wa wakoloni wa Kiingereza ambao walikujwa wakali, kwa sababu CCM haifuati Katiba wala sheria.

“Yako mambo ambayo itabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni tume huru (ya uchaguzi). Suala hilo lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977. Tukienda hivyo sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” alisema.

Kingunge ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo ya waziri anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na mkuu wa mkoa alisema, “(Pia) Sheria inayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa. Hivi sasa sheria inasema matokeo ya uchaguzi wa Rais hayahojiwi mahakamani. Lazima hilo suala lipate jibu sasa. Kwa hiyo Katiba na sheria iseme, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kuhojiwa mahakamani. Tusipokuwa na hilo, tutakuwa na matatizo makubwa sana.”

Alisema pamoja na kwamba Chadema inapendwa na wananchi wengi na Edward Lowasa aliyegombea urais kwa tiketi chama hicho, anapendwa, bado ni vigumu kushinda kwa sababu mfumo uliopo sasa.

“Tufanye yoyote, lakini tuhakikishe, ama tunapata Katiba Mpya au vipengele hivi vya sheria vinafanyiwa marekebisho. Kwa maoni yangu, kundi hili lililo madarakani bila shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi, halitataka mabadiliko,” alisema.

Alisema enzi zao walifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitolea kwa nguvu na wengine, na yeye akiwamo, waliacha kazi za mishahara mikubwa na kujiunga na Tanu kupigania uhuru.

“Tulifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitoa mhanga. Wengi tu waliacha kazi, mtu anamaliza chuo kikuu anasema sitaki kazi anaingia Tanu kusaidia. Kwa hiyo tukawa na jeshi kubwa la vijana waliohakikisha nchi inapata uhuru,” alisema.

“Ninyi mnapambana katika mazingira magumu na wazee wenzenu walipambana katika mazingira hayo. Haikuwa rahisi. Wapo wengi walitusaliti, wengine hawakufanya lolote. Baba yangu tuligombana, nilipoacha kazi kwenda kuitumikia Tanu. Miezi sita hatukuzungumza.”

Akizungumza mkutano huo, Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwatia moyo vijana walioshtakiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, akisema bado jeshi kubwa la vijana linahitajika.

“Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Si haki kusema unakwenda mahali pengine, mwenzako amepasafisha, safisha pa kwako. Nimefurahia moyo huo. Kama alivyosema Ngombale, tunataka jeshi kubwa zaidi, watu wengi zaidi,” alisema Lowassa.
1.jpg
 
Yako mambo ambayo itabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni tume huru (ya uchaguzi). Suala hilo lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977. Tukienda hivyo sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” alisema.
 
Ili upinzani utendewe haki ni kweli kabisa yaliyonenwa na Mzee, shida inakuja ili kufikia hayo alioshauri ugumu wake unafanana na kushinda u raisi kwa mazingira ya sasa.
 
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya, vyama vya upinzani visahau kushinda urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Kauli ya Kingunge imekuja siku moja baada Rais John Magufuli kumteua Jaji Themistocles Kaijage kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya Jaji Damian Lubuva kufikia muda wake wa kustaafu.

Kwa muda mrefu, NEC imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kutokuwa huru kwa sababu ya uongozi wake wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, huku sheria zikikataza matokeo ya nafasi ya urais kupingwa mahakamani.

Mbali na mwenyekiti kuteuliwa na Rais, wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo ni wakurugenzi wa wilaya ambao pia huteuliwa na Rais kwa kuwa NEC haina wafanyakazi wake kote nchini.

Akizungumza katika mkutano wa kuwafariji vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushtakiwa kwa makosa yaliyohusu Uchaguzi Mkuu uliopita, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliwatia moyo vijana hao, akisema hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.

Kingunge, aliyetumia muda mrefu kueleza historia ya maisha yake katika siasa na jinsi alivyopambana katika harakati za kudai uhuru, alisema hali ya sasa ni mbaya kuliko wakati wa wakoloni wa Kiingereza ambao walikujwa wakali, kwa sababu CCM haifuati Katiba wala sheria.

“Yako mambo ambayo itabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni tume huru (ya uchaguzi). Suala hilo lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977. Tukienda hivyo sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” alisema.

Kingunge ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo ya waziri anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na mkuu wa mkoa alisema, “(Pia) Sheria inayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa. Hivi sasa sheria inasema matokeo ya uchaguzi wa Rais hayahojiwi mahakamani. Lazima hilo suala lipate jibu sasa. Kwa hiyo Katiba na sheria iseme, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kuhojiwa mahakamani. Tusipokuwa na hilo, tutakuwa na matatizo makubwa sana.”

Alisema pamoja na kwamba Chadema inapendwa na wananchi wengi na Edward Lowasa aliyegombea urais kwa tiketi chama hicho, anapendwa, bado ni vigumu kushinda kwa sababu mfumo uliopo sasa.

“Tufanye yoyote, lakini tuhakikishe, ama tunapata Katiba Mpya au vipengele hivi vya sheria vinafanyiwa marekebisho. Kwa maoni yangu, kundi hili lililo madarakani bila shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi, halitataka mabadiliko,” alisema.

Alisema enzi zao walifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitolea kwa nguvu na wengine, na yeye akiwamo, waliacha kazi za mishahara mikubwa na kujiunga na Tanu kupigania uhuru.

“Tulifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitoa mhanga. Wengi tu waliacha kazi, mtu anamaliza chuo kikuu anasema sitaki kazi anaingia Tanu kusaidia. Kwa hiyo tukawa na jeshi kubwa la vijana waliohakikisha nchi inapata uhuru,” alisema.

“Ninyi mnapambana katika mazingira magumu na wazee wenzenu walipambana katika mazingira hayo. Haikuwa rahisi. Wapo wengi walitusaliti, wengine hawakufanya lolote. Baba yangu tuligombana, nilipoacha kazi kwenda kuitumikia Tanu. Miezi sita hatukuzungumza.”

Akizungumza mkutano huo, Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwatia moyo vijana walioshtakiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, akisema bado jeshi kubwa la vijana linahitajika.

“Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Si haki kusema unakwenda mahali pengine, mwenzako amepasafisha, safisha pa kwako. Nimefurahia moyo huo. Kama alivyosema Ngombale, tunataka jeshi kubwa zaidi, watu wengi zaidi,” alisema Lowassa.
View attachment 449805
Bila tume huru ya uchaguzi! I will never vote again!
 
Back
Top Bottom