Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

VIVIANET

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2015
Posts
2,129
Reaction score
2,918
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya, vyama vya upinzani visahau kushinda urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Kauli ya Kingunge imekuja siku moja baada Rais John Magufuli kumteua Jaji Themistocles Kaijage kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya Jaji Damian Lubuva kufikia muda wake wa kustaafu.

Kwa muda mrefu, NEC imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kutokuwa huru kwa sababu ya uongozi wake wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, huku sheria zikikataza matokeo ya nafasi ya urais kupingwa mahakamani.

Mbali na mwenyekiti kuteuliwa na Rais, wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo ni wakurugenzi wa wilaya ambao pia huteuliwa na Rais kwa kuwa NEC haina wafanyakazi wake kote nchini.

Akizungumza katika mkutano wa kuwafariji vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushtakiwa kwa makosa yaliyohusu Uchaguzi Mkuu uliopita, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliwatia moyo vijana hao, akisema hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.

Kingunge, aliyetumia muda mrefu kueleza historia ya maisha yake katika siasa na jinsi alivyopambana katika harakati za kudai uhuru, alisema hali ya sasa ni mbaya kuliko wakati wa wakoloni wa Kiingereza ambao walikujwa wakali, kwa sababu CCM haifuati Katiba wala sheria.

“Yako mambo ambayo itabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni tume huru (ya uchaguzi). Suala hilo lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977. Tukienda hivyo sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” alisema.

Kingunge ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo ya waziri anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na mkuu wa mkoa alisema, “(Pia) Sheria inayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa. Hivi sasa sheria inasema matokeo ya uchaguzi wa Rais hayahojiwi mahakamani. Lazima hilo suala lipate jibu sasa. Kwa hiyo Katiba na sheria iseme, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kuhojiwa mahakamani. Tusipokuwa na hilo, tutakuwa na matatizo makubwa sana.”

Alisema pamoja na kwamba Chadema inapendwa na wananchi wengi na Edward Lowasa aliyegombea urais kwa tiketi chama hicho, anapendwa, bado ni vigumu kushinda kwa sababu mfumo uliopo sasa.

“Tufanye yoyote, lakini tuhakikishe, ama tunapata Katiba Mpya au vipengele hivi vya sheria vinafanyiwa marekebisho. Kwa maoni yangu, kundi hili lililo madarakani bila shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi, halitataka mabadiliko,” alisema.

Alisema enzi zao walifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitolea kwa nguvu na wengine, na yeye akiwamo, waliacha kazi za mishahara mikubwa na kujiunga na Tanu kupigania uhuru.

“Tulifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitoa mhanga. Wengi tu waliacha kazi, mtu anamaliza chuo kikuu anasema sitaki kazi anaingia Tanu kusaidia. Kwa hiyo tukawa na jeshi kubwa la vijana waliohakikisha nchi inapata uhuru,” alisema.

“Ninyi mnapambana katika mazingira magumu na wazee wenzenu walipambana katika mazingira hayo. Haikuwa rahisi. Wapo wengi walitusaliti, wengine hawakufanya lolote. Baba yangu tuligombana, nilipoacha kazi kwenda kuitumikia Tanu. Miezi sita hatukuzungumza.”

Akizungumza mkutano huo, Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwatia moyo vijana walioshtakiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, akisema bado jeshi kubwa la vijana linahitajika.

“Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Si haki kusema unakwenda mahali pengine, mwenzako amepasafisha, safisha pa kwako. Nimefurahia moyo huo. Kama alivyosema Ngombale, tunataka jeshi kubwa zaidi, watu wengi zaidi,” alisema Lowassa.
1-jpg.449805
 
Sielewi kwanini wapinzani wamekuwa waongo hivi, kila uchaguzi wanadai wameibiwa kura kwa sababu ya kukosa tume huru ya uchaguzi, lakini sijawahi kuona juhudi zozote zinazofanya kuhakikisha nchi imepata tume huru ya uchaguzi. Pia sijui kwanini wanakubali kuingia kwenye uchaguzi huku wakijuwa kuwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Wapinzani mtadai lini tume huru ya uchaguzi?

Na wewe inakuhusu
 
Wapinzani wanatakiwa wazaliwe upya. Hadi sasa ni vigumu kujua wanapinga nini na kwa mipango ipi.
woote wanahangaika mahakamani kwa kesi ziko inversely proportional na malengo yao. Kama wanakwepa majukumu yao ya msingi na kwenda kuanza kulalama.
 
Hoja yako ni nzuri sana lakini kwa kutokujua umechanganya na majungu .
 
Sielewi kwanini wapinzani wamekuwa waongo hivi, kila uchaguzi wanadai wameibiwa kura kwa sababu ya kukosa tume huru ya uchaguzi, lakini sijawahi kuona juhudi zozote zinazofanya kuhakikisha nchi imepata tume huru ya uchaguzi. Pia sijui kwanini wanakubali kuingia kwenye uchaguzi huku wakijuwa kuwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Wapinzani mtadai lini tume huru ya uchaguzi?
tuliidai kwenye rasimu ya warioba wale wahuni wa kijani wakachakachua ma kuuvuruga mchakato wote maana wanajua bila tume huru wizi wao hufanikiwa haraka
 
Hili jambo tukiwaachia wapinzani pekee yao hatuitendei haki nchi yetu. Hili ni la kila mzalendo wa taifa hili. Naifikie mahali tuwaachie wajukuu wetu nchi isiyo na figisu figisu
 
Hili jambo tukiwaachia wapinzani pekee yao hatuitendei haki nchi yetu. Hili ni la kila mzalendo wa taifa hili. Naifikie mahali tuwaachie wajukuu wetu nchi isiyo na figisu figisu

Lakini wapinzani ndio wamekuwa wakilalamika kuibiwa kura, siamini kama wangeweza kuingia kwenye uchaguzi wowote bila tume huru...tunao viongozi wa dini ambao wangeweza kusaidia ila wapinzani wa Tanzania wameshindwa kabisa kudai jambo la msingi ambalo ni tume huru ya uchaguzi
 
sasa ulitaka wafanyaje toa solution maana tumedai toka rasimu ya warioba mkachakachua sasa hivi tena mkulu kasema hana mpango na katiba mpya ok maybe tungeandamana sasa mmezuia maandamano TUFANYEJE????
 
Umesoma vizuri bandiko langu? nimeuliza lini wapinzani watadai tume huru ya uchaguzi, sijasema wataomba maana upinzani hauwezi kuomba chama tawala kikawapa bali kudai..na kudai lazima mbinu za kisiasa zitumike
mfano mdogo kama wakati wa joto la kampeni lilivyokuwa kubwa halafu ukawa wakasema bila tume huru hatutafanya uchaguzi tutaingia barabarani na kipindi chote cha kampeni kama wangekuwa wanaendelea na maandamano tu na jinsi walivyokuwa wanaungwa mkono uchaguzi usingefanyika na tume huru ingepatikana
 
Lakini wapinzani ndio wamekuwa wakilalamika kuibiwa kura, siamini kama wangeweza kuingia kwenye uchaguzi wowote bila tume huru...tunao viongozi wa dini ambao wangeweza kusaidia ila wapinzani wa Tanzania wameshindwa kabisa kudai jambo la msingi ambalo ni tume huru ya uchaguzi
Vivianet mazingira yaliyojengwa na watawala (ccm) ni mpaka njia mbadala lakini si ya kistaarabu

Tangu nchi ipoteze muelekeo ktk Katiba mpya 2014 tumepoteza wote si wapinzani pekee.
Kikwete asingeperekeshwa na ukereketwa angeweza kutupa KATIBA mpya. Lakini mwanaadamu ni dhaifu hata akiwa kiongozi kama yeye alivyokuwa.

Kuhusu kuibiwa kura ni kuwa mfumo hauko sawa ki ushindani
 
Sijakukatalia kuwa mfumo hauko sawa ki ushindani sasa wapinzani wameridhika nao ndio maana wanakubali kuingia kwenye uchaguzi kila wakati la sivyo tuseme hatuna upinzani wa kweli.
 
Sielewi kwanini wapinzani wamekuwa waongo hivi, kila uchaguzi wanadai wameibiwa kura kwa sababu ya kukosa tume huru ya uchaguzi, lakini sijawahi kuona juhudi zozote zinazofanya kuhakikisha nchi imepata tume huru ya uchaguzi. Pia sijui kwanini wanakubali kuingia kwenye uchaguzi huku wakijuwa kuwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Wapinzani mtadai lini tume huru ya uchaguzi?
Kaka usitoe povu bure mawaziri wakuu wa ccm wanaweza kudai tume huru kweli?! Haiwezekani kujichoma kisu mwenyewe hawa sio wapinzani ,niwapika matukio wakati cuf wanashughulikia tukio la p.lipumba kumeondoa uenyekiti CDM nao wanashughulikia tukio la lema mahakani,hapo tume itaijia wapi
 
Majungu yapi tena?

Kwa sasa wapinzani kazi yao kubwa ni kumtoa Lissu na Lema kila siku mahabusu!
Dada nakuhakikishia 2020 Tume itakuwa hii hii ya Lubuva sababu upinzani TZ umekufa!Sana sana watu wakianza kudai katiba mpya Lowassa ataibuka na kusema hataki siasa za kiuharakati
CCM imeisha shinda easily 2020
 
Sijakukatalia kuwa mfumo hauko sawa ki ushindani sasa wapinzani wameridhika nao ndio maana wanakubali kuingia kwenye uchaguzi kila wakati la sivyo tuseme hatuna upinzani wa kweli.

Upinzani umekufa
Kama hata UKUTA umewashinda kwa vitisho uchwara wataweza kudai katiba mpya inayo kuja na mikiki mikiki ya mapambano na vyombo vya dola?
Lowassa na Sumaye wameua sana upinzani!
 
Sielewi kwanini wapinzani wamekuwa waongo hivi, kila uchaguzi wanadai wameibiwa kura kwa sababu ya kukosa tume huru ya uchaguzi, lakini sijawahi kuona juhudi zozote zinazofanya kuhakikisha nchi imepata tume huru ya uchaguzi.

Pia sijui kwanini wanakubali kuingia kwenye uchaguzi huku wakijua kuwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Wapinzani mtadai lini tume huru ya uchaguzi?
Nani kukuombea Tanzania kuna upinzani? Tume huru kwa maana gani wakati Tanzania tuna chama kimoja kilichojigawa kwa majina tofauti
 
Nani kukuombea Tanzania kuna upinzani? Tume huru kwa maana gani wakati Tanzania tuna chama kimoja kilichojigawa kwa majina tofauti

Umpingea ukweli kwa sababu hata tukisema vyama vyote vya upinzani visusie uchaguzi hawa jamaa wanaweza wakaunda vya vingine ili kupata ushahidi kwa uchaguzi ulikuwa wa kidemokrasia.
 
Wapinzani hawataki Tume ya Uchaguzi Huru zaidi ya kutaka waingie Ikulu.

We unaona watu kila siku wanasema Ikulu Ikulu!! Ikulu Ikulu!

Kuna watu wa kuona mbali hapo?
 
Back
Top Bottom