Nimeshangaa kidogo. nimesoma kwenye gazeti moja habari za Kingunge Ngombale Mwiru anajaribu kufurukuta kujitetea mbele za watu. Hii inaweza kumletea mwisho mbaya. Nashangaa kwa nini asinyamaze. najua akinyamaza siku akiibukia pazeri hakuna atakayekumbuka upuuzi alioufanya.
Nikafikiri kuwa Siasa maana yake ni kuziba masikio na kufungua mdomo? tangu Kingunge alipojitokeza kwa mara ya kwanza kuwa mpambe wa Mtangaza nia, bila kujali yuko nyuma ya nani watu tulimkosoa sana. Maneno yote yaliyosemwa juu ya mwenendo wake huo bado hajasikia? Ameziba masikio? Anapanua mdomomkusema? Hana mshauri? Eti anatishia kuihama CCM?
Kuna watu wangapi wa kumfuata Kingunge? au anasubiri 'Mzee' akiamua naye afuate? Hivi anayoyasema kama Lowasa angepitishwa kwenye bora tano angeweza kuyasema? Hivi bado haoni sababu za mchakato kuwa kama ulivyokuwa ili kukinusuru chama?
Kama angekuwepo wakati wa Pilato angelifungulia jambazi la Baraba kwa kisingizio kuwa watu wengi wamemtaka? Ninamshangaa kwa kuwalaumu 'wazee'. Akina Mkapa, Karume, Mwinyi. Anasahau kuwa alistahili kuwa mmoja wao. Alistahili kuwa nao akikisaidia Chama alichokianzisha kiendelee kuheshimika kikiwa madarakani au nje ya madaraka (maana lazima siku moja kitatoka madarakani'.
Kingunge hana mshauri? Anamshauri nini? Ngoja niseme mambo mengine yasiyohusiana na mada hiyo hapo juu.
1) Uzee mara nyingi huonekana kwenye makunyanzi ya ngozi, na kutembea na mkongojo. Hauonekani kwenye fikra. Ndiyo maana watu wanaoshika mikongojo huendewa na kutakiwa kutoa mawazo yenye busara.
2) Siku moja Tembo alikuwa anavuka daraja. Kwa jinsi daraja lilivyokuwa na uzito wa tembo likawa (daraja) linatingishika. Baada ya tembo kuvuka akasikia nzi anasema 'kidogo tulivunje daraja'. Kumbe alikuwa mgongoni mwa Tembo wakati 'wakivuka' daraja.
Nakipongeza Chama Cha mapinduzi kwa kulivuka daraja la kwanza. Kumtafuta mgombea. Haikuwa kazi ndogo, pia namuasa mzee kingunge ulitakiwa kuwa kama kina mzee warioba, Dr. salim Ahmed Salim, Butiku, na wengineo amabo hakuwa na kambi.
Vile vile mzee kingunge yakupasa kujua kuwa unapoandaa watu wa kukushangilia ujue na wenzako wataanda watu wa kukuzomea tu na hivyo ndivyo ilivyotokea leo hii watu wote watakupuuza