Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Magamba mwaka huu mtagawana fito Kingunge ameanza ngoja Lowasa mwenyewe afunguke ccm ipasuka vipande-vipande Pasco umemsikia Kingunge?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu NTOBI ni afadhari wanaojua huu UFA na makada tu pamoja na baadhi ya wasomi. lkn kama wapiga kura wa vijijini wanhekuwa wanajua haya, basi ilikuwa CCM kwisha. Bado wana bahati hii.
 
Ndio madhara ya kuchakachua maoni ya wananchi.. Nafikiri amepata fundisho.
 
Mtu ukipewa pesa lazima uitolee maelezo ya matumizi. Ndilo analofanya Ngombale. Ana justify pesa ya Lowassa.
 
Kwenye hatua ya kwanza huwa hamna kupiga kura majina yote yanachukuliwa na kuangaliwa moja baada ya jingine na wale wote wenye tabia mbovu mbovu na ambao Tume ya maadili inaona hawafai huwa majina yao hayarudi, wale ambao majina yanarudi ndio hupigiwa kura sasa, nilivyoelewa mimi!

Ndo uhuni wenyewe huo sasa unaopelekea watu kuenguliwa kiajabu ajabu tu.

Mtu kama Amina Salum Ali anapita anaenda hadi tatu bora halafu watu makini kama Mark Mwandosya na Agustino Mahiga wanaenguliwa bila hata kujua ni kwa sababu zipi.

Kwa nini hayo majina yote 38 yasipigiwe kura na kuchukua watano waliopata kura nyingi na kuendelea na utaratibu huo hadi kumpata mtu mmoja?

CCM ni wahuni hadi wanafanyiana uhuni wao kwa wao na wakiunda serikali wanauendeleza uhuni wao kwa wananchi.
 
Maneno ya wakosaji! Mbona wao wamefanya sana fitna kwa wengine? Tunasubiri Oktoba 25 tupige kura.
 
Kingunge anasahau kamati iliyomchinja lowassa ndio iliyomchinja malecela akiwa makamu mwenyekiti wa chama taifa na yeye kingunge hakupaza sauti kumlilia!

Kinachoonekana sasa ni mbinu mbadala ya kundi LA mafisadi wanaomzunguka lowasa kutaka wasisahaulike kwenye utawala mpya

Pia kasahau kutuambia yeye na mwalimu walitumia busara gani kumfunika lowassa!
 
kwa kifupi sana


wakati wa kikao cha maadili kujadili report za watia nia kusomwa membe na lowasa wote walikatwa majina ...report zao zilikuwa mbaya sana..tena mbaya mno...ila ya lowasa ilikuwa mbaya zaidi kuliko.....mtu aliyeongoza kwa kuw ana alama za juu kwenye maadili ni Makongoro,magufuli, makamba, migiro na huyo amina... kamati ikaazimia kuchuku majina hayo kwa sababu walizozijua wao...baada ya mda mweneyekiti akaonekana kutoridhika na hiyo tano bora..akamwita mstaafu wa awamu ya tatu na ya pili na pia kina malecela...akalamimika kuwa tano bora yote imejaa watu ambao wao wazee wastaafu waliwataka..yeye kama mwenyekiti hana mtu...iweje tano bora awe na mtu mmoja tena mwanamke..mvutano kidogo ukatokea...mwenyekiti akapewa uhuru wa kuamua anachotaka...ndipo akasema namuondoa mmoja na kuweka mwingine...akaliondoa jina la Makongoro na kuweka la membe..wazee wastaafu wakashangaa sana ...ili amani ya yerusalemu iendelee kudumu wakakubaliana na mawazo ya mwenyekiti japo kwa shingo upande...
wakarudi chumba cha mkutano wakawaeleza wajumbe wa maadili juu ya mabadiliko hayo ...minong'ono ikatokea mle ndani..gafla mwenyekiti akafunga kikao.... na kutoka na hiyo tano bora iliyochachuliwa kwa kuondolewa makongoro na kumwingiza membe...hii ni kwa kifupi sana hivyo ndivyo ilivyokuwa...badae huko mbele nikipata mda ntaeleza kwa nini lowasa alikatwa tena kwa kutumia ''collecting ink''...
 
Maneno ya wakosaji! Mbona wao wamefanya sana fitna kwa wengine? Tunasubiri Oktoba 25 tupige kura.

Hata huko kupiga kura ni kutimiza wajibu wa kujisumbua tu maana tayari Magufuli ndo rais anayesubiri kuapishwa.

Usitegemee kabisa Jaji Lubuva amtangaze mgombea tofauti na Magufuli kuwa ndo mshindi wa urais.

Hiyo tume ya uchaguzi ni tawi la CCM.

Si wenyewe mmeona mwaka huu yule Jaji mkuu wa zamani Agustino Ramadhani alitangaza nia kupitia CCM?

Yule mwaka 2010 si ndo alikuwa makamu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi chini ya mwenyekiti Lewis Makame..?

Hiyo tume ya uchaguzi ni makada wa CCM tu na jukumu lao kubwa ni kulinda maslahi ya chama kwanza.
 
Mzee amelalamikia taratibu kutofuatwa ........ hajalalamikia Lowasa pekee kukatwa .....
Mkuu mbona waliochukua form walikuwa wengi wakiwemo Mh.Membe,Mwigulu,Nyerere nk. Mbona muda wote alikuwa anahudhulia mikutano ya Lowasa na kumpigia debe na kujaribu kumtetea kwa hoja za kulazimisha tu!! Tusijidanganye hapa atetei cha kanuni wala nini sijui, kakasirika baada ya mteule wake kukatwa hana jingine analotetea hapa ni unafiki tu, Baba wa taifa angefufuka leo hii angemshangaa mjamaa mwenzake damu damu, sio Kingunge tunayemjua sisi kabadirika kabisa!
 
Mfumo wa ccm ni mbovu na Dr wao kila akifanya dili akishtukiwa huwa anakimbia nje na kwanza anatunga tukio kama la juzi ili kupoteza watanzania kisha anakimbia haibu.sasa yuko swiss.

swissme

lipi hilo,lile la majambazi wa ukonga stakishari?.dah!!....
 
Mkuu mbona waliochukua form walikuwa wengi wakiwemo Mh.Membe,Mwigulu,Nyerere nk. Mbona muda wote alikuwa anahudhulia mikutano ya Lowasa na kumpigia debe na kujaribu kumtetea kwa hoja za kulazimisha tu!! Tusijidanganye hapa atetei cha kanuni wala nini sijui, kakasirika baada ya mteule wake kukatwa hana jingine analotetea hapa ni unafiki tu, Baba wa taifa angefufuka leo hii angemshangaa mjamaa mwenzake damu damu, sio Kingunge tunayemjua sisi kabadirika kabisa!

Hata kama hatetei kanuni lakini bado anachokisema ni cha msingi.

Mchakato wa CCM hata mimi nisiyewapenda niliuona ni wa kijanja kijanja.
 
Hata Kingunge mwenyewe ni batili. Mtu gani haamini wala biblia takatifu wala Quran tukufu. Tunajua kwa nini anashabikia hiyo kambi sababu ni kwamba mwanaye Kinjekitile ni msafirisha madawa ya kulevya mkubwa. Na katika wagombea ambao wangemsaidia wasimkamate mwanae ni Lowassa tu kwa sababu naye ni Fisadi.
kumbe Kinjekitile ni mtoto wa kingunge?halafu kumbe anauza madawa ya kulevya ndo akili zake hazipo kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Kosa kubwa alilofanya Kingunge ni Kuonyesha kwa wazi ni mtu gani alitaka awe kiongozi!Hakutendea haki wanachama wengine waliojitokeza....Kama Mwinyi,Mkapa na Kikwete wangejitokeza hadharani na kutangaza wagombea ambao wanawapenda Chama kingegawanyika kabisa...kutokana na hilo Kingunge anakosa sifa ya kuzungumzia mchakato wa uchaguzi kwa kuwa watu wanafikiri anatoa haya maelezo kwa sababu mgombea wake alienguliwa...amepoteza sifa ya kuwa mshauri katika kwa chama kwa sababu yuko biased...Hii ndo siasa pale karata zinapochangwa vibaya!
 
Kingunge ni mtu wa jk,anacho kifanya hapo ni kumhadaa lowasa na kumpoza ili atulie hio ni fitna yetu ccm na kingunge ndo mpikaji mkubwa, ccm ni zaidi ya chama.
 
Leo Mzee Kingunge kaongea na Vyombo vya Habari, ameanza kwa kupinga mfumo uliotumika kuwachuja wagombea wa urais kupitia CCM.

Kingunge amesema "Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu ktk kuwajadili wagombea"

Amesema Kamati ya Maadili ya safari hii imefanya kazi isiyowahusu kikatiba - kukata majina ya wagombe.

Kingunge amesema Kamati ya Maadili ya CCM yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama.

Amesisitiza Kamati ya Maadili haikuwa na madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.

Kwa mujibu wa Kingunge, Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.

attachment.php

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akiongea na waandishi wa Habari - Julai 15, 2015

Kingunge amewapongeza sana kina Kimbisa, Nchimbi na Sophia kukataa maamuzi ya Kamati Kuu, waliisamamia Katiba ya Chama.

Kingunge anadai CCM ni chama cha wanachama wote, taratibu na kanuni zikipuuzwa na kufanya vitu kwa maamuzi ya kikundi fulani.

Kwa mujibu wa Kingunge, kwenye vikao vya CCM Ulifanyika uhuni na dharau kwa wanachama wengine. Wakubwa waliopewa madaraka wanaona hakuna lolote tunaloweza kufanya ila mimi nitasema.

Kingunge anasisitiza, Kilichofanyika Dodoma hakikuwa sawa, Kamati Kuu iliporwa kazi yake, hii ni dharau kwa wanachama na wagombea wote.

Anasema Kamati Kuu ya Taifa CCM, ipo chini ya Halmshauri Kuu ya Taifa yenye madaraka ya kujadili mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu; na Halmshauri Kuu ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu, lakini utaratibu huo haukuwepo.

"Nawaheshimu sana Mzee Mkapa, Mwinyi, na Karume, lakini nasikitika waliotoa michango ya kutotoa haki kwenye Kamati Kuu. Waliogombea 1995 walikuwa 16, Kamati Kuu iliwasikiliza na kuandaa orodha ya watu 6," alisema Kingunge.

"Tulipofika NEC - wajumbe wakasema mbona Jina La Lowassa halikuwemo, mjadala ulikuwa mgumu, watu walisema lazima aingie kwenye orodha. Kwa mara ya kwanza muundo wa Chama ulikuwa tested baada ya wajumbe kutaka jina la Lowassa kwenye orodha ya majina 6,” aliongeza Kingunge.

"Mimi na Mwalimu tulishangaa kuona Lowassa anakubalika kiasi kile, Wajumbe wa Kamati Kuu walikuwa kimya na kushindwa kutetea mapendekezo yao. Mwalimu na Mimi ikabidi tuingilie kati na kusaida K'Kuu, tulifanikiwa kuwashawishi wajumbe wa NEC na wagombea wakaanza kujieleza," aliendelea kuongeza.

Kingunge ameendelea kudai kuwa, wote wakati huo walikubaliana kwamba NEC ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo ya Kamati Kuu.

"Safari hii tumeona wazi kwamba NEC yote msimamo wao ulikuwa wazi, lakini haikutumika busara, vitu vikaenda kama vilivyopangwa na “KITENGO”. KITENGO kilitoa maelekezo ya kumzuia Lowassa asipate haki yake ya msingi ndani ya Chama.

"Kuna watu wananiuliza kwamba Lowassa Fisadi, na wewe mzee unamuunga mkono, sasa ningependa kusema hivi:

"Hadithi ya Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa ya Richmond. Kamati Teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo sana, na hatimaye kwa kulinda heshima ya serikali na chama akajiuzulu.

"Lowassa sio kwanza kuwajibika kisiasa, ktk awamu ya kwanza ya Mwalimu - kuna viongozi wa kisiasa waliuzulu. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Usalama Taifa wote walijiuzulu kisiasa na Mwalimu aliwashukuru kwa kuwajibika.

"Lowassa alijiuzulu kuwajibika kisiasa, lakini ikabadilishwa kuonekana ni yeye ndiye aliyefanya makosa, ndio ukaanza wimbo wa ufisadi. Serikali yenyewe ilimsafisha kupitia TAKUKURU, lakini wimbo wa ufisadi ukaendelea, wakaja na wimbo mwingine wa Gamba.

"Yote haya yalipangwa na 'KITENGO' kilichoandaa kashfa ya Richmond. Edward ana historia ndefu ndani ya Chama.” aliendelea mzee Kingunge.

Kwa mujibu wa Kingunge, Wilaya ya Monduli ni moja ya wilaya ambayo mambo ya Chama yanaenda vizuri sana, na Kinana alimsifu Lowasa kwa hilo kuwa amekitumikia chama.

Kingunge anadai Lowassa amekuwa mtendaji mzuri hata serikalini, kila sehemu aliyopitia alionyesha namna alivyoweza kushughulikia matatizo ya wananchi.

Anadai mradi wa maji wa Ziwa Victoria, walishindwa wakoloni lakini limewezekana chini yake Lowassa akiwa waziri wa maji.

Amesema Lowassa kila alipoenda amefanya vizuri, na huu mchakato huu wa juzi ndani ya CCM umeonyesha wazi Lowassa anapendwa na watu.

"Zipo hadithi za kijinga kwamba watu wanaojitokeza wamepewa pesa, ni mawazo ya watu waliofilisika. Watu wanamlilia Lowassa hawamjui, hizo zote pesa zote anatoa wapi? Ana kiwanda cha pesa - hata angekuwa Bakheresa asingeweza!” alisema mzee Kingunge.

Mzee Kingunge alisema Lowassa ana kila sifa ya kuwa Rais na mwenyekiti wa Chama, mwingine yeyote inabidi ajifunze sana haya. Akasisitiza kuwa 'Uongozi wa Chama na Nchi umetumia nguvu kubwa sana kupuuza wananchi wanataka nini na kuhakikisha wanayempenda hapati kitu.

"Yalitokokea Dodoma yametia doa kubwa ktk historia ya Chama chetu chenye kuheshimika sana nje na nchi kiujumla. Nchi ili itengamae lazima chama kinachoongoza kijiendeshe kwa misingi ya haki na demokrasia, yaliyojiri Dodoma yametia dosari kabisa. Yaliyotokea Dodoma ni uvunjani wa misingi ya haki - wagombea walipaswa kusikilizwa kwenye Kamati kuu, walivunjiwa heshima na kunyimwa haki…” alisema mzee huyo.

"Chama kilichofanya maamuzi ya Dodoma hakikuwa chama kinachozungumziwa kwenye Katiba. Nawaomba viongozi wetu warudi kusoma ahadi za mwanachama, warudi pia wasome utangulizi wa katiba ya CCM. Kilichotokea Dodoma hakikubaliki, si halali na si haki.” alisema mkongwe huyo ndani ya CCM.

Kwa mujibu wa mzee Kingunge, pamoja na haya yote lakini Chama lazima kiendelee. Amesema CCM imempata mgombea, ndugu Magufuli, maneno yake ya leo hayamhusu yeye, yeye hakuwepo ktk 'KITENGO' cha kuharibu mambo.

Mzee kingunge ameongeza kuwa Lowassa yupo tayari kushirikiana na Chama kusaidia Chama kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu, lakini yaliyotokea lazima yazungumzwe kwa uwazi ndani ya vikao vya Chama ili watu watoe madukufuku yao.

Kingunge anadai Mkutano Mkuu umetamka Mgombea ni Magufuli, lakini ili kupata ushindi - chama kitahitaji nguvu na ushirikiano wa ndugu Lowassa na kuongeza kuwa anaamini Ndugu Magufuli atafurahia suala hilo na ataandaa mazingira mazuri ya kuipata sapoti hiyo.

Anadai Kabla ya Uchaguzi inabidi CCM kufanya mazungumzo ili wakubaliane na kukosoana lakini mwisho wa siku watoke tukiwa wamoja ili kupambana na adui.

Mzee huyo amedai Lowassa pia aliwashinda wote waliomtaka kuvua gamba na akaendelea kubaki ndani ya Chama.

Kingunge ameulizwa wakati wa Richmond alikuwa mbunge lakini hakuonekana kumtetea Lowassa, kwanini? Amedai 'Vitu vingine havipaswi kusema hadharani, niliona mambo yameharibika, nikakaa na Lowassa nikamshauri awajibike kisiasa.’

Ameulizwa kama ana mpango wa kurudisha kadi ya Chama kuonyesha kutokuridhishwa na uvunjifu wa katiba ya Chama; akajibu 'Siku nikitaka kurudisha kadi yangu nitawaambia, mimi kadi yangu namba 8 na nilihusika ktk kuunda chama hiki, nikifikia maamuzi nitasema.’

Mwisho amemalizia kwa kusisitiza: “Yaliyotokea Dodoma si halali na si haki…”

Asanteni
Hiki kizee ni kinafiki sana. Mbona hakikulalamika rafu iliyofanywa kwenye bunge la katiba ambamo yeye alikuwa mganga wa kienyeji?
 
Lowasa angeingia top 5 ndiye angepita...!!! na asingeweza chochote kuongoza hii nchi zaidi ya malumbano, kumkata juu kwa juu ilikuwa ni sahihi, na kumpiga teke membe ilikuwa sahihi ili kuequalize wote waliokuwa na magroup (na hizo ni hekima za mkapa) ...wagombea wenye uwezo wa kuongoza hii nchi walikuwa wawili tu ndani ya CCM ambao hawaangalii uso wa mtu kwenye utendaji kazi...MAGHUFULI na MWAKYEMBE.
 
haya sio mambo ya kudharau, kwa kuwa hakuna mwingine wa kutoa haya.! Kwa kweli anajiamini..! Ndio tunataka watu wenye msimamo kama wa huyu mzee..!
#Bg Up

Ni kweli mawazo ya kingunge ni sahihi kichama kwa sasa kuliko binadamu yeyote aliyewahi kuumbwa chini ya jua. Yeye ni miongoni mwa watu watatu walio-design na kuandika katiba ya CCM, anaielewa katiba sawa na mimi ninavyoielewa Biblia.
 
Ndo uhuni wenyewe huo sasa unaopelekea watu kuenguliwa kiajabu ajabu tu.

Mtu kama Amina Salum Ali anapita anaenda hadi tatu bora halafu watu makini kama Mark Mwandosya na Agustino Mahiga wanaenguliwa bila hata kujua ni kwa sababu zipi.

Kwa nini hayo majina yote 38 yasipigiwe kura na kuchukua watano waliopata kura nyingi na kuendelea na utaratibu huo hadi kumpata mtu mmoja?

CCM ni wahuni hadi wanafanyiana uhuni wao kwa wao na wakiunda serikali wanauendeleza uhuni wao kwa wananchi.

Bado sijaelewa kuhusu yule Jaji Augustino Ramadhani ambaye tuliaminishwa kwamba hana kashfa je ni ithibati gani zilizotumika kumdhalilisha kiasi hiki? Na wale waliomshawishi kuchukuwa fomu wanajionaje?

Jaji hadhi yake imeshuka sana na hiki ni kiburi na uroho wa madaraka alionao kutoitambuwa hadhi ya Jaji. Hili ndio jinga kuliko wote.
 
Back
Top Bottom