Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
Hapo wadau wanao muita Gaidi basi atakuwa wa ajabu sana kuwaacha Raia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo wadau wanao muita Gaidi basi atakuwa wa ajabu sana kuwaacha Raia.
Vipi mkuu, ulikua unamuwazia nani kwani?Unataka nipotezwe?
Kumbuka nafahamika
Wadau wanasema ni mwana CCM.Hivi hizi sare za CCM ni kwamba ni mwanachama wa CCM au ni fake?
Pamoja na yote yaliyotokea hakustahili kufaGuys I am informed there’s a guy shooting randomly near Stanbic Bank, anyone with more news?
Inadaiwa kuna watu wameuawa. Ni Karibu na Makao Makuu ya Stanbic.
========
Mtu mmoja ambaye alionekana kufyatua risasi karibu na Ubalozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam amedhibitiwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, (IGP) Simon Sirro amethibitisha kuuawa kwa askari wawili kwenye mapambano ya kurushiana risasi yaliyotokea eneo la Daraja la Salenda jirani na Ubalozi wa Ufaransa, Dar es Salaam.
Tukio hilo limetokea leo Jumatano Agosti 25, 2021 baada ya mtu mmoja ambaye hajafahamika kuzua taharuki baada ya kufyatua hewani risasi huku akisikika akisema kuwa anawatafuta polisi.
Akizungumza katika kikao kazi cha maofisa wa polisi, Sirro amesema mtu huyo naye ameuawa kwa kupigwa risasi.
“Mmeziona clip zinaruka sasa hivi akaingia barabara kubwa akawa anatamba na SMG na yeye amepigwa risasi na askari wetu hivyo, askari wetu wamefariki na yeye amefariki” amesema IGP Sirro.
Ameeleza kuwa wanaendelea kufuatilia kufahamu mtu huyo ametokea wapi na baadaye watatoa taarifa kamili.
IGP Sirro amenukuliwa kupitia kipande cha video kilichorushwa kwenye mtandao wa kijamii wa Wasafi Fm.
PIA SOMA:
1. Mashuhuda wasimulia tukio la aliyekuwa akipiga risasi
UPDATE: Waliouawa ni Polisi Watatu na Mlinzi mmoja, wengine sita wajeruhiwa.
Jeshi la Polisi limesema idadi ya Watu waliouwawa na Mtu mwenye Bunduki aliekua akifyetua risasi ovyo karibu na Ubalozi wa Ufaransa Dar es salaam ni Watu wanne huku kati yao Watatu wakiwa ni Polisi na mmoja ni Mlinzi wa Kampuni binafsi ya ulinzi.
"Leo August 25 2021 tumekutwa na tukio baya kabisa, tukio la kihalifu ambalo limepoteza maisha ya Watu wanne na watatu kati yao ni Askari Polisi, limetokea katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni Askari wetu walikua kazini akatokea Mtu akawashambulia kwa Bastola na alipowashambulia na kuanguka alichukua Bunduki za Askari hao na kuanza kurusha risasi ovyo kuelekea Ubalozi wa Ufaransa"
"Ukiachia Watu wanne waliouwawa leo tuna Watu 6 ambao wamejeruhiwa kwenye tukio hili na wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, taarifa zaidi tutaendelea kupeana kadri muda unavyokwenda, ni mapema sana kubaini kwanini alifanya vile lakini tumeshaanzisha Timu ya upelelezi na muda sio mrefu tutakamilisha"
"Kuhusu baadhi ya video kusema kwamba huyu Mtu ni Mkazi wa Upanga sisi hatuthibitishi mambo kupitia clips za video, tunathibitisha mambo kupitia upelelezi kwahiyo upelelezi ndio utakaoeleza, kuhusu swali la Waandishi kuhusu kuwepo kwa dalili zozote za ugaidi kwenye tukio la leo hatuwezi kusema chochote hii ni mapema lakini uchunguzi ndio utakaosema kama kuna ugaidi au hakuna ugaidi"
"Kwa sasa hatuwezi kusema amekutwa na kitu gani mfukoni, Polisi bado wapo eneo la tukio... ni mapema sana kusema amekutwa na nini kwasababu Wataalamu wapo kazini, kuhusu kama ni Raia kama sio Raia uchunguzi ndio utasema baada ya upelelezi kukamilika tunachojua sasa huyu ni Muhalifu"
UPDATES: Polis wafika Upanga katika nyumba aliyokuwa akiishi Hamza
kutoka Upanga Dar es Salaam kwenye nyumba aliyokua akiishi Hamza, Mwanaume aliyefyatua risasi na kuwauwa Watu wanne leo Jijini Dar es salaam ( Askari Polisi watatu na Mlinzi wa Kampuni binafsi mmoja).
Polisi wameifunga nyumba hiyo na kuondoka na Ndugu wa Hamza kwenda nao Polisi usiku huu ambapo walifika hapa toka saa kumi na moja jioni, endelea kukaa karibu na AyoTV na Youtube ya millardayo kufahamu zaidi.
olisi wameifunga nyumba aliyokua akiishi Mwanaume aliyefyatua risasi leo na kuuwa wanne Dar es salam, baada ya kuifunga nyumba hii iliyopo Upanga Dar es salaam wameondoka pia na Ndugu wa Mtu huyo aitwae Hamza kwenda nao Polisi usiku huu pamoja na Pikipiki aliyokua akiitumia.
Hamza amekua gumzo leo hii Dar es salaam baada ya kuwaua kwa risasi Watu wanne leo na kujeruhi wengine sita, endelea kukaa karibu na Youtube ya millardayo kufahamu zaidi.
View attachment 1907510
View attachment 1907511
View attachment 1907519
Hii ni developing news…
Kuna mtu mmoja, kapigwa risasi na kuanguka katikati ya barabara
View attachment 1907602
View attachment 1907621
View attachment 1907645View attachment 1907646
Huyu anadaiwa kauawa.
What’s the source of this intelligence??
Na watu walioanza kuwaza kadi ya CHADEMA ilikua vipi?Wadau wanasema ni mwana CCM.
Lakini nafikiria kwani CCM na tukio kunauhusiano?
Kitu kikiwa mtandao maamuzi yanakuwa kwa wengi.Na watu walioanza kuwaza kadi ya CHADEMA ilikua vipi?
Tuepuke kujaji mambo mapema mkuu. Mbona wengine walianza kuhusisha na CDM kwa kadi fake? Nadhani unanipata mkuu.Wadau wanasema ni mwana CCM.
Lakini nafikiria kwani CCM na tukio kunauhusiano?
🤣🤣🤣 Amekuweka wewe wakati muhusika washamubainiMwanzisha Uzi ondoa Jina langu kwenye heading. Mimi sijauawa. Na wala sikuwepo jana. Nielewe please. Unanisababishia usumbufu kwa ndugu zangu.
Hata mimi nilianzisha uzi kupinga hayo.Tuepuke kujaji mambo mapema mkuu. Mbona wengine walianza kuhusisha na CDM kwa kadi fake? Nadhani unanipata mkuu.
Hata mimi nilianzisha uzi kupinga hayo.Tuepuke kujaji mambo mapema mkuu. Mbona wengine walianza kuhusisha na CDM kwa kadi fake? Nadhani unanipata mkuu.
Sawa mkuu. Hata sasa baada ya kijulikana kwamba ni mwanachama wa CCM, nadhani haifai kuhusisha chama chake, jambo libaki kwa mhusika mwenyewe. Watu waache ushabiki wa mambo ya kisiasa. Nadhani hili litawafunza watu baada ya mhusika kujulikana ni mwanaCCM tofauti na walivyoanza hadi kufake kadi ya CHADEMA. Ni hayo tu mkuu.Hata mimi nilianzisha uzi kupinga hayo.
Watu tulianza kuhukumu mapema sana.
Hii habari ingefikia mkononi mwa mkenyaLabda wanaweza kusaidia kwenye upelelezi.
Kweli kabisa mkuu hata mimi nilieleza hivyo.Sawa mkuu. Hata sasa baada ya kijulikana kwamba ni mwanachama wa CCM, nadhani haifai kuhusisha chama chake, jambo libaki kwa mhusika mwenyewe. Watu waache ushabiki wa mambo ya kisiasa. Nadhani hili litawafunza watu baada ya mhusika kujulikana ni mwanaCCM tofauti na walivyoanza hadi kufake kadi ya CHADEMA. Ni hayo tu mkuu.
Eneo la ubalozi linaishia kwenye uzio wao.Popote duniani Ardhi ulipo ubalozi ni nchi nyingine
Ulipo ubalozi wa ufaransa ni nchi ya ufaransa
Askari waliokuwepo waliouawa walikuwa kwenye ardhi ya nchi ya ufaransa eneo la ubalozi wa ufaransa Tanzania
Hamza ni gaidi sababu alirusha risasi na kuua watu waliokuwa kwenye ardhi ya nchi ya ufaransa polisi watatu na mlinzi mwingine wakiwa nchini ufaransa na risasi zikatua nchi ya ufaransa
Ni gaidi sababu kavamia nchi ingine na kuvurumisha marisasi hivyo ni gaidi