kitali
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 5,204
- 8,315
Wana JF
Niko hapa Kinondoni Makaburi, kuwaletea pumziko la milele la mwana JF, Mzalendo Sanctus Mtsimbe.
View: https://www.youtube.com/live/PA4ndBZNpIE?si=EeOI7LGNCd2OU0J2
Tangu nimejiunga JF ile 2006, hii ndio mara yangu kwanza kuja kumzika mwana jf makaburi ya Kinondoni.
Toka msiba imetokea sikuwahi kuuliza cause of death, ila nilipoelezwa, nimemnyanyulia Mtsimbe mikono juu, huyu ni bonge la shujaa wa uhai hadi kifoni, kumbe alikuwa anakabiliwa na changamoto qya kiafya ya ugonjwa ambao ni terminal, hivyo alikuwa unaupigania uhai wake kimya kimya, na hakuwahi kuutaja na wala hakuwahi kuonekana with sick face, aulibeba ugonjwa wake moyoni mwake kimya kimya hadi amekufa kishujaa.
Kwa vile akiwa hai, mwenyewe hakuwahi kusema ana changamoto hiyo ambayo ni terminal illness, kwa heshima ya marehemu, naomba tuheshimu his right to privacy, hivyo naomba msiulize marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani, ila moja ya magojwa terminal, ila sio ugonjwa wa kuambukiza, na sio ngoma!.
Katika mabandiko yangu yaliyopita kumhusu Sanctus Mtsimbe, nilisema tuna fanana mambo mengi,
- Tribute to Sanctus Mtsimbe: Sio tu ni smart kwa mavazi na muonekano, pia ni smart kwa mawazo, maneno, na matendo, na very smart upstairs!
- Pumzika Sanctus Mtsimbe, Kazi Umekamilisha, Mwendo Umeumaliza. Asante Kutuachia Hazina Kubwa ya Maarifa Humu JF Tutakuishi Milele!. Pumzika
Leo msibani tumezidi kufanana, kumbe first wife yuko Marekani, na mini first wife yuko Marekani. Mtoto mkubwa alikuwa Marekani, na mimi watoto wakubwa wako Marekani.
Bongo akavuta kitu, dogo dogo, kitu white, chombo kweli kweli, mimi pia Bongo nimevuta kitu, white...
RIP Rafiki yangu Mzalendo Comred
Karibuni.
Paskali
Hahahaha hongera kutuwakilisha mkuu.